KCSE Past Papers 2020 Kiswahili Karatasi ya 2 (102/2)

Karatasi Ya 2 Maajibu

(a) Kwa kurejelea kifungu, fafanua matatizo manne yanayoweza kusababishwa na matumizi ya simu kwa familia. (alama 4)

i. Kunyamaziana/Upweke. Licha ya kuwa pamoja kila mtu anashughulika na simu yake.

ii. Kutofahamu kinachoendelea kwenye ujirani wao/Watoto Kutoskia mama yao.

iii. Ugomvi/hasira unaweza kuzuka baina yao. Mama anawakaripia watoto na kuwanyang’anya simu.

iv. Inaweza kumtenga mhusika/ wahusika na ulimwengu mpana – hawamwoni jirani.

v. Huweza kuwatumbukiza katika janga/mkasa k.v. moto./uharibu/hatari.

vi. Huzubaisha. Mtu kujisahau na kusema mambo yasiyotarajiwa – Mzee Mbula kuchekeshwa na yule bwana wa viroja.Watoto kutosikiza wazazi

vii. Italeta

sahau / kutowajibika / uzembe / ugomvi / kutofahamu / kutomakinika / mapuuza / utelekezaji

(b) Eleza mambo matano yanayoonyesha kuwa familia hii ina mshikamano. (alama 5)

i. Inakaa pamoja ukumbini/sebuleni.

ii. Mama Tola anataka kujua kinachomchekesha Mzee Mbula ili nao wapate kucheka.

iii. Kutokuwepo kwa ugomvi wowote pale nyumbani.

iv. Wanahusiana vyema. wanamlahaka mwema.

v. Mama Tola anamsikiliza Mbula na kufuata ushauri wake anapoelekea (Mama Tola) kukasirishwa na wanawe/mama anatii.

vi. Wote wanacheka kwa furaha Mama Tola anapocheka.

vii. Wote wanakubali kujifunza kutokana na tukio na kukubali kujirekebisha

(c) Fafanua uhusiano uliopo kati ya familia ya Mzee Mbula na majirani. (alama 2)

husiano ni mzuri – jirani anafika na kutaka kuingia ndani moja kwa moja.

kukakaa na wanawe

Kosomesha watoto

Anavyotamka Dah….

Usasa- mke mmoja/watoto wawili/familia noogo

(d) Thibitisha kuwa Mzee Mbula ni mtu anayejikuta baina ya usasa na ukale. (alama 2)

(e) Eleza maana za misamiati ifuatayo kwa mujibu wa kifungu. (alama 2)

Usasa – Anafahamu teknolojia ya kisasa; simu. Ukale- Anafahamu tamaduni fika na desturi anazijua kwa kina. Matumizi ya chungu. Matumizi ya maneno ya hekima/methali

i. Limejenga hema

Limejenga hema -limedumu/Limetamalaki/Limekuwa mtindo au mazoea/limekita mizizi/kuweko kwa muda mrefu/Limekaa au kimeishi/limesakini au limeselelea/limelea au limesehelea

ii. kuitapakaza

Kuitapakaza -kuieneza/kufanya iwe kila mahali/kuitandaza/kuiravagaza /kuizagaza/kusambaza/ kuitapakanya/ kuihanikiza / kuihinikiza.

(a) Kwa maneno 50, eleza visababishi vya ukame kwa mujibu wa taarifa. (alama 4; 1 ya mtiririko)

Matayarisho

i. Kipindi kirefu cha uhaba wa mvua hasa katika msimu mzima au zaidi.

ii. Visababishi vya ukame huwa shughuli za binadamu kama vile kukata miti. Hizi husababisha mmomonyoko wa udongo

iii. Kiangazi ambacho huongeza kiwango cha joto ambayo hufanya maji kugeuka mvuke haraka pia husababisha ukame.

iv. Hali ya el ninyo husababisha kiangazi katika maeneo yasiyokuwa na mvua na pia el ninyo hufuatwa na msimu wa kiangazi.

v. La nina

vi. Mabadiliko ya hali ya anga yanasababisha ongezeko la kiwango cha joto duniani.

Nakala Safi

i. Ukame husababisha kupungua kwa mimea na mavuno.

ii. Kuwepo kwa dhoruba za mchanga hasa katika majangwa.

iii. Ukosefu wa maji ya kunyunyizia husababisha njaa.

iv. Makazi ya wanyama huathiriwa vibaya.

v. Hali ya afya huzorota na kunakuwa na magonjwa kama vile utapiamlo.

vi. Kutokana na uhaba wa maji na chakula, ukame husababisha uhamaji, uhamiaji na ukimbizi.

vii. Kukwama kwa maendeleo ya viwanda kutokana na ukosefu wa maji/ukosefu wa maji huathiri maendeleo ya viwanda.

viii. Ukame husabisha ukosefu mkubwa wa maji.

ix. Kukosekana kwa umeme ambao huzalishwa kwa maji huwa tatizo kuu/ maji huhitajika kuzalisha umeme.

x. Kiangazi husababisha mizozo ya kijamii; watu huzozania rasilimali haba, hasa maji./uhasama wa kijamii.

xi. Kiangazi kikali husababisha kuenea haraka kwa mioto.Vifo vya binadamu na wanyama.Uharibifu wa rasilimali husababishwa na moto huo.

(b) Fupisha ujumbe wa aya ya tano hadi saba kwa maneno 70. (alama 6; l ya mtiririko)

i. Binadamu wanaweza kujikinga na makali ya ukame kwa kuhifadhi maji katika mabwawa.

ii. Kusafisha maji ya bahari kwa kuyatoa chumvi na kemikali ili yatumiwe katika shughuli nyingine.

iii. Kutumiwa wakati wa ukame/kukuza mimea.

iv. Kutafiti kuhusu hali ya anga ili kuweka mipango itakayosaidia.

v. Kuwa na mipangilio mizuri ya matumizi mazuri ya ardhi kama kubadili aina ya mimea inayopandwa itakayozuia mmonyoko wa udongo.

vi. Kupunguza matumizi ya maji hasa katika mazingira ya nyumbani.

vii. Kusafisha maji yaliyotumiwa nyumbani ili yatumike tena.

C.Matumizi ya Lugha

(g) Mvua isingalinyesha/isingelinyesha mapema tusingalivuna/tusingelivuna mazao mengi. Mvua isingenyesha mapema tusingevuna mazao mengi.

(h) Mgeni aliwasili tulipokuwa tunafagia njia / tukifagia njia.

(i) Mwenyewe – kiwakilishi / kiwakilishi cha peke/kijina/kibadala (w) hakuwa – kitenzi kisaidizi Ts / T amekupa – kitenzi kikuu

(j) “Mwanangu,” akasema Neema huku akimkazia macho, “huoni unamtia mwenzako wasiwasi?”

(k)

i. ukate / ulete / ubebe/mkononi/mguuni mtini / mtoni / mjini/mchezo

ii. hakiliki, hakiandikiki /hakisomeki

(l) Uongozi wa chifu huyo umesifika sana.

Vitabu kilicho kabatini kimeandikwa.

RH

Darasa lenye uchafu limeoshwa vizuri.

(m)

Ngoma hizo hazikuhifadhiwa (ili) ziuzwe mjini.

Ngoma hizo hazikuhifadhiwa (ili) zisiuzwe mjini.

Ngoma hizo zilihifadhiwa ili zisiuzwe mjini.

Ngoma hizo hazikuhifadhiwa wala kuuzwa mjini

(n) Bili alikuwa anawashauri /akiwashauri vijana kuhusu umuhimu wa michezo.

(o)

Alimnyesha Tindi pombe iliyomlewesha Alimlevya Tindi kwa kumnywesha pombe Alimnywisha Tindi kwa pombe ikamlewesha Alimnywesha Tindi pombe ikamlevya Alimnyesha pombe Tindi ili imleweshe

(Asitumie fanya).

(p) Vitabu vingine havistahili kusomwa na watoto wachanga (wingi)

(q)

Hamadi

heko / hongera / pongezi / kongole / huree /hario/ oyee

(r)

karimu

butu / pole/tamu/gutu/chigi

(s)

kabiliwa / tingwa / patwa / fikwa /zongwa/alizunguliwa (MNYAMBULIKO)/alitatizwa/alitanzwa/ alisibiwa/aliandamwa/alisumbuliwa/alisakamwa/alitaswa/alisibwa.

hakwenda nguu / hakufa moyo akidondosha sarufi

(t)

i. kamili

ii. -enye afya

iii. -enye uhai

iv. ondoa mwangaza

v. komesha

4. ISIMUJAMII: (Alama 10)

Umewahutubia wanaeneobunge lako kuwaomba wakuchague kuwa mbunge wao. Hata hivyo, umegundua kwamba hujafanikiwa kuwavutia upande wako.

Fafanua sifa kumi za lugha ambayo ungetumia kuwavutia.

Sajili ya hotuba za kisiasa (hoja 1 + maelezo 1)

i. Kutumia lugha ya kushawishi k.v mtoto wenu.

ii. Kujisawiri kama mtumishi wao – Tayari kuwatumikia

iii. Kuchanganya msimbo/hamishi/sheng’:Mimi ni hustler

iv. Kuwakashifu wanasiasa wenzako: watu wa vitendawili

v. Kutoa ahadi. – Nitajenga viwanja vya michezo.

vi. Lugha ya kujisifu.: Nimefanya mengi

vii. Matumizi ya chuku.:Nitaleta mifereji ya maziwa

viii. Maswali ya balagha ili kuwaaminisha.: Nani asiyenijua.

ix. Kutumia viwakilishi vya nafsi ya kwanza ili kuibua ukuruba. (Nita..).

x. Matumizi ya msamiati wa kisiasa. (kura) manifesto).

xi. Lugha ya kunyenyekea / kuomba. (Naomba) adabu/heshima

xii. Lugha yenye ucheshi.

xiii. Matumizi ya nyimbo.

xiv. Matumizi ya mafumbo, hasa ya kuwapigia vijembe wapinzani. – fisi

xv. Kujisawiri kama ndiye pekee anayeweza kuwaokoa raia kutoka kwenye matatizo/ changamoto/matumaini.

xvi. Anajisawiri kama anayewategemea.

xvii. Taharuki – Harusi ya kumakinika

xviii. Takriri/uradidi. xix. Lugha ya mdokezo – kuhusisha

xx. Lugha ya kudadisi/Maswali na majibu

xxi. Lugha legevu.

xxii. Matumizi ya misimu.

xxiii. Sentensi au kauli ndefu (maelezo).

xxiv. Kauli fupi.

xxv. Viziada lugha/ ishara.

xxvi. Matumizi ya michoro (mabango) Picha.

xxvii. Lugha chepesi.

xxviii. Lugha Sanifu.

xxix. Lugha ya porojo/propaganda.

xxx. Matumizi ya tarakimu.

xxxi. Matumizi ya utohozi. xxxii. Matumizi ya lakabu.

 

 

(Visited 212 times, 1 visits today)
Share this:

Written by