KCSE Past Papers 2017 Kiswahili Paper 3 (102/3)

2017 Fasihi Karatasi ya 3

Sehemu A: Fasihi Simulizi Majibu

Lazima (20 marks)

(a) “Huu ni wimbo wa sifa.” Thibitisha kauli hii kwa kutoa mifano mitatu kutoka kwenye utungo huu. (alama 3)

(i). Kuonyesha Mbwene kama aliye jasiri- aliwakabi1i_kwa kitali kikali.

(ii). Kumrejelea Mbwene kama shujaa asiyeshindWa- hawakujua kwamba mbele ya mhimili huu wetu Walikuwa vipora. (iii). Kumtaj aanayesifiwa kwa maj ina mbalimbali-Mbwene, Mwana wa Ngwamba, Upepo wa Kusi, Mhimili.

(iv). Kumsawiri kama bingwa wa kupindukia- Hakuwa na kifani.

(v). Kusifia ushindi//kitali alichopigana. Wagundi walijua Walikuwa na mwana wa Ngwamba/kwetu kukenda kicheko.

(b) Andika sifa tatu za jamii ya nafsi neni katika utungo huu. (alama 3)

(i) Ni wakulima- kurejesha vikataa.

(ii). Ni wafugaji kurejesha mifugo.

(iii). Utekaji nyara – kuwaokoa vipusa wetu.

(iv). Mazoea ya uchokozi/ kupigana vita- walikuja kwa ndimi zilizojaa matusi. . .aliWakabi1i Mbwene, nao wakalipiza.

(c) Huku ukitoa mifano, bainisha vipengele vinane vya kimtindo ambapo nafsineni imetumiwa kufanikisha uwasilishaji wa umngo huu. (alama 8)

(i). Matumizi ya vihisishi iIi_kuibua hisia/kusisitiza ujumbe — ah, ee

(ii). Usambamba -wali wakibeba sime -Wali wakibeba mata – Wali wakibeba mienge – kuirej esha hadhi yetu -kuirejesha mifugo yetu

(iii). Sitiari- Walivipora

(iv). Tashbihi — ja samaki kwenye dema

(v). Lakabu — Upepo wa Kusi.

(vi). Nahau — cha kufa na kupona -kitali kikali.

vii. Chuku- kupigana (N gwamba) kwa siku kumi bila kula wala kunywa.

(viii). Tanakuzi – kicheko — kilio

(ix). Miundo ngeu ya sentensi/ kufinyanga sarufi -wetu mabarobaro – matusi kutumwaiya (x) Inkisari- zilohimili, kukcnda.

(xi) TasWira- utungo unasawiri picha ya mapigano.

(xii) Matumizi ya mistari mishata ili kuibua taharuki- ya moto kutangazia. . .

(d) Tungo za aina hii zinaendelea kufifia katika jamii yako. Fafanua hoja sita utakazotumia kuishawishi jamii yako kukinga dhidi ya hali hii. (alama 6)

 

  • Kuwatambua mashujaa
  • Kurithisha utamaduni wa jamii
  • Ni kitambulisho cha jamii.
  • Hutumiwa kuwafunza vijana mbinuishi kama vile ujasm, kutoa maamuzi yafaayo. . .. shujaa anahitaji kutoa maamuzi kwa kuzingatia mahitaji ya jamii yake.
  • Hukuza uzalendo, jamii inaweza kuwatmnia Wanaosifiwa kama vielelezo vya uzalendo.
  • Hupitisha historia ya jamii, hivyo kuwafunza vijana kuhusu kwa mfano, maadui Wa jamii zao, vita vilivyopiganwa na mafanikio yaliyofikiwa.
  • Ni nyenzo ya kurithisha fani yenyewe ya uimbaji.
  • Hukuza ubunifu. Kadiri vijana wanavyosikiliza nyimbo za aina hii zikiimbwa, ndivyo wanavyojifunza mitindo mbalimbali ya utungaji na uwasilishaji. Hutumiwa kuonya dhidi ya matendo hasi kama vile usaliti/ huadilisha.
  • Ni njia ya kupitisha maarifa, kama vile ya kupigana vita.
  • Mtu kufahamu: ni lini atashambulia, ni lini ataepuka shambulizi.
  • Hukuza utangamano/ushirikiano.
  • Watu wanapoimba nyimbo hizi pamoja hujihisi kuwakundi moja linalomuenzi shujaa mmoja.
  • Ni njia ya kujibumdisha. Ni nyenzo ya kupitisha Wakati, badala ya kujiingiza kwenye vitendo visivyofaa.
  • . Hupitisha amali na tamaduni za jarnii. Desmri za jamii hutajwa katika baadhi ya nyimbo. Mtahiniwa anaweza pia kupendekeza njia za kudumisha kipera hiki. Baadhi ni:(i) Kuzihifadhi kwenye maandishi

    Kuzihifadhi kwenye kanda

    Kuzifanyia utafiti

    Mashindano ya tamasha za muziki

    Kuzifunza shuleni

    iii) Kuwahimiza vijana kuzitunga (6xl) Kutaja- ‘/2 Mfan0/ kueleza-‘/1 Tanbihi Mtahiniwa anaweza pia kuj adili hasara za kutourithisha utungo wa aina hii, akawa anaionya jamii yake dhidi ya kutourithisha.

    SEHEMU B: RIWAYA

    K. Walibora: Kidagaa Kimemwozea

    Jibu swali la 2 au la 3.

    2. “Lakjni waliogopa…waliogopa hata kuwa na uoga.”

    (a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)

    (i) Haya ni maneno ya mwandishi/msimulizi.

    (ii). Yanawarejelea raia ya Sokomoko.

    (iii) Wanaugulika kwa dhuluma za Mtemi mara tu baada ya kurithi mamlaka kutoka kwa Mzungu.(iv) Wanalalamika kwa min0ng’0n0 kwa vile Wanaogopa adhabu ya Mtemi.

    (b) Bainisha tamathali moja ya usemi ambayo imetumiwa katika dondoo hili. (alama 2)

    Chuku — kuogopa hata kuwa na uoga. Woga umepigiwa chuku.

    (c) Kwa kurejelea hoja kumi na nne kutoka kwenye riwaya hii, thibitisha kwamba raia wa Tomoko walistahili kuogopa hata kuwa na uoga‘ (alama 14)

     

  • Utawala wa mkoloni kunyakua mali ya Waafrika na kuwatefékezea kwenye sehemu duni 
  • Watu kuuawa na Mazungu na kumpwa kwenye Mto Kiberenge 
  • Ukatili Wa Mtemi — mauaji ya Chichiri Hamadi na Mama Imani.
  • Kutumia vyombo vya dola kukabiliana na upinzani. Anawatia Amani, Imani na Matuko Weye korokoni.
  • Wizi wa mali ya umma — Nasaba Bora kunyakua shamba la Chichiri Hamadi
  • Utawala wa kiimla — tunaambiwa ulimi wake ulitoa amrisho na cheche za moto (uk. 14)
  • Matusi — tunaambiwa ulimi wake ulitoa karipio na matusi. (uk. 14)
  • Kukiuka haki za watoto — Nasaba Bora anakitupa kitoto mlangoni pa Amani.
  • Kuachiwa majukumu — Nasaba Bora anampagaza Amani ulezi wa mtoto wake.
  • Upufuju wa maadili — Nasaba Bora kuhusiana kimapenzi na Insichana mdogo.
  • Wizi Wa kitaaluma — Majisifu kuiba mswada wa Arnani. Dhiki ya kisaikolojia — Amani kulazimika kuchimba kaburi la Mterni angali hai.
  • MtemikumpigaAmanikikati1ikwa shumma ambazo hajathibitsha Askari kumpiga Mama Imani kikatili na kusababisha kifo chake Majirani Wa Imani kutorntetea anapochomewa nyumba na Mtemi.
  • Kimya chao kinamhuzunisha Imani.
  • Serikali kuwatelekezea Wazee kamavile Matuko Weye kwenye ugonjwa na umaskini Usaliti wa kimapenzi.
  • Michelle kumwacha Major N00n/ Majununi. Maturnizi mabaya ya dawa.
  • Oscar Kambona anapatikana na bangi, anafungwa. Uchochezi ~ Wanafunzi wanamsingizia Amani kwamba kawachochea dhidi ya serikali, anafimgwa Kutoshughulikiwa kwa watoto wenye mahitaji maalum.
  • Majisifu kuwaona‘watot0 Wake kuwa mashizi.
  • Viongozi kutowahakikishia raia huduma bora za afya.
  • Pesa zilizotengewa uj enzi wa hospitali zinatumiwa vibaya; wanaishia kujenga
  • . zahanati.
  • . Nasaba Bora kulipa wcma kwa ukatili. Licha ya DJ kumletea barua, Nasaba Bora anakataa kumpeleka hospitali anapoumwa na jibwa lake.
  • . Unyanyasaji wa kijinsia Nasaba Bora anamwachia mkewe upweke; ati anakwenda kusuluhisha migogoro ya mashamba.
  • Ubakaji — Ben Bella ni mbakaji, ni sugu wa jela.
  • Wizi wa mitihani — wazazi wa Fao kumwibia mtihani
  • Mwalimu Fao kuhusiana kimapenzi na mwanafimzi wake. Anamtunga mimba.
  • Nasaba Bora kuwatoza raia kodi ili kumpelcka mwanawe ng’ambo
  • Nasaba Bora kuwafuta wafanyakazi kwa sababu zisizo na msingi kama vile kunadhifisha mazingira.
  • Nasaba Bora na Majisifu kuwalipa wafanyakazi mshahara duni
  • Wauguzi kutomtibumtoto wa kina Imani na Amani. Mtoto anakufa.
  • Nasaba Bora kumuua paka kikatili
  • Nasaba Bora kumtaliki mke wake na hali yeye arnekuea mzinifu
  • Bi Zuhura kutaka kuhusiana kimapenzi na kij ana md0go/ anataka kumhuj Lunu Amani.
  • Kuzorota kwa huduma za kiafya- DJ anatoroka kwenye zahanati kutafuta tiba ya kienyeji kwa kukosa rnatibabu humo.
  • Raia kutozwa kodi ili Nasaba Bora ampeleke mwanawwe ng’ambo.
  • Pesa zilizotengewa ufadhili wa masorno ya watoto maskini kutumiwa kuwasomeshea wa walio nacho kama vile Madhubuti.
  • Ufisadi- Mtemi kujitengenezea faili ili apate mali.
  • Hali duni katika vituo vya kurekebishia tabia. Seli katika afisi ya Mtemi ni choo. Ben Bella analalamikia hali duni huko jela.
  • Mwalimu Majisifu kushindwa kidhibiti uraibu wake Wa dawa licha ya elimu yake3. (a) “Usinivue nguo kwa macho yako wee!”

    Kwa kurejelea hoja kumi na mbili kutoka kwenye riwaya hii, thibitisha kwamba mzungumzaji anastahili kuvuliwa nguo. (alama 12)

    – Dondoo limetolewa uk. 21. Mtahiniwa aonyeshe mambo ambayo Nasaba Bora ametenda, ambayo ni ya aibu/dhuluma/ ya kumfanya ashutumiwe. Kuvua ng11o- kuona uozo/kuangaza uovu/kusutwa kwa uovu Baadhi ya hoja ni:

     

  • Mauaji — Nasaba Bora kumuua Chichiri Hamadi
  • Uzinzi – Kuhusiana kimapenzi na Lowela.
  • Kuwafuta Wafanyakazi kwa makosa yasiyo na msingi kama vile kunadhifisha mazingira Kuwapokonya Chichiri Hamadi na Mama Imani shamba.
  • Kuchoma nyumba ya akina Imani Kumpiga Amani kikatili Kudharau watu Wenye mahitaji maalum.
  • Anapogundua yule msichana ni kilema anahizika, hamtaki mapenzi tena.
  • Kumuua paka kikatili Kuwatoza raia
  • kodi kumpeleka mwanawe ng’ambo Kumwachia mkewe upweke; ati anakwenda kusuluhisha mi gogoro ya mashamba, anashindwa hata kutekeleza majukumu ya unyumba
  • Kumtupa mtoto wake kibandani mwa Amani
  • Kumpagaza Amani ulezi
  • Kumtafutia mwanawe kazi kwanjia ya kifisadi,
  • kughushi hatimiliki
  • Anamwacha mwanamke azalie njiani licha ya rai za mkewe.
  • Anashindwa hata kusoma hotuba ya rais kwenye sherehe muhimu.
  • Anachangia matumizi mabaya ya pesa zilizotengewa ujenzi wa hospitali, wanaishia kujenga zahanati.
  • Anamlazimisha Amani kumchimbia kaburi angali hai.
  • Anashindwa kukabiliana na hali ya ushinde; anajiua/anakufa kifo cha aibu. Anashindwa hata kuhusiana na ndugu yake.
  • Anasahau mafundisho ya kidini ya baba yake. Uongozi wake unawatelekeza wazalendo kama vile Matuko Weye na Chwechwe Makweche katika ugonjwa na hali duni. Ufisadi.
  • Anajitengenezea faili ili kupata mali akiwa mkuu katika Wizara ya Ardhi.
  • Anamtarajia ndugu yake Majisifu kuandika habari zake kwenye gazeti japo kwa kweli hastahiki.
  • Anamtaliki mkewe kwa tuhuma ambazo hajathibitisha.
  • Kutelekeza vituo vya kurekebishia tabia- seli katika afisi yake ni ch00 cha shimo refu.(b) Tathmini umuhimu wa barua ya Ben Bella kwa Mashaka katika kuijenga riwaya hii. (alama 8)

     

  • Ukiukaji wa haki za wafungwa- hajui kinachotokea nje ya kuta za jela.
  • . Kuonyesha ukosefu wa uwajibikaji wa vijana- yeye na Mashaka
  • . Kuonyesha uzinifu wa Nasaba Bora; anahusiana kimapenzi na Lowela.
  • . Kuonyesha ukiukaji Wa haki za kibinadumu; Lowela anaifunga mimba
  • Ndiyo inayoonyesha aliyekitupa kile kitoto mlangoni pa Amani.
  • Kuonyesha ukatili wa Lowela ~ anatoka nyumbani bila kuwajuza
  • Ndiyo kiini cha kuvunjika kwa uchumba wa Ben Bella na Mashaka na
  • Inachimuza tabia ya Mashaka. Hana uwezo wa kustahimili mazito.
  • Barua ya Ben Bela inaonyesha Hall Ziuni katika vituo vya kurekebishia tabia.
  • Anasema aliyopitia yalimfunza kuwa bado Tomoko haijapata uhuru. . Kuonyesha maudhui ya rnapenzi- anasema alijua bado Mashaka anampenda.
  • wanasuhubiana Wakiwa wachanga; shuleni.
  • yake bila kujali usalama wa kijusi.
  • Wazazi; anakitupa kitoto chake.
  • Kuonyesha uthabiti Wa moyo Wa Ben Bella.
  • Anasema baba mkwe hawezi tena kuwa shemeji, hivyo analaizimika kumwacha Mashaka. kuwehuka kwa Mashaka
  • Inabadilisha msuko Wa riwaya- Mashaka anashindwa kukabiliana na kutengana kwao, anawehuka na kuacha shule.SEHEMU C: TAMTHILIA T. Arege: Mstahiki Meya Jibu swali la 4 au la 5.

    4. “Tuyashughulikie ya leo. Kesho, keshokutwa na mtondo harutakuwepo. Wayatakig nigi ya mtongggoo? “

    (a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)

    (i) Ni maneno ya Meya.

    ii. Anamwambia Diwani III

    (iii) Wamo ofisini mwa Meya.

    (iv) Meya amesema wageni watawapa mkopo wa kulipa mishahara. (v). Diwani III anasema hili ni suluhisho la sasa lakini ni mzigo kwa . Wamo ofisini mwa Meya. watakaobakia. Ndipo Meya anasema haya.

    (b) Bainisha sifa ya mzungumzaji inayodokezwa na kauli iliyopigiwa mstari. (alama 1)

    – Mapuuza/kutowazia ya kesho/ukosefu Wa \uwajibikaji/\ubinafsi

    (c) Eleza sifa tano Za anayeambiwa maneno haya. (alama 5)

     

  • Diwani III ni msema kweli. Anamwambia Meya Lukweli kwamba mikopo itakuwa mzigo kwa vizazi vijavyo.
  • Ni mshauri bora. Anamshauri Meya Wabuni mikakati ya kuliinua pato la Baraza.
  • Ni mpiganiaji haki. Anasema kwamba mama mwenye kuuza ndizi analipa kodi hivyo madiwani Wanastahili kulipa.
  • Ni myenyekevu. Anazungumza na Siki/anamsikiliza Siki. Anasema wanawahitaji Wafanyakazi.
  • Ni mwadilifu. Kinyume na madiwani wenzake, anapinga Wazo la kuunda kamati za kuhudumu. Anataka Baraza liimarishe pato ili wafanyakazi Wote wafikiriwe kwa nyongeza ya mishahara badala ya kuwawazia madiwanitu.
  • Ni mwenye busara. Anamwambia Meya kuwa mi gomo itaathiri pato la Baraza.
  • Ni mtambuzi Wa mambo. Kinyume na Meya, anajua kwamba hata kazi za mikono zinahitaji akili; kwamba Watu wanahitaji kufunzwa kazi hizo.
  • Ni mtiifu. Meya anap0nga’ng’ania kwamba mishahara ya madiwani iongezwe, anasema yu radhi kufanya hivyo shingo upande.
  • Ni mzalendo. Anawazia vizazi vya kesho vya Cheneo; hataki kuviachia mzigo.
  • Ni mwenye msimamo thabiti. Anang’ang’ania kwamba Baraza linastahili kubuni mikakati ya kuongeza pato badala ya kuongeza mishahara ya walinda usalama.(d) Kwa kurejelea hoja kumi kutoka kwenye tamthilia, onyesha jinsi kutoyataka ya mtondogoo kulivyozorotesha hali ya maisha Cheneo. (alama 10)

     

  • Meya anapuuza umuhimu wa kuwepo kwa dawa hospitalini; raia wanakufa. Dadavuo Kaole.
  • Meya anapuuza kuboresha elimu; inaishia kuwa duni, anaharibu pesa kuwapeleka Wanawe ng’ambo. Baraza linapuuza malalamishi ya wafanyakazi, linayaona kuwa mkoromowa chura; mgomo unaangusha uongozi wa Meya.
  • Meya analipagaza Baraza deni kupitia kwa kandarasi, anamwambia mwanakandarasi alipandishe Baraza mahakamani; analifisi Baraza Zaidi.
  • Meya anapuuza mpango wa kimaendeleo wa miaka kumi; Cheneo inaendelea kuwategemea wafadhili. Kupuuza malalamishi ya wafanyakazi kunalifanya jiji kujaa uvundo; wageni wanaahirisha ziara.
  • Badala ya kumsikiliza Diwani III kuhusu haja ya kubuni mikakati ya kuinua uchumi wa Baraza, anapanga njia ya kudumisha uzalendo kupitia propaganda, anadhoofisha uongozi Wake.
  • Meya anamfanya Bili kuwa mshauri wake akijua kuwa Bili si mfanyakazi wa Baraza.
  • Bili anaishia kuiba fimbo ya Meya. Diwani I anatoka na fimbo bila kuwazia madhara yake; Bili anaiiba; Wao hawafaidiki. Raia wanamchagua Meya kila mara wakijua kuwa ni dhalimu; wanakosa mahitaji ya kimsingi kama vile chakula.
  • Meya anashindwa (anapuuza) haja ya kuwahakikishia Watu usalama wa chakula. Wanakulzi mizizi na matunda rnwitu, baadhi Wanakufa.
  • Wanataaluma (Siki)wanachelea kuingia kwenye siasa. Wanajinyima nafasi ya kuuwajibisha uongozi.
  • Wanyonge kama vile Dida wamekubali hali zao; Dida anasema kwamba hajaii, bora mameya Wawepo, naye apate nyumba za kunadhisisha. Wanaendelea kunyanyaswa.
  • Baraza linampa Meya mamlaka makubwa kikatiba; anaishia kuitumia kuwafiirusha wafanyakazi wanaogoma, na kujigawia vipande vya ardhi.
  • Meya anatumia pesa za mkopo kuagizia mvinyo kutoka ng’amb0, anaishia kulifilisi Baaza.
  • Meya anampa mhubiri sadaka bila kuwazia athari; kwamba analifilisi Baraza zaidi.
  • Badala ya kutafuta njia za kukomesha mgomo, Meya anasema kuna vijana wasio na kazi. Anaishia kujisababishia kung’olewa mamlakani.
  • Meya anajigawia viwanja na kumgawia Eili; anaishia kuufanya uongozi wake uchukiwe. Anang’olewa mamlakani.
  • Baraza linawabagua wafanyakazi. Madiwani wana bima za afya, wafanyakazi wenginc hawana. Wafanyakazi wanagoma, Meya anang’0lewa rnamlakani
  • Meya anachochewa na Diwani I na Diwani II kupuuza malalamishif migomo ya wafanyakazi, anasema kuna vijana wengi wasio na kazi. Wafanyakazi wanaishia kugoma, uvundo unaj aa, Meya anang’olewa mamlakani
  • Meya anapuuza Mpango wa maendeleo wa miaka kumi akidai yale ya kimilenia ndiyo muhimu. Cheneo inashindwa kuwatoshelezea raia mahitaji ya kimsingi kama vile chakula; watu wanakufa kwa njaa na ukosefu wa lishe bora5. “Ni mgao Wa wakubwa kula kwanza na sisi wengine kupigania makombo yanayoanguka chini.” (a) Fafanua sifa tano za mzungumzaji. (alama 5)

    (i) Beka ni jasiri. Anamwambia Meya kwamba wamekuja kumweleza Wala si kujieleza.

    (ii) Ni msema kweli. Anamwambia Meya kwamba hawataki kucheleweshewa mshahara.

    (iii) Ni mwenye busara. Anaona haja ya kuwa na akiba ila hawana cha kuweka kwani rnshahara ni duni.

    (iv) Ni mtetezi wa haki. Anamwambia Meya madiwani wamepata nyongeza ila wao wafanyakazi hawana.

    (v) Ni mwenye fiisimamo imara. Anasema kulikotoka pesa za madiwani zao zitoke hukohuko; hakubaliani na Meya.

    (vi) Ni mwenye mawazo mapevu. Anatambua kuwa kuna ugavi usiofaa wa mali ya umma.

    (b) Thibitisha ukweli wa kauli hii kwa kurejelea hoja kumi na tano kutoka kwenye tamthilia. (alama 15)

    – Mtihiniwa aonyeshe namna wanyonge hawafaidikikwa rasilimali za Cheneo huku wenye nguvu wanafaidika. Anaweza pia kuonyesha tofauti za kipato. Baadhi ya haja ni:

    (i) Nyumba ya Meya inanadhifishwa huku mji umejaa uvundo.

    (ii) Madiwani kuongezewa mshahara — wafanyakazi hawaongezewi.

    (iii) Madiwani kutotozwa kodi huku muuza ndizi anatozwa.

    (iv) Madiwani wana bima ya matibabu; wafanyakazi hawana.

    (V) Madiwani wanaishi kwenye majumba, Wafanyakazi Wanaishi vibandanii

    (vi) Kwa Meya kunapikiwa hata mbwa, watu wanakula mizizi na matunda mwitu.

    (vii) Madiwani wanausafiri, wafanyakazi hawana.

    (viii) Meya anajigawia viwanja na kumgawia Bili, wengine hawana.

    (ix) Meya anaunda kamati za kulihudumia Baraza ili kuwafaidi wafuasi wake huku Wafanyakazi wanakosa hata glavu za kuoshea vyoo.

    (x) Meya anawapeleka wanawe kusomea ng’ambo, wengine wanapata elimu duni.

    (xi) Meya anampeleka mkewe kuzalia ng’ambo, wengine wanapata huduma hafifu Za kiafya; zahanati haina hata dawa ya kuua vij asumu. Mtoto anakufa kwa kula chakula kibaya.

    (xii) Meya anampa mhubiri sadaka na hali hawaongezei Wafanyakazi mshahara.

    (xiii) Meya, Diwani I na Diwani II wanajilipa ovataimu na hali hawana hata pesa za kuwaongezea wafanyakazi mshahara.

    (xiv) Meya na madiwani wanapanga nj ama za kujidumisha mamlakani bila kupanga lolote ‘la kumfaidi raia wa kawaida. Diwani III anawaambia hayo.

    (xv) Bili,kwa sababu ya akili yake, ameiba fimbo. Meya na madiwani I na II hawafaidiki kutokana na ukosefu wao wa busara.

    (xvi) Waridi anawatarajia wagonjwa kulipia matibabu na hali jamaa yake anapokufa anajiuzulu.

    (xvii) Katiba inampa Meya mamlaka malmbwa; madiwani wanalazimika kuuwajibikia uongozi wa Meya kwa kukubaliana na baadhi ya maamuzi hata kama si ya haki.

    (xviii) Meya anatumia entertainment vote yake kujiburudisha yeye na Bili na hali wagonjwa wanakufa kwa ukosefu wa dawa.

    (xix) Meya anafanikisha kufidiwa kwa mwanakandarasi ili yeye pia afaidike, na hali Baraza halina hata vifaa vya kimsingi vya wanaosafisha mji.

    SEHEMU D: USHAIRI

    (a) Fafanua mambo sita ambayo yanaweza kuzorotesha maadili ya anayelengwa na shairi hili.

    (i) Kufuata ushawishi wa wenye dhambi

    (ii) Kuandamana na washerati

    (iii) Kuandamana na wajeuri

    (iv) Kuwasifu waongo

    (v) Kuandarnana na wafisadi

    (vi) Kuwapa nafasi watu wabaya/kuandamana na wabaya

    (vii) Kukubali kupembejwa na washerati

    (viii) Kufilata njia za wajeuri/kuathiriwa na wajeuri

    (b) Bainisha tamathali mbili za usemi zilizotumiwa katika shairi hili.

    (i) Tashbihi – kama mwali – kiakili – mithili yao mapembe ya fahali

    (ii) Sitiari – ni shubili – Kemikali- Si Injili

    (c) Andika aina mbili za urudiaji zilizotumiwa katika shainri hili.

    (i) Urudiaji wa neno – mwanangu.

    (ii) Urudiaji wa sentensi/kishazi – mwanangu sikubali

    (ii) Urudiaji Wa silabi — ngu, li

    (d) Ainisha shairi hili kwa kuzingatia vigezo vifuatavyoz

    (i) idadi ya vipande katika mishororo.

    – Ukawafi — vipande, 3 katika kila mshororo

    (ii) mpangilio wa maneno katika mishororo

    – Kikwamba — neno, mwanangu kuanzia kila mshororo.

    (iii) idadi ya mizani katika mishororo.

    – Msuko — kibwagizo ni kifupi.

    (iv) mpangilio wa vina katika beti.

    – ukara — Vina vya kati vinabadilika, vya nje vinatiririka

    (e) Andika aina mbili za uhuru wa kishairi zilizotumiwa katika shairi hili.

    (i) Inkisari

    – sikuperembe. Wasikuperembe

    – siwe.usiwe

    – ndo.ndio

    (ii) Lahaja

    – usifwate.usifuate – hino.hii

    (iii) Udondoshaji maneno — ujeuri sera yao — ujeuri ni (ndio) sera yao.

    – duniya.dunia

    Andika ubeti wa tano kwa lugha ya nathari.

    – Mwanangu usiandamane na wafisacIi’kwani Wao ni mfano wa kemifiili. utu Wao unaongozwa (wao wanaongozwa) na tamaa wala si injili/dini. (Mwanangu) Usikubali kuandamana nao; waambie (wahepe) kila siku.

    (a) Eleza mikakati sita inayotumiwa na waajiri kujikuza kiuchumi. (alama 6)

    (a) (i) Kumthamini mfanyakazi waonapo ana uwezo wa kuwazaIi§hia riziki

    (ii) Kuwafanyiza kazi ngumu/kwa muda mrefu — kukupindisha mgongo

    (iii) Kumsifu kiongo — watakwita kwa majina

    (iv) Kujinasibisha na wafanyakazi — kumwonyesha mfanyakazi Wao ni Wamoja; kwa faida ya pamoja.

    (v) Kumhadaa mfanyakazi kwa zawadi

    (vi) Kumshawishi/kumhimiza kuendelca na kazi (vii) Kulipa pato duni/kumpimia kipato

    (viii) Kumwaminisha wanaweka malengo pamoj a ili kuvuta uaminifu wake mfanyakazi

    (ix) Kumtengenezea kandarasi ya kazi

    (X) Kumsukuma ili kufikia shabaha.

    (b) Bainisha tamathali tatu za usemi zilizoturniwa katika shairi hili. (alama 3)

    Sitiari — u chambo – ndoana- nyenzo ya kufanyia kazi – u nundu – u ndovu – ukiwa yao makasia – dau- nchi – miamba- matatizo

    (ii) Tashbihi — kama sahani na kawa. -ja fahali

    (iii) Kinaya — kusifu kiongo, ujira duni kwa kazi nyingi.

    (iv) Taswira (Taswira mwendo) Kukupindisha mgongo- kutesa/kufanyiza kazi nyingi. Picha ya mtu anayeinama/anayeumia.

    (v) Tashtiti — shairi zima linawafanyia tashtiti waajiri.

    (c) Huku ukitoa mifano, bainisha aina mbili za umuhimu wa kishairi aliotumia mshairi.

    i) Inkisari — walo —. walio -ndo-ndio

    (ii) Kufinyanga sarufi- ndoana umeshika — umeshika ndoana – yenu matarajio – matarajio yenu -makoma kuangusha — kuangusha makoma – yao kazi- kazi yao- yako thamani- thamani yako

    (d) Andika mifano ya mistari mishata katika shairi hili.

    – We u chombo cha

    Kwamba we na wao mu

    – Watakwonyesha wao

    – Katika kuyavyaza na

    – Ambayo ubatizo wake ni – Na usidhani una hiari ya

    (e) Bainisha nafsineni katika shairi hili.

    – Mzindushi/mfilamishi/mtetezi wa Hiki/mwajiriwa/mfanyakazi.

    (f) Fafanua toni ya shairi hili.

    – Ya kukashifu/ya uchungu (Na usidhani una hiari ya kuamua …

    (g) Andika ubeti wa tatu kwa lugha ya nathari.

    – Ukiwa ndiwe chombo cha kuyafanikisha mamb0/ malengo ya mabepari, Watakusifu na kukuhimiza uendelee kufanya kazi kuwazalishia mali. Hata hivyo wanakupa ujira mdogo ili usikidhi/ usitosheleza haja zako. Uendelee kuwategemea.

    SEHEMU E: HADITH FUPI K. Walibora na S. A. Mohamed (Wah): Damu Mveusi na Hadithi Nyingine

    8. (a) Tathmini umnuhimu wa Lucy katika kuijenga hadithi, “Tazamana na mauti”

    “Mizizi ya Matawi” (Ali A. Ali)

    (b) “Aaa, bibi yangu namuomba Mungu anisamehe dhambi zangu ..”’

     

  • Lucy Anaonyesha ukengeushi — anatamani London kwa kupenda ya fahari yaliyopo.
  • Kuonyesha ndoto ambazo vijana wanazo na ambazo zinawapor0m0sha- ndoto yake ya London inamsababishia kifo.
  • Kuendeleza maudhui ya elimu; hafanyi vyema katika mtihani wa kidato cha sita.
  • Kuendeleza dhamira/suala la uharniaji ng’ambo. Anatafuta sababu za kmnpeleka ng’ambo, anaishia kujifunga kwa mzee mgonjwa ili kukidhi haja yake.
  • Kuonyesha maudhui ya ubinafsi — anamsaidia Mzee Crusoe ili afaidike. Anapomsaidia hapo sinema, Crusoe anamwahidi zawadi.
  • Kuonyesha/kuendeleza maudhui ya tamaa; hataki riziki, anataka muluki.
  • Kulinganua_maishaya Uingereza na huku; serikali ya huko inashughulikia/inawakidhi wasio na kazi.
  • Kuendeleza maudhui ya ndoa. Anaolewa na Crusoe ili afaidike kwa mali yake.
  • Kuujenga msuko (ploti) Wa hadithi .Kuhudhun’asinema kwake kunabadilisha mkondo Wa hadithi. Anaolewa na Crusoe, anaenda London.
  • Kupitia kwake mwandishi anamj enga mhusika Crusoe. Anaonyesha uwajibikaji wa Crusoe. Anataka kumrithisha kihalali kabla hajafa.
  • Anaendeleza maudhui ya unafiki. Anasema yeye ni mwanamke mwenye bahati sana ili kumshajiisha Crusoe amrithishe.
  • Filamu anayotazarna inamdokezeal inamtabiria msomaji yatakayotokea.
  • Kuonyesha matatizo yanayowakumba vijana. Ukosefu wa nafasi za kazi na matarajio yaliyokiuka rnipaka yanamfanya kumhadaa Crusoe kwa mapenzi.
  • Kunyesha maudhui ya uwajibikaji. Anampa dawa Crusoe kule kwenye sinema. (i) Eleza muktadha Wa dondoo hili.- Dondoo limetolewa uk. 115.

    Ni maneno ya Bi. Kudura.

    (ii) Anamwambia Bimkubwa.

    (iii) Wamo nyumbani mwa Bimkubwa.

    (iv) Bimkubwa amemuuliza kama ana mwana.

    (ii) “Jamii ya,” Mizizi ya Matawi Tazamana na Mauti.”Matawi inastahili kusamehewa ” Fafanua kwa kutoa hoja sita kutoka kwenye hadithi.

    – Mtahiniwa afafanue makossa ambayo jamii hii imetenda/ Aonyeshe uzfhaifu Wa Wahusika mbalimbali katika jamii hii Aonyeshe kwa nini jamii inastahili kusamehewa.

    Baadhi ya hoja ni:

    (i) Bimkubwa kutomwambia Sudi usuli wake.

    (ii) Bimkubwa kumwambia Sudi kwamba mumewe alikufa na kumwaminisha kuwa alikuwa na baba.

    (iii) Bimkubwa anamsababishia Sudi dhiki ya kisaikolojia kwa kutomwambia usuli wake.

    (iv) Bi. Kudura anakitupa kitoto chake.

    (v) Bi Kudura kutomtafuta mtoto wake awali.

    (vi) Sudi alihusiana né. Waridi Ulaya lakini amemsahau.

    (vii) Kupata watoto nje ya ndoa — Bi. Kudura anamzaa Sudi nje ya ndoa.

    (viii) Mapuuza — vijana kutoona faida ya uj ana na kuuthamini ( Bi. Kudura anajutia haya).

    (ix) Japo Bimkubwa alimlea Sudi vyema, hatujaonyeshwa iwapo alimrithi kihalali.

    (x) Bi. Kudura anaishi na Sudi kwa muda bila kumwambia yeye ndiye mama yake hadi pale anapoulizwa na Bimkubwa na kuona aibu.

(Visited 267 times, 2 visits today)
Share this:

Written by