KCSE Past Papers 2016 Kiswahili Paper 2 (102/2)

2016 Kiswahili Karatasi ya 2

Lugha

(a) Eleza athari za madeni kwa nchi zinazoendelea.(alama 2)

❖ Asilimia kubwa ya patu la mataifa yanayoendelea huishia kulipa madeni haya.

❖ Hivyo inakuwa vigumu kwa mataifa hayo hujikwamua kutokana na umaskini

(b) Kwa nini umaskini unatawala mataifa yanayoendelea? (alama 4)

❖ Ufisadi, uongozi mbaya, turathi za kikoloni, uchumi kutegemea kilimo chenye mvua isiyotabirika, idadi kubwa ya watu, nafasi adimu za kazi, madeni na ukosefu wa elimu

(c) Mwandishi anatoa mapendekezo yapi kwa mataifa yanayoendelea katika kutatua tatizo la ufukara?(alama 4)

❖ Kuibuka na mikakati bora ya kupambana na umaskini.

❖ Sera zinazotambua kuwa rain wake wengi ni maskini.

❖ Kuzalisha nafasi za aura kuimarisha miundo msingi.

❖ Kuendeleza elimu inayolenga kutatua matatizo maalum

❖ Kupanua viwanda.

❖ Kuhakikisha kuwa mfumo wa soko huu hauishii kusababisha kufungwa kwa viwanda.

(d) Mfumo wa soko huru una mathara gani kwa mataifa yanayoendelea? (alama 2)

❖ Unaweza kuwa chanzo cha kufa kwa viwanda asilia.

(e) Taja visawe vya maneno yafuatayo kama yalivyotumika katika kifungu. {alama 3)

(i)Turathi za kikoloni >

❖ Masalio ya kikoioni / ukoloni mambo leo / athari za ukoloni.

(ii) Kuatika

❖ Kuzalisha/ kuwa

❖ chanzo/ kuanzisha/ kuleta/ kusababisha/ kupanda.

(iii) Kuyaburai

❖ Kuyasarnehe/ kuyaondoa/ kuyasahau/ kuyapuuza/ kuyafudlia mbali

Muhtasari (alama 15)

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu mnswali. Taifa huundwa na watu wanaoishi katika nchi moja na wanaojitambua kisiasa kama watu walio na mwelekeo, maono na hatima sawa. Utaifa hujengwa kwenye misingi ya mapenzi kwa nchi, Utambuzi wa cheo, eneo, hadhi, rangi na hata makabila wanakotoka raia wa taifa moja si chanzo cha kuwatanganisha.

Nchi moja huweza kuundwa na watu walio na tofauti chungu nzima zikiwemo tofauti za kikabila, kitabaka na kimawazo. Hata hivyo, watu hao huwa na folsafa na imani sawa kama taifa inayoashiriwa hasa na wimbo wa taifa. Hata hivyo haya yotc hayawezi kuwafikia katika kiwango cha kuunda taifa. Uzalendo ndio mhimili mkuu wa utaifa. Uzalendo ni mapenzi aliyo nayo mtu kwa nchi yake. Mapenzi haya humwongoza mtu katika mawazo yake, itikadi yake, matendo yake, matamanio yake na mkabala wake kuhusu nchi na hatima ya nchi yake.

Mzalendo hawezi kushiriki katika matendo yanayoweza kuiletea nchi yake maangamizo kwa vyovyote vile. Mzalendo huongozwa na mwenge wa wema. Mzalendo hawezi kushiriki kwenye shughuli zozote zinazohujumu mshikamano wa kitaifa. Yeye hatawaliwi na ubinafsi wa kutaka kufaidi nafsi yoke naya jamii yake firtyu. Matendo yake yote huongozwa na ari ya kuiboresha nchi yake. Anayeipenda nchi yake hujiepusha na ulafi wa kujilimbikizia mall.

Yuko radhi kuhasirika mradi taifa lake linufaike. Utaifa ni mche aali unaopaliliwa kwa uzalendo, kuepuka uchu wa nafsi na taasubi hasi zikuwepo za kikabila na ubinafsi. Hali hii inapofikiwa, hatima ya taifa na mustakabali wa raia wake huwa wenye matumaini makubwa

(a) Kwa maneno 40 – 50 dondoa sifa kuu za utaifa.(alama 6, 1 ya mtiririko)

❖ Kuwepo kwa hatima sawa

❖ Kuwepo kwa maono sawa

❖ Kuwepo kwa folsafa/ imani/itikadi sawa.

❖ Kuwepo kwa mwelekeo mmoja.

❖ Umejengwa kwa hisia za mapenzi kwa nchi.

(b) Ni nini misingi ya kutathmini mzalendo? (maneno 60 – 70) (alama 9, 1 ya mtiririko)

❖ Hawezi kushiriki kwenye shughuii zozote zinazohujumu mshikamano wa kitaifa.

❖ Hawezi kutawaliwa na ubinafsi

❖ Hujiepusha na ulafi wa kujilimbikizia mall.

❖ hawezi kutenda mambo ya kuiletea nchi yakemaangamizo.

❖ Yuko radhi kuhasirika kwa manufaa ya taifa lake.

❖ Matendo yake huongozwa na mwenge wa wema.

❖ Matendo yake huongozwa na ari kuiboresha nchi yake.

3.matumizi Ya Lugha (alama 40)

(a) Tumia nomino yoyote katika ngeli ya 1-1 kutunga sentensi. (alama 1)

❖ Mfano wa nomino ni kama: chumvi, sukari, mvua, chai, asali, furaha, huzuni, petrol nk. Mfano wa sentensi- Chumvi imemwagika.

(b) (i) Nini maana ya silabi (alama 2)

❖ Ni sauti moja au zaidi zinazotamkiwa kama fungu moja la sauti.

❖ Silabi ni kipashio cha utamkaji ambacho hutumiwa kwa pamoja kama fungu moja la sauti.

❖ Tamko, pigo, tamshi.

(ii) Tunga neno lenye muundo huu wa silabi: Irabu + konsonanti + konsonanti + irabu

afya, anza, ibia, enda, unga, uzwa, igwa, ugwa.

(c) Tunga sentensi hii upya kwa kufuata maagizo: Wasichana wanaingia darasani kwa haraka (andika kinume chake) (alama 2)

❖ Wasichana wanatoka darasani polepole/ taratibu/ asteaste/ halahala/ ala ala.

(d) Tambua kiambishi awaii na tamati kati neno: Alalaye (alama 2)

❖ A – awali o a – ye – tamati

(e) Ainisha vivumishi katika sentensi hii: mzee mwenyewe ni mkongwe na amepewa zawadi kwa kuwa shamba lake lilitoa mazao mengi. (alama 4)

❖ Mwenyewe – kivumishi cha pekee Mkengwe – kivumishi cha sifa Lake -kivumishi kimilikishi Mengi – kivumishi cha idadi

(f) Askari wasipopiga doria wala kushikiana na raia hawatakuwa wametuhakikishia usalama.

(yakinisha sentensi hii) (alama 2)

❖ Askari wakipiga/ wanapopiga/ wapigapo/ watakapopiga doria na kushirikiana na raia watakuwa wametuhakishia usalama.

(g) “Shughuli yetu itakamilika kesho”, mama alimwambia mwanaye Juma. (Andika katika usemi wa taarifa). (alama 2)

❖ Mama alimwambia mwanawe/ mwanaye Juma kuwa shughuli yao ingekamilika siku ambayo ingefuata.

(h) Changamua sentensi ifuatayo kwa kielelezo cha matawi. Mpria ulichezwa tulipokuwa tukipika.(alama 3)

 

(i) Dhihirisha matumizi matatu tofauti ya kimaana yatakayotokea ketenzi “ona” kikinyambuliwa katika kirai hiki “ona ndoto”. (alama 3)

❖ Onea ndoto

❖ Onewa ndoto

❖ Oneshwa ndoto

❖ Onesha ndoto

❖ Onoana ndoto

(j) Eleza matumizi ya hali za “ka” na “hu” katika sentensi zifuatazo: (i) Balozi huja hapa kila mara. (alama 1)

❖ Hali ya mozoca kila mara kila siku mara kwa mara (ii) Mpishi alipika, akapakuwa na akagawa chakula. (alama 1)

• vitendo vinafuatana Mfulultzo wa vitendo Mfuatano wa vitendo Kufululizwa kwa vitendo

(k) Eleza maana mbili zinazojitokeza katika sentensi: Tuiiitwa na baba. Mtendaji ni baba

❖ Mtu mwingine alituita mimi pamoja na baba. Sisi pamoja na baba

❖ Mimi na mtu mwingine tuliitwa na baba Mimi na watu wengine tuliitwa na baba.

(I) Akifisha: Shangazi alimwambia mwanawe njoo nikupcleke kwenu jioni mtoto aliuliza kwetu wapi?(alama 4)

❖ Shangazi alimwambia mwanavve, “Njoo nikupeleke kwenu jioni.” “Mtoto aliuliza, “Kwetu wapi?-

(m) Eleza matumizi mawili ya kiambishi -ji-.(alama 2)

❖ Mwanzoni mwa baadhi ya nomino katika ngeli ya LI-YA.

❖ Kujirejeiea/ kircjeshi cha mtenda/ kujitendea.

❖ Kuonyesha uzoefu

❖ Kuonyesha ukubwa Kuonesha udogo/ udunishaji

(n) Tunga sentensi hii upya kwa kutumia visawe vya maneno yaliopigwa mstari. Kiambaza kilimuumiza ghulamu alipokuwa akipanda. (alama 3)

❖ Ukuta ulimuumiza mvulana alipokuwa akiuparaga

(o) Tumia kitenzi “Fa” katika sentensi kuonyesha mazoea. (alama 2)

❖ Hufa/ hufisha/ afaye/ wafao

(p) Ainisha vihusishi katika sentensi ifuatayo: Babu alipika mapema kuliko wote halafu akaondoka.(alama 2)

❖ Kuliko – kulinganishi/ kiwango Halafu – wakati

(n) Tunga sentensi hii upya kwa kutumia visawe vya maneno yaliopigwa mstari. Kiambaza kilimuumiza ghulamu alipokuwa akipanda. (alama 3)

• Ukuta ulimuumiza mvulana alipokuwa akiuparaga

(o) Tumia kitenzi “Fa” katika sentensi kuonyesha mazoea. (alama 2)

• Hufa/ hufisha/ afaye/ wafao

(p) Ainisha vihusishi katika sentensi ifuatayo: Babu alifika mapema kuliko wote halafu akaondoka.(alama 2)

• Kuliko – kulinganishi / kiwango Halafu – wakati

(q) Tumia kitenzi “tafakaru” kama nomino katika sentensi. (alama 1)

• Kutafakari kwake kulimnufaisha.

• Utafakari huo utamwezesha kupiga hatua kimaendeleo. Tafakari zao ndizo zimewafikisha walipo.

(r) Andika upya sentensi ifuatayo kwa kutumia viwakilishi badala ya nomino zilizopigwa mstari. Mwanamziki ataembelea mji. (alama 1)

• Yeye/ yule/ huyu/ huyo atatembelea mji

3.matumizi Ya Lugha(alama 10)

Kwa kutoa mifano maridhawa, eleza kaida zozote tano ambazo matumizi ya lugha hutegemea katika jamii.

❖ Mazingira/ mahali

❖Jinsia/ uana

❖ Cheo/ hadhi

❖ Umri

❖Mada

❖ Muktadha

❖ Wakati/ misimu

❖ Malezi

❖ Taaluma/ kazi/ shughuli

❖ Mila/ desturi/ u’amaduni

❖ Hadhira.

❖ Njia ya mawasiliano I mani/ dini / itikadi + Tajriba/ uzoefu/ ujuzi

❖ Elimu(kiwango cha elimu)

❖ Hali/ hisia

❖ Lugha azijuazo mtu

❖ Wahusika

❖ Uhusiano

❖ Madhumuni/ lengo/ nia

❖ Tabaka

❖ Falsafa/ mtazamo

 

(Visited 380 times, 1 visits today)
Share this:

Written by