KCSE Past Papers 2021 Kiswahili Karatasi ya 2 (102/2)

Kenya Certificate of Secondary Education

Kiswahili Karatasi ya 2

1. UFAHAMU

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali. (Alama 15)

Alikuwa wakati wa jioni jua limepunguza udhia wake na upepo mwanana ulikuwa ukipita na kuzipapasa ngozi zetu mfano wa pamba. Kama ilivyokuwa desturi yetu hapo kijijini, siku hiyo pia tuliketi nje ya nyumba yetu tukafanya duara kulizunguka birika la kahawa. Kila mmoja alichukua glasi akajimiminia kiasi cha kahawa alichotaka na kurudi kuchukua mahali pake kitini.

Tulipotia fahamu tulipata mazoea haya yamekita mizizi nasi tukawa hatuna budi kuyakumbatia. Hatukuyakumbatiatu, bali tuliyakumbatiakwa dhati yamoyo. Vikao hivi havikuwa tu hazina kubwa kwetu bali pia vilikuwa vya thamani isiyomithilika. Hapa ndipo tulinoleana bongo kwa kupashana habari. Leo hii tumo katika kuzungumzia nguzo kuu za maendeleo, tena maendeleo ya haja ambayo yataibadilisha sura ya mwananchi na nchi. Nahodha wa kikao cha leo anampa msemaji wa kwanza nafasi naye hakusita kushika usukani.

‘Nionavyo mimi, maendeleo yatawezekana ikiwa elimu itaweza kukidhi haja za watu. Sio nadharia tupu ambayo huwezi kuitumikiza ikaleta matokeo. Lazima nchi imwezeshe kila mtu kupata elimu ya msingi ambayo itamsaidia kufikia habari za kimsingi, iwe ni kupitia kwa magazeti au vitabu. Habari hizo zitamfunua macho, akaona na kuhakiki mambo. Wenzangu, jibu ni elimu! Maendeleo yanategemea elimu,” kijana mmoja alisema kwa mhemko.

Muda wote huo kila mtu alikuwa ametulia. Wapo waliotikisa vichwa kukubaliana naye na wapo waliovitikisa kukataa. Hata hivyo, walikuwepo waliokaa tu kama mawe. Hawakuonyesha ishara yoyote ya kuguswa na maneno yale.

Mwendesha mjadala alifanya ishara na mara kijana wa miraba minne aliyekuwa amevaa shati lililompwaya akasimama na kuzungumza kwa sauti nzito. “Mtazamo wangu mimi bwana ni tofauti. Ukitazama duniani kote, kila nchi iliyoendelea imewekeza sana viwandani. Uzalishaji wa viwandani ndio dawa mjarabu. Hebu vuta fikra! Kila tunachotumia kuanzia kalamu, kitabu, nguo, msumari, saruji … yaani kila kitu chenye nafasi katika maisha yetu kimepitia hatua za uzalishaji viwandani…”

“Si ndio hayo! Naona unaniunga mkono aisee! Viwanda huendeshwa kwa elimu au ukipenda maarifa. Na maarifa hayo huja kwa mafunzo ambayo ni elimu,” alifafanua yule kijana wa kwanza.

‘Nipe muda Sudi! Nipe rnuda nimalizie hoja yangu. Ninachosema ni kuwa elimu bil utumizi wake kuzalisha huduma na bidhaa muhimu haina nafasi kubwa katika maendeleo y jamii. Elimu si mwisho wa yote bali mwanzo. Elimu inafaa kuzalisha. Na uzalishaji muhimu zai ni wa viwandani. Kwa hivyo, nionavyo mimi msisitizo mkubwa unafaa kuwa katika kutengeneza viwanda na kuvifanya kuzalisha.”

Jama alimali a mazungumzo yake akatulia na kupiga funda la kahawa. Hapo ndipo mwendesha mjadala alipompa kijana mwingine nafasi naye atoe maoni yake. Kijana huyo mdogo wa kimo na umbo alianza kusafısha koo huku wenzake wakirnshangilia. Kwa kawaida kijana huyo alikuwa na mbwembwe nyingi.

“Bwana Spika,” alian a huku wenzake wakishangilia kwa kila namna. Walipotulia aliendelea, “Mimi najua wapo watakaoniita mjinga hapa lakini naamini miundombinu ni muhimu zaidi. Watu hawawezi kuendelea bila mfumo mzuri wa barabara na reli, usambazaji wa kuridhisha wa umeme, viwanja vya kutosha na bora kwa ajili ya vijana kunoa vipawa vyao…

Maneno yake yalifunikwa ghafla na kelele za kumshangilia na kumsifu huyu kijana waliyemwita Sumaku. Hii ilikuwa lakabu waliyompa kwa uwezo wake wa kuelewa mainbo kwa wepesi na kwa kujua kuwavutia vijana wenzake maana alijua wapi pa kugonga ili gogo litoe mlio. Alipoona bado wanashangilia aliinua mkono wake wa kushoto juu na kusema, “Basi! Basi,

wananchi, sina shaka ujumbe umefika.” Kisha aliketi na kuwaacha wenzake wakiumwa mbavu kwa vicheko. Utulivu ulirejea taratibu. Kabla kila mmoja amakinike, mwendesha mjadala alimpa nafasi mzee mmoja aliyekuwa amevutwa na mazungumzo hayo naye kuchangia. Mzee yule alicheka kidogo, akasafisha koo na kuwapongeza wachangiaji waliomtangulia kisha naye akasema yake. “Mambo hayo yote ni kama pacha lakini pekee hayatoshi.

Miundomsingi inahitaji watu wa kuitumia, navyo viwanda vinahitaji wafanyakazi. Watu hao wasipokuwepo, vitu hivyo havina maana. Watu hao wanahitaji kuwa na afya bora. Hospitali zinahitaji kuwa katika kiwango cha kutoa huduma za kuridhisha. Zinahitaji wataalamu wasiobabaisha, vyombo vya kisasa vya udodosi na upasuaji, dawa nzuri na mazingira safi kwa ajili ya wagonjwa. Halafu huduma hiyo nzuri iwe inaweza kufıkiwa na kila mtu.”

Alitua kidogo. Sasa kila mtu alikuwa ametulia kama ardhi iliyonyeshewa. Kisha akaendelea, “Pamoja na hayo, ipo haja ya huyo mfanyakazi kupata pa kuweka ubavu wake. Akiisha kuichapa kazi anahitaji kurudi nyumbani. Si nyumbani kwa maana ya mahali pa kupangisha bali nyumbani kwa maana ya mahali pake mwenyewe.

Hivyo panahitaji kuwepo mpango wa wafanyakazi kununua nyumba kwa bei nafuu. Mtu si kaına ndege anayeweza kuishi mtini na akaamka kushika shughuli zake. Mtu huhitaji makao yake. Haya yote yakifanywa kwa pamoja na kwa ufanisi basi tutakuwa tumeanza kujiandaa kupaa kwa mbawa zetu wenyewe.”

Alipomaliza kusema alishika njia na kwenda zake bila kutazama nyuma. Sote tulijikuta tunacheka kwa sauti huku tumetabasamu.

(a) Baiaisha mambo matntu ambayo yanaleta utangamano baina ya vijana wa jamii hii. (alama 3)

(b) Kupata elimu pekee hakutoshi kuleta maendeleo.” Thibitisha kwa hoja mbili kutoka (alama 2)

(c) Kwa kutoa hoja nne, onyesha uhusiano uliopo kati ya nguzo mbalimbali za maendeleo kwa mujibu wa kifungu.(alama 4)

(d) Eleza mambo matatu ambayo yanawachangamsha vijana katika kifungu (alama 3)

(e) Kauli, “upepo mwanana ulikuwa ukipita na kuzipapasa ngozi zetu,” imetumia tamathali gani ya usemi? (alama 1)

(f) Eleza maana ya, ‘tulinoleana bongo’ kwa mujibu wa taarifa.(alama 1)

(g) Andika kisawe cha ‘hoja’ kwa kurejelea kifungu. (alama 1)

UFUPISHO 2. Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali. (Alama 15)

Binadamu hakuumbwa kuishi katika upweke na kujitenga. Aliuınbwa kuwa selıemu ya mfumo wa ushikamano na wenzake. Baadhi ya jamii zinaeleza kwamba Mungu alimuumba mwanamume kwanza na alipoona kwamba anaishi kitwea akamuunıbia mwananıke kuwa mshirika wake. Hatua hii ikawa ndio mwanzo wa watu kuishi paıııoja kama mke na mume.

yumkini hiki ndicho kiini cha familia. Mshikamano wa familia ni muhimusana kwa sababu hujenga uhUsiano mwemana hushirikianakünawazo, kikazi na hata zinapozuka haja nyinginezo.

Mababu zetu W£tlihitaji sana umoja wa familia.

Umoja huo ulifaa mno katika hali mbalimbali. Wakati huo Watu WalizuRgukwana misitu mikubwa ambamo waliishi wanyama wakali kama Vile simba, chui na duma. Wanyama hao walikuwa hatari kwa binadamu na hivyo kuwahitaji watu kuungana kuwakabili.

Enzi hizo za mababu pia zilishuhudia uhasama wa kikoo. Koo mbalimbali zilishindana kunyang’anyana mifugo na kung’ang’ania ardhi ili kujijengea himaya zao. Katikati hili pia ushirikiano wa karibu ulihitajika ili kujihami dhidi ya uvamizi wowote ule. Kutokuwepo kwa uvamizi kulimaanisha kuwa jamii ilipata utulivu na ınoyo wa kuendeleza shughuli zao za kila siku ambazo zilikuwa msingi wa maendeleo yao. Watoto nao walipata mazingira salama nâ tulivu ya kucheza na kukua.

Ushirikiano huu haupo tu katika familia za wanadamu. Tunawaona wanyama wakiwa katİka makundwi. anatembekau,cheza, kula na kulala katika makundi.

Makundi haya ni muhimu Sâflâ katika maisha ya wanyama mbalimbali. UlimBwengu wa wanyama una adha tele. Adha hizo huwa kisiki mkubwa katika maisha ya wanyama. Zipo hatari za baadhi ya wanyama kuwindwa na kufanywa kitoweo. Mnyama akiwa peke yake huwa windo rahisi kwa wawindaji.

Wakiwa katika kundi husaidiana kushika zamu na kutanabahishana hatari ibishapo. Kwa kufanya hivyo huokoleana maisha. Nao wanyama wanaowinda huwa na kibarua kigumu kupata windo wakiwa waenda pweke. Hata simba, mfalme wa msitu, huhitaji kufanya shirika na wenzake ili ktıliwahi windo kwa urahisi. Wapo wanyama wala nyama ambao hufa kwa kukosa chakula kwa sababu ya kukaa peke yao.

Hii leo utaona kuwa watu hawashirikiani katika familia tu. Wanashirikiana pia katika mazingira ya shule ambapo wanapokezana maarifa mbalimbali ambayo ni muhimu katika maisha yajayo. Panapokuwa na ushirikiano mzuri kivuno huwa tele kwa mwanafunzi ambaye hujizolea mengi.

Hupata elimu ambayo humfungua macho kuona sura tofauti tofauti za ulimwengu, hukuza kipawa chake ambacho anakitumia kwa manufaa yake na ya jamii pana, hujifunza udugu ambao ni muhimu katika kuishi na watu wengine baada ya masomo, na mwanafunzi huweza pia kukomaa kimawazo na kuwa kiungo muhimu cha taifa.

Hata hivyo, haya hayaji tu na kumtamia mtu eti kwa sababu amefika na kuishi shuleni kipindi chote cha masomo. Hupatikana kwa mwanafunzi kujenga uthabiti wa fikra na mazoea ya daima kulenga kuwa mtu bora kwa wenzake, awe anawajua au hawajui. Kumbuka kuwa hata wanyama hufanya juhudi kubwa katika kujenga ustadi wao kushirikiana kulipatawindo au kukwepa wawindaji.

Taasisi zilizobuniwa kuwa nyenzo za kuendeshea maisha yetu zinajengwa katika misingi hiyo ya familia. Watu huja pamojana kuunda sheria na kanuni zinazoelekeza utendakazi wao. Bila mpangilio unaohakikishaumoja na ushirikiano miongoni mwa watu, huduma zetu muhimu zingekwama na kutuletea dhiki isiyo mfano.

Askari hushirikiana ili kufanikisha kazi yao ya kukomeshuahalifu, walimu hushirikiana kuhakikisha kuma mwanafunzi amepata elimu ipasayo na ipasavyo, dereva na utingo wake, lazima washirikiane ili kufanikisha safari ya abiria, rais na mawaziri wake hawana budi hushirikiana ili kufanikisha ajenda ya maendeleo.

Ulimwengu wa sasa unahitaji watu wawezao kushirikiana. Wanaposhirikiana, shughuli iliyo mbele yao huwa nyepesi na matunda yake huwa ya kufana.

Tunaona manufaa ya ushirikiano kwa uwazi zaidi viwandani. Wafanyakazi wa viwandani hugawanya majukumu. Kila mmoja huwa na jambo maalumu analofanya katika mfumo mzima wa uzalishaji bidhaa. Na ndio sababu kiwanda huweza kuzalisha bidhaa nyingi bora na kwa wakati mfupi.

Mfano huu wa viwanda unatukumbusha kuwa sawa na viungo vya mwili, sisi wanadamu tuna wajibu maalumu wa kutekeleza kwa kushirikiana na wenzetu. Vinginevyo, kila mmoja alifanya jeuri ya kushika njia yake, uzito wa safari utakuwa mkubwa kwake. Ndio maana wakasema kuwa mtu pweke ni uvundo.

(a) Fupisha ujumbe wa aya tatu za kwanza kwa maneno 100.(alama 6)

Matayarisho

Nakala Safi (alama 6)

(b) Eleza kwa maneno 140, masuala ambayo mwandishi ameibua kuanzia aya ya nne hadi ya sita. (alama 9)

Matayarisho

Nakala Safi (alama 6)

3. MATUMIZI YA LUGHA(alama 40)

(a) Tofautisha sauti zifuatazo:

” (i) /l/ na /r/ (alama 2)

(ii) /m/ na /b/

(b) Bainisha matumizi ya ‘ni’ katika sentensi ifuatayo: (alama 1)

Wasaidieni wale, walinisaidia wakati wa shida.

(c) Andika neno moja lenye silabi za muundo ufuatao: (alama 1)

Konsonanti + Konsonanti, Irabu + Konsonanti, Konsonanti, Irabu

(d) Tunga sentensi kubainisha kiunganishi kitegemezi. (alama 2)

…………. ……………….. … .. …………………

(e) Tumia neno ‘vile’ katika sentensi kama:

(i) Kiwakilishi (alama 1)

(ii) Kielezi (alama 1)

(f) Kutokana na mzizi ‘—erevu’ unda:

(i) nomino (alama 1)

(g) Nomino Zifuatazo Zilizo katika ngeli gani?(alama 2)

(ii) chanda ………………………

(h) Ainisha Virai katika sentensi ifuatayo:(alama 3)

Wale wengine watasafiri ughaibuni kwa ndege. ……………………………………………

(i) Andika sentensi ifuatayo katika hali ya umoja.(alama 1)

Nguo Walizouza madukani mwao ziliwavutia watalii. ………………………………………….

(j) Geuza sentensi ifuatayo katika hali yakinishi. (alama 1)

Makuli hawajakuarifu kwamba mizigo hiyo haikuwa yetu? …………………………………………..

(k) Akifisha sentensi ifuatayo. (alama 1=2)

lo kadio hamadi ndiye mwandishi wa kisiwa chenye tunu

(l) Andika sentensi ifuatayo katika usemi halisi (alama 2)

‘ Mama alimwita Juma na kutaka kujua namna alivyofaulu kuuzima moto huo. …………………………………………….

(m) Andika sentensi ifuatayo upya kwa kufuata maagizo. (alama 2)

Seremala alilainisha mbao. Seremala alikuwa kiwandani. (Unganisha kuwa sentensi moja inayoanza kwa ‘Mbao’ bila kubadilisha maana.)

……………………………………..

……………………………………..

………………………………………

(n) Andika kinyume cha sentensi ifuatayo kwa kuzingatia maneno yaliyopigiwa mstari. (alama 1)

Punde tu alipouliza swali hilo Koru aliingiq darasani.

………………………………………

(o) Andika sentensi ifuatayo katika hali ya mazoea.(alama 1)

Jani ambalo lilipukutika lilipeperushwa na upepo.

(p) Changanua sentensi ifuatayo kwa kielelezo cha mstari. Wakulima hawa wanapanda zao hili daima.(alama 2)

(q) Andika sentensi ifuatayo upya ukianzia kwa yambwa tendewa.(alama 1)

Andai alimnywesha babu uji kwa kikombe.

(r) Tunga sentensi moja kuonyesha maana mbili za neno somo.(alama 1)

(s) Tunga sentensi kubainisha matumizi yafuatayo ya ‘kwa’.(alama 2)

(i) sehemu ya kitu

(ii) namna

(t) Tunga sentensi moja kubainisha kishazi huru na kighazi kitegemezi. (alama 2)

(u) Andika maana mbili zinazojitokeza katika sentensi ifuatayo: (alama 2)

Fundi alimkatia Makaa utepe huo.

(v) Zimwi lilizidi kukimbia.

Shujaa aliongeza mwendo kulifikia.

(Unganisha kuwa sentensi moja kwa kutumia neno ‘kadiri’)(alama 2)

(w) Tunga sentensi zifuatazo: (alama 2)

(i) agizi

(ii) Hisishi

4. ISIMUJAMII (Alama 10)

(a) Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali.

“Karibu, karibu! Keti.

Naam, jitambulishe kwa jopo hili…

Bwana Nuru, ni jambo lipi ambalo linakufanya kuamini kwamba nafasi hii inakuafiki wewe?”

(i) Bainisha sajili ya makala haya.(alama l)

(ii) Eleza sifa nne za sajili hii kwa kurejelea makala haya.(alama 4)

(b) Wewe ni kinara wa chama cha Wanamawasiliano Bora shuleni mwako. Umepewa jukumu la kuwatangazia wenzako mashindano ya uogeleaji yakiendelea shuleni mwako. Fafanua sifa tano za lugha utakayotumia. (alama 5

(Visited 981 times, 1 visits today)
Share this:

Written by