KCSE Past Papers 2021 Kiswahili Karatasi ya 1 (102/1)

Kenya Certificate of Secondary Education Kiswahili Karatasi ya 1 – Insha

1. Lazima

Rafiki yako anasomea ng’ambo. Alipoondoka nchini, Kaunti yenu ilikuwa inakabiliwa na kutojitosheleza kwa chakula. Mwandikie barua kumweleza hatua ambazo Kaunti yenu imcchukua kutatua tatizo hill.

2. Fafanua manufaa ya kuboresha miundomsingi nchini.

3. Tunga kisa kinachodhihirisha maana ya methali ifuatayo:

Aliye kando haangukiwi na mti.

4. Tunga kisa kinachoanza kwa maneno yafuatayo: “Maskini, anaonekana kuemewa na hisia za kupoteza.

Huu mchezo wa bahati nasibu utakuja kutuangamizia kizazi,” akajisemea Kutu huku akimtazama mja aliyekuwa kainamia meza huku ameshika kichwa…

 

(Visited 2,888 times, 1 visits today)
Share this:

Written by