Karatasi Ya 3
Mwongozo Wa Kusahihisha
i. Mzungumzaji ni Mwalimu Mstaafu
ii. Anazungumza na hadhira ambayo imekukja kumuaga
iii. Yuko shuleni
II. Toni ya kuonya/kutahadharisha – si vizuri kukitia kutumbua mchanga
III.
i. Kuwadhalilisha wenzake kama vile Baraka, FEsto, Mshamba na Nangeto
anapoonyesha hali yao mbaya ya awali
ii. Kufichua njama za kifisadi- anasema pesa zilizochangishwa na rais zililiwa na
wakora kama vile akina Festo
iii. Anapewa nafasi yka Mwalimu Mosi kuhutubu lakini anamuaibisha anasema
anafurahia kuondoka kwa Mwalimu Mosi
iv. Kutotambua mchango wa Mwalimu Mosi – anasema Mosi ataondoka shule ipumzike
v. Anashindwa kustahimili changamoto shuleni
vi. Anajidhalilisha kwa kusifia suala kama vile utapeli na wizi, hajiamini – anajiita
zumbukuku asiyeweza kuimarika
vii. Anakosa kuyawajibikia maisha yake. Anamlaumu Mwalimu Mosi, anasema
umaskini wake ulisababishwa na Mwalimu Mstaafu
2
viii. Anakosa kuwajibikia Familia yake. Hatekelezi majukumu yake kama mume na
mzazi
ix. Kutelekeza familia – hakuwahi kupita kwa Mwalimu Mosi kuwajulia hali
wanafamilia yake (uk. 128)
x. Kukmhuribia Mwalimu jina kwa kusema kuwa amekioa kitoto chake (uk. 130)
b).i. Taswira – uoni – nyeupe, nyembamba
ii. TAshihisi – vi kujianika
iii. Takiriri uridiaji – Alijaaliwa mvi
iv. Tashbihi – kama theluji
v. Taashi – mvi – ishara ya hekima
vi. Kinaya
vii. Usimulizi
viii. Chuku /Udumisi
ix. Mdokezo
2. a) i. Haya ni maneno ya msimulizi
ii. Yanamhusu Sauna
iii. Sauna yumo nyumbani mwa Bi. Kangara
iv. Anahisi anakabiliwa na hatari Fulani ndipo moyo unamwenda mbio
v. Anapofungua lango anakumbana na polisi ana kwa ana.
II
i. Taswira hizi – anahisi/kikali
ii. Mwendo – anatoka nje, moyo kumwenda mbio, kusimama
iii. Usikivu – mbisho hafifu/anasikia
iv. Mguso – vipapasio
III
i. Tasbihi – anajihisi kama anayetarajia kuwa na kinyang’anyiro cha upiganaji
masumbwi
ii. Tashhisi – kusimama kwa vipapasio vya akili/moyo wake ukimwambia
iii. Mdokezo wa methali – yake ya arobaini imefika
iv. Kutumia usimulizi wa wakati uliopo – mara anasikia
v. Nahau – kumwenda mbio
b)3i. Kunyesha changamoto zinazokumba hospitali za umma. Selume anashangaa namna
alivyoweza kustahili matatizo kama vile ukosefu wa glavu hospitalini.
ii. Kuangazia suala la ufisadi. Dawa zilizotengewa hospitali zinauzwa na wasimamizi
wa hospitali (uk. 140). Ruzuku kutolewa kwa wasiostahili.
iii. Kuonyesha ukosefu wa uwajibikaji wa wasimamizi wa taasisi za umma. Hospitali
haijalipia umeme (uk. 140)
iv. Kuendeleza ploti – kupitia sadfa. Kituo kinakamilika wakati ambapo Sulume
anajiuzulu; anapata kazi na mkondo wa matukio kubadilika
v. Kuonyesha migogoro inayosababishwa na tama ya rasimlimali. Mgonjwa
analemazwa katika mapigano ya kung’ang’ania ardhi (141)
vi. Kujenga tabia za wahusika. Kwa mfano, utu wa Ridhaa. Anaanzisha kituo cha afya
na kuwapa ajira Selume na Kaizari
vii. Kuonyesha athari za matumizi mabaya ya vileo. Mwanafunzi anakufa kutokana na
pombe harame (uk 142).
viii. Kuonyesha ukengeushi. Wasomi wanashindwa kukabiliana na matatizo/changamoto
wanatumia mbinu hasi ili kujisahaulisha na hali yao duni (uk. 142)
ix. Kuangazia changamoto zinazokumba sekta ya elimu. Halmashauri ya mikopo
kutotosheleza mahitaji ya wanafunzi
x. Kuonyesha umuhimu wa mshikamano a kifamilia katika maisha ya watoto. Kipanga
anaingilia matumizi mabaya ya vileo kwa kukataliwa na aliyedhani ndiye babake.
xi. Kuonyesha athari za kufuata mila zinazorudihsa nyuma maendseleo ya kijamii.
Tuama anakasirika kwa kupashwa tohara
xii. Kuaangazia suala la ukiukaji wa haki wa zatoto. mama yake Pete kutoshughulika
kutambua kwamba binti yake amekua na mahitaji yake yamebadilika
xiii. Kuonyesha jukumu la ujamii katika kuwarithisha vijana mbinuishi. Mwanzo mpya
inawapa vijana kama vile kipanga huduma za ushauri nasaha unaoshaidia kubadilisha
tabia
xiv. Kuangazia uozo wa kijamii. Uavyaji mimba – Pete anajaribu uavya mimba.
3. a)i. Nahau – Kujitanua kifua
ii. Mdokezo wa methali – mimi ni mwana wa mhunzi na bila shaka wa mhunzi
asiposana huvuvia
iii. Chuku – kuinua tani mia moja/kufufua maiti
iv. Tashbihi/ulinganishi – kama Yule mbabe wa kivita
v. Bilagha – angeweza kuinua tani ngapi vile za chuma?
vi. Taswira – uoni – kuinua, wakitazama
vii. Mbinu rejeshi – hadithi ya Fumo Liyongo na ile ya Akavi
viii. Tabaini si tofauti
ix. Udokezaji – anadokeza ushujaa wa Liyongo hatujui ni shujaa wa aina gani
4 x. Ubanaji – Baba, babangu
xi. Utata – matumizi ya neon hivi yanaweza kurejelea dhana zifuatazo
a) Namna
b) Kimchezo
c) Bila kusumbuka
d) Palepale
e) Wakishangaa
xii. Kutumia usemi halisi na wa taarifa
b).i. Kuendeleza mshikamano/ushirikiano wa kifamilia. Mwangeka na Mwangemi
wanapendana. Wanashiriki shughuli mbalimbali
ii. Kuangazia historia ya jamii. Mwangeka anataja vita baina ya jamii yake na Akavi ili
kuwaokoa mifugo. Kutajwa kwa mashujaa
iii. Kuendeleza tamaduni kama vile utambaji. Nyanya anawahadithia kina Mwangeka
kuhusu Fumo Liyongo
iv. Usuluhishaji migogoro/kuendeleza shughuli za usuhilishaji wa migogoro katika
jkamii. Babu Msubili ni jaji wa kienyeji
v. Kudhibiti vitendo vya wanajamii/kupitisha na kuendeleza imani za kijamii. Babu
hakupenda kukutana na mwanamke asubuhi. Mama ya msimulizi anawakataza
kumpelekea uji asubuhi; anawatuma ndugu wake wa kiume
vi. Kudumisha nidhamu. Mwangeka na Mwangemi wanapomwiga Babu wanachapwa
na Babu, kasha wanakatazwa chakula.
vii. Kutoa mwongozo kuhusu namna ya kushi. Mama mwangeka na Mama Mwangemi
wanakilaani kitendo cha kukmwiga babu; wanawaadhibu zaidi ili kukomesha tabia
hii.
viii. Kudumisha mahusiano ya kijamii/kaida zinazoongoza mahusiano ya kifamilia.
Mwangeka na Mwangemi wanamwiga Babu ili kumkumbusha kwamba anastahili
kuwa mtani wao kama ilivyo desturi ya jamii yao
ix. Kuendeleza shughuli za kijamii, kwa mfano michezo ya watoto na uigizaji
x. Kendeleza imani kuhusu majukumu ya jijinsia katika jamii. Mwangeka anapobeza
kuwepo kwa shujaa wa kike (Mekatilili uk 179). Kuonyesha imani ya jamii kwamba
shujaa wa kivita sharti awe mwanaume. Babu anamkumbusha mwangeka kuwa
wanaume hawalali mapema
xi. Kuendeleza mbinu za kijadi za urekebishaji tabia/ufunzxaji wa maadili. Babu
anatumia kichapo, ambacho njia pekee iliyoaminika kumshinikiza motto kutii
xii. Kuhimiza maridhiano. Mwangeka na mwangemi wanawapa majogoo wao punje za
mahindi pamoja na kuwakumbusha asiyekubali kushindwa si mshindani (uk. 183).
5
4. a).i. Ni maneno ya Aisya/Mamapima
ii. Anawaambia wanasaagamoyo walikutana sokoni
iii. Wapo kwenye lango kuu sokoni
iv. Pombe yake imemwagwa; anajutia matendo yake ya awali
b) . i. Usambamba – Nilijua ninawaponza
Nilijua ninawapunja
ii. Tashhisi – Nilimezwa na tama
c). Ploti
i. Kupitia kwake tunaelezwa kuhusu usuli wa utoaji wa kandarasi ya uokaji keki; yna
Ngurumo walimwandama Husda
ii. Baadhi ya matukio katika maisha ya wahusika Fulani yanaangaziwa katika kibanda chake
cha pombe. Ngurumo anasema alisoma na Tunu (uk. 57). Tunaonyeshwa kuwa Siti
alikuwa mlevi hapo awali (uk. 58).
iii. Wimbo anaimba Mamapima ni kipengele cha ploti. Anautumia kuitetea kazi yake (uk
60.)iv. Anajenga mgogoro kati ya wanamabadiliko na wanaotaka hali ibakie hivyo. Tunu
anasema amekuja kuwakomboa walevi ilhali Mamapima anasema anaharibiwa biashara.
v. Matukio kwenye biahsara yake yanawezesha kujua nani aliyempiga na kumuumiza Tunu.
Ngurumo anaashiria miguu ya tunu iliyoumia (uk. 63)
vi. Kuonyesha hatima ya mgogoro baina ya viongozi na wanyonge. Anasema wamemgeuka,
wameimwaga pomebe
vii. Kuonyesha mustakabali wa Sagamoyo. Anajuta, anaomba msamaha; anaonyesha
kuibadili nia/kueleza uaminifu ake kwa Tunu; anataka kuibusu miguu ya Tunu (uk. 92).
Maudhui
i. .Anaendeleza suala la ufisadi. Anapewewa kandarasi ya kuoka keki kwa kuwa yeye ni
rafiki kya Husda
ii. Kuonyesha upujufu wa maadili. Anahusiana na Ngurumo kimapenzi
iii. Kuonyesha ukosefu wa uwajibikaji. Anauza pombe haramu huku akijua ni hatari
iv. Anaangamiza kizazi cha cijana. Kwa kuwauzia dwa za kulevya (mtu I, mtu ii
wameathirika na matumizi ya dawa za kulevya) (uk. 62)
v. Anaonyehsa matumizi mabaya ya cheo. Anapewa kibali cha kuuza pombe haramu kwa
sababu mumewe ni kikaragosi cha watawala
vi. Anaonyesha haja ya maridhiano. Anajutia matendo yake, anaomba masamaha na
kumtambua tunu (anataka kumbusu)
6vii. Kuangazia mabadiliko. Anajutia aliyotenda. Anajiunga na wanaotetea mabadiliko
viii. Anaendeleza maudhui ya tama na ubinafsi. Anauza pombe haramu bila kujali athari zake
kwa jamii. Kumweka Husda kawpani ili anufaike.
5. a)i. Wanachangia kuendeleza uchumi. Hata wanapokosa ajira, wanajiajiri. Sudi anachonga
vinyago; Ashua anauza mandazi
ii. Wanapigania haki za wanyonge. Tunu na Sudi wakiwa chuoni walikuwa viongozi wa
harakati za kupigania haki
iii. Wanawazindua wanasagamoyo kuhusu haja ya kuwa na uongozi unaozingatia misingi ya
kidemokrasia. Tunu na Sudi wanawahamasisha Wanasagamoyo kuhusu aki zao
iv. Wanaukosoa uongozi. Tunu anamkabili Majoka na kumwambia kwamba
Wanasagomoyo wana haki ya kuihsi (uk. 45)
v. Wanahimiza haja yka kuzingatia maadili ya kijamii. Ashua anaheshimu asasi ya ndoa.
Anakataa ushawishi wa Majoka
vi. Wanachangia kuboresha hali ya utendakazi katika taaluma zao. WAlimu wanagoma ili
kupata mazingira mazuri ya kufanyia kazi
vii. Wanatoa kielelezo cha uongozi ufaao. Tunu anasema kwamba wanahitaji viongozi
wanaofahamu matatizo yao
viii. Wanafunza kuhusu umuhimu wa familia na malezi. Sudi anamwambia Ashua awafikirie
watoto wao (uk. 48)
ix. Wanaunda na kuimarisha itikadi za kijinsia zinazowawezesha kuleta mabadiliko katika
jamii. Licha ya Sudi na Tunu kushukiwa kuwa wapenzi, hawalegezi juhudi zao za
kuuhamasisha umma. Sudi anachonga kinyogo cha mwanamke.
x. Kuwakosoa wanyonge ambao wanatumiwa kama vibaraka. Tunu anamuuliza Ngurumo
kipi muhimu; dhifa au kufunguliwa kwa soko. Sudi anawatanabahisha kina Boza kuhusu
suala la mijikata
xi. Baadhi yao wanaendeleza ubaguzi wa kijinsia. Ngurumo anasema hawezi kumpa
mwanamke kura.
xii. Wanasisitiza umuhimu wa elimu na ustaarabu. Ashua anasema kutoelemika kuna tatizo
(uk. 28), naye Husda anasema elimu bila ustaarabu haifai
xiii. Baadhi wanakwamiza juhudi za kupigania haki. Ngurumo anatumiwa na Majoka
kumpiga na kumnyamazisha Tunu.
b).i. Kuendeleza mgogoro wa kinafsia. Majoka anasema kuna kilio kikubwa ndani kwa ndani
(uk. 73).
ii. Kuchumuza matukio ya awali; kwa mfano kuuawa kwa Jabali (uk. 73)
iii. Kudokeza hatari iliyomnyojea Majoka – mikono yangu imefungwa kwa minyororo (uk.
73). Majoka kusema yuko katika safari ya jongomeo.
7iv. Kuonyesha udhaifu wa uongozi wa Sagamoyo. Majoka anamuuliza Daktari/Babu kama
ndiye rubani wa ombwe hilo (uk. 74)
v. Kujenga sifa za wahusika. Tunasawiriwa tama ya Husda inayomfanya kuuza pombe
haramu.
vi. Yanaangazia usaliti katiaka ndoa. Majoka anakiri kuwa anampenda Ashua; hampendi
mkewe Husda.
vii. Kuonyesha nafasi ya lmwanamke katika jamii; wanasawiriwa kama wasioweza
kutegemewa. Majoka anasema hawashikiki
viii. Kuonyesha ukosefu wa uwajibikaji wa uongozi. Majoka anasema hajashika usukani (uk.
80)ix. Kuonyehsa kuwa Wanasagamoyo wamezinduka. Majoka anasema wanaililia damu yake
(uk. 79)
x. Kuonyesha kwamba Sagamoyo haipigi hatua kimaendeleo. (uk. 81)
xi. Kuonyesha suala la mgongano kati ya utawala wa Babu na ule wa Majoka. Majoka
anasema kwamba athari ya chombo cha Babu/kinatikisa chake (cha Majoka) na
kukifanya kutaka kuubadilisha mkondo.
xii. Kutanabahisa/kumsuta Majoka kuhusu uongozi wake, na kumwonyesha haja ya
kubadilika. Babu anasema: Huoni kisima kimeingiwa paka na maji hayanyweki tena?
6. a)i. Akipanda harudi chini
ii. Hawezi kuporomoka /huanguka
iii. Amepta mbinu za kuendela kupanda (ameotesha makwezi)
iv. Makao/mahali pake ni pale juu/mamkani
v. Kushuka kwake si halali/ni haramu
vi. Hakumumiwa ila hubaki huko juu
vii. Haoni hatari wala wasiwasi
viii. Amejishikiza penye manufaa
ix. Amepanga mikakati ya kujipatia pato
x. Hata mti ukiporomoka, hushuki
xi. Hata akipigwa vita, hashuki
xii. Atakatalia juu hata akipigwa na radi
xiii. Hashuki kwa hiari
b) .i. Taswira hisi – ukweli jua mchungu/ yu furahani
ii. Taswira uoni – utabaki kutazama
iii. Taswira mguso – kugandama
8c) .i. Urudiaji silabi/ ngu, ngu, ngu (ubeti 1)
ii. Urudiaji wa neon – tangu, tangu amepanda akapanda
iii. Urudiaji wa mstari/kipande – mpanda ngazi jamani
d). i. Kufinyanga sarufi/kubananga lugha – hili mja ubaini – ubaini hili mja, mengi mazao –
mazao mengi
ii. Inkisari – ngawiraye – ngawira yake / walo – walio
e). i. Tanakuzi – mpanda – shuka, juu – ardhini
ii. Chuku – mpanda ngazi kubakia pale miaka na dahari/kushuka chini kuwa haramu
iii. Sitiari – mpanda ngazi – kiongozi anayepata mamlaka / kilelelkwenye mamlaka / ufanisi
f). i. Mistari mine katika ubeti
ii. Vipande viwili katika mishororo
iii. Vina vinabadilika kulingana na ubeti
iv. Mizaani 8,8 = 16 katika mshororo
v. Kipande cha mwisho cha ubeti kuanzia ubeti unaofuata
7 a) i. Alikuwa na uwezo wa kutenda mambo akiwa kijana, sasa hana
ii. Alikuwa na afya, sasa hana
iii. Alikuwa na ushirika wa ndugu na jamaa; sasa hana
iv. Anachoshika sic hake – sasa hamiliki lolote
v. Amepoteza baadhi ya viungo alivyokuwa navyo. Sasa hana neon
vi. Vitamu ni vichungu kwake
vii. Hana la kumfurahisha kama awali
viii. Vilivyokuwa laini vigumu
b). i. Shairi lina beti tatu
ii. Kila ubeti una mishororo saba
iii. Kila mshororo una vipande viwili
iv. Vina vya ndani na vya nje vinatiririka
v. Mizani 8,8 = 16 katika kila mshororo
vi. Kila ubeti unaanza kwa kauli; U wapi ujjana wangu
vii. Kila ubeti unajitosheleza
9viii. Kipande cha kwanza kinatoa wazo na cha pili kinakamilisha
ix. Shairi limetumia mistari kifu/toshelezi
x. Kila ubeti kuanza kwa swali la balagha
c).i. Taswira hisi – machungu
ii. Taswira uoni – tazama hii dunia
iii. Taswira mguso – laini , gumu
iv. Taswira muojo – kitamu, kichungu
v. Taswira mwendo – mayo imeshika njia
d). i. Kweli kinzani – kitamu sasa kichungu
ii. Tashhisi – afya imehsika njia
iii. Tasfida – wamehama ulimwengu
iv. Usambamba – Afya ya ujana wangu, siku ya ujanawangu.
e).i. Nafsineni – mzee/mtu aliyekonga
ii. Toni ya majuto/machungu kukata tama – U wapi ujana wangu?
8 a) Inaonyesha mwisho wa urafiki baina ya Sungura na Fisi-huo ukawa mwisho wa urafiki
wa Sungura na Fisi
b).i. Fanani kuzungumza moja kwa moja na h adhira – mjukuu wangu
ii. Matumizi ya chuki – mtu kujikwaa na mwingine kuwa ndiye anayehisi uchungu kuhitaji
kutwa kujaza tumbo
iii. Tashhisi – moyo wa fisi unamrai
iv. Methali – atanguliaye kisimani hunywa maji maenge
v. Nahau – alishika tariki
vi. Urudiaji – guu mosi, guu pili
vii. Ritifaa – sungura nazungumza na fisi na ilhali fisi hayupo
viii. Tasfida – uwezo wa kuyatoshelezea mumbile haja – badala ya – kwenda haja kubwa
ix. Kuigiza – alijikokota hivi…
x. Swali la balagha – itakuwaje…?
xi. Ucheshi – kicheko
xii. Tanakali za sauti – ndo ndo ndo!
xiii. Taswira – fisi akilia
xiv. Mtambaji kuhoji hali/ upenyezi wa mtambaji – sijui kama mjukuu wangu..
10.xv. Kuchanganya sauti ya usimulizi baina ya nafsi ya tatu hadi ya pili kupunguza masafa
ujumi kati ya fanani na hadhira
xvi. Kuchanganya nyakati (uliopita na sasa) ili kupunguza masafa ujumi.
c). i. Kuashiria mwisho wa usimulizi
ii. Kuiondoa hadhira kwenye ulimwengu wa fantasia hadi ulimwengu halisi
iii. Kuwapa kitulizo wasikilizaji/kuwaondolea watu mwemeo wa matukio ya hadithini
iv. Konyesha mwisho wa mgogoro wa hadithi ni – unaashiria mwisho wa urafiki wa fisi na
sungura
v. Kusawiri jamii ya fanani – ni wafugaji – anazungumza kuhusu ng’ombe
vi. Kuchochea wengine ili waweze kutamba hadithi
vii. Kusawiri mandhari ya jamii ya fanani
viii. Kuonyesha funzo la hadithi
d). i. Kushiriki kwa kupiga makofi
ii. Kushiriki kwa kuimba nyimbo,
iii. Kuigiza badhi ya matukio/matendo ya wahusika
iv. Kuuliza maswali
v. Kutoa mifano
vi. Hisia/wawazoonyesha usoni huweza kumfany abadilishe uwasilishaji
vii. Kuto-majibu kwa methali na vitendawili iwapo ngano itamalizikia kwa mtambaji
kuwategea vitendawili
viii. Kutoa mifano ya baadhi ya wahusika wa hadithini kutoa jamii zao iwapo wataulizwa
ix. Wanaweza kuchukua nafasi ya kuimba upya ngano hiyo