KCSE Past Papers 2018 Kiswahili Paper 2 (102/2)

Kenya Certificate of Secondary Education Kiswahili

UFAHAMU (Alama 15)

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.

“Mabibi na mabwana, ndugu wapenzi, alianza Bi. Mkesha, “huu ni mwaka wa tano tangu tufanye uchaguzi mkuu uliowapa vigoda wenzetu hawa. Katika kipindi hiki kumetokea mengi ya kujipigia kidari, pametokea pia mengi, mengi mabaya ya kuitia jamii ya Tungama izara.

Tumejipa mkono wa tahania kwa uteuzi wetu mzuri. Vilevile tumejisuta kwa uteuzi usio wa kuridhisha. Ndugu wapenzi, sina haja ya kuwakumbusha yote ambayo tumepitia; mmeyashuhudia yote.

Ila ninayotaka kusema ni kwamba malengo yetu ya kuwateua viongozi yamesalitiwa. Ndugu zangu, itakumbukwa kwamba watangulizi wetu walianza safari ya kurejesha utu wa Mwafrika wakiwa na nia thabiti ya kuwabwaga maadui watatu wa maendeleo.

Je, mnawajua maadui hao? Ni ujinga, magonjwa na umaskini.

Waanzilishi wa taifa hili, pamoja na viongozi waliowafuata walipigania huduma za bure za afya, na elimu ya bure na ya lazima kwa wote. Vijana wetu walijitoma ugani kuzamia lulu ya elimu; wakaxidhihaki vitabu hadi kufikia kilelecha cha elimu.

La kusikitisha ni kwamba elimu hii imekuwa laana kwao. Mnajua kisa na maana ya hali hii? Natija iliyotarajwa haikupatikana. Na haya si mageni kwetu. Mnajua wapo vijana humu vijijini ambao wamepiga lami kwa miaka na mikaka bila kuambulia kazi za hadhi ambazo waliahidiwa huko vyuoni.

Hatimaye hawa hawa wenye shahada mbili, na wengine hata tatu, ndio wanaokuwa matarishi wa wale ambao walichechemea masomoni.

Vijana wengine, kwa kukosa hata huo utarishi, wamearnua kuanzisha biashara rejareja ili kujikimu; wamekosa la mama, wanaamwa la mbwa. Sina haja ya kuwafafanulia kiini cha hali hii ya kutamausha.

Ni dhahiri kwamba uthabiti wa taifa lolote lile hutegemea uthabiti wa uongozi, na uaminifu wa raia wake katika kuuwajibisha huo uongozi. Hata hivyo, inasikitisha kwamba wengi wetu tuinejipoka uwezo wa kuuwajibisha uongozi kwa kuwa mawindo rahisi ya uzungukaji mbuyu.

Huu ndio uwele ambao umeufisidi utu wetu na kutusahaulisha thamani za kitaifa. Hebu niambie ewe mama mwenzangu, kuna faida gani kuuza kura yako kwa kibaba cha unga na noti ya shilingi mia moja, ati kwa kuwa unaambiwa, ‘Ukinichagua nitahakikisha kwamba ile Affirmative Action imezingatiwa?

Ipo haja gani kuchomwa na jua ukiwafuata hawa hawa viongozi, ukiwaimbia nyimbo za kuwatia raia kichaa cha shangwe ili kuwapembeja wawapigie kura? Je, faida kwako imekuwa gani? Hujangojea kwa kipindi chote hiki kusakafiwa kwa hiyo barabara uliyoahidiwa siku ulipouza kura yako? Na ile ahadi ya ‘mwenzetu’ ya kuwaajiri vijana wetu kwenye Jeshi la Wanamaji imetimia? Hatujashuhudia watu wa akraba moja wakisombwa kutoka humu lcijijini kwenda kuchukua nyadhifa katika mashirika ya umma?”

“Kweli waso hayawanamji wao, Bi. Mkesha amejikosha kweliweli,”Bi. Kuli alimwambia mwenzake Bi. Kengemeka kisha akaendelea.” Anatuambia yepi mageni ambayo masikio haya yangu yaliyokula chumvi ya miongo sita ushei ya miaka hayajasikia?”

“Anasema tumpe nafasi ajitome kwenye uwanja wa majogoo,” akajibu Bi. Kengemelca, “atakuwaje tofauti na hao wanaurne?” Hata hao wanawake tumewahi kuwapa nafasi, wakatutenda zaidi ya wanaume. Usinikumbushe kura yangu niliyoipoteza kwa kumkweza Bi. Shali kwenye usukani. Siwezi kusahau namna ile ahadi ya maji ya mabomba na kuchimbwa kwa visima ilivyoishia kwenye kauli yake tu.”

Tumetendwa sote mwenzangu,” alisema Bi. Kull, “inasikitisha kwamba dau ta masomo ya wanangu limeenda mrama huku nikikimlilia huyo huyo Bi. Shali. Kila mara tunasikia kupitia vyombo vya habari kwamba serikali imeanzisha Hazina ya Eneobunge kuyafadhili masomo ya watoto kutoka familia maskini. Lengo kuu, nasikia, ni kuhakikisha kwamba asilimia kubwa ya watoto haipati fursa ya kujiunga na shule tu, bali pia inakamilisha masomo ‘Hata hivyo, lıuu ni mwaka wa tatu tangu wanangu watatu waache masomo kutokana na ukosefu wa karo.

Na „ usidhani ni karo ya shule ya kitaifa, la, hasha! Ni karo ya shule za kutwa ambapo niliwapeleka baada ya huyu huyu Bi.Shali kunitilia huku akinitolea huko kuhusiana na ufadhili wa masomo.”

“Usinikumbushe yaliyomfika mwanangu Neema,” alisema Bi. Kengemeka huku akitwaa ukingo wa kanga yake kujipangusa machozi. “Mwana huyu alikaa nyumbani kwa muhula mzima,” akaendelea Bi. Kengenıeka,” dhiki ya kuwaona wenzake wakienda shuleni huku yeye anabaki nyumbani ikamfanya kuwa windo rahisi la mmoja wa hao wabunge, akaambulia uja uzito ambao hakuulalia wala kuuamkia.

Mwenyewe mbunge ameshika hamsini zake kana kwamba hakufanya lolote.

Mwanangu Jabali naye amehiari kuwa kibarua katika shamba la mbunge wa sasa. Mwenyewe anasema anataka kudunduiza pesa ili arudi shuleni kukamilisha mwaka wake wa mwisho. Na usidhani ni hao wangu tu waliofikwa na ya kuwafika. Tumewaona wana wa wenzetu tuliopiga foleni pamoja kuwateua hao hao wabunge, wakitumiwa kama masoko ya dawa za kulevya. Wengine wamegeuzwa walanguzi wa dawa hizi,” Bi. Kengemeka alikamilisha uzungumzi wake na kushusha pumzi kana kwamba ameutua mzigo mzito.

Hata hotuba ya Bi. Mkesha ilipofikia ukingoni, Bi. Kuli alimwambia mwenzake, “Ninavyoona ni kwamba wanasiasa wote wamefınyangwa kutoka aina sawa ya udongo. Ikitokea kwamba tutampa huyu Bi. Mkesha kura, tumpe kwa kulazimika kikatiba kupiga kura; tusiwe na matarajio makuu.

Inasikitisha kwamba vijana wetu waadilifu hawataki kujitia najisi kwa kuingilia siasa. Yule kijana wetu Angaza angekubali rai ya wazee kujitoma ukingoni tungemuunga mkono.

(a) “Malengo yetu ya kuwateua viongozi yamesalitiwa.” Thibitisha kauli hii kwa kurejelea hoja sita kutoka kwenye taarifa. (alama 6)

(b) Eleza mchango wa wanyonge katika hali ya uongozi nchini Tungama. (alama 3)

(c) Bainisha mbinu nne ambazo Bi. Mkesha anatumia kuishawishi hadhira yake. (alama 4)

(d) (i) Andika kisawe cha, ‘kuwapembeja’ kwa mujibu wa taarifa.

(ii) Andika maana ya, ‘amejikosha’ kulingana na taarifa.

2. UFUPISHO (Alama 15)

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.

Tangu jadi, jamii za Kiafrika zilikuwa na majukumu bayana ya kijinsia. Kila jamii ilipania kuyarithisha majukumu haya kwa vijana wa vizazi tofautitofauti. Katika jamii nyingi, vikao maalumu viliandaliwa ili kuwaelekeza vijana kuhusu namna ya kukabiliana na majukumu yao ya kijamii. Nyakati nyingine mafunzo haya yalitolewa katika vipindi vya burudani kama vile utambaji wa ngano. Kadhalika, maarifa ınengi kuhusu namna ya kukabaliana na majukumu na changamoto za jinsia mahususi yalitolewa kupitia sherehe maalumu za kitamaduni almaarufu miviga. Mifano ya sherehe hizi ni kama vile upashaji tohara, arusi, na hata matanga. Jamii za zamani, kama zilivyo za kisasa, zilikuwa na matarajio mahususi kwa watu wa jinsia zote.

Mathalani, katikajamiinyingine zaKiakika, mwanamumendiye aliyetarajiwakuikimu aila yalıe.

Katika kipindi cha Usasi na Kuhemera kwa mfano, mwanamume ndiye aliyekuwa na jukumu la kwenda kichakani kuwinda. Hali kadhalika, mwanamume ndiye aliyetarajiwa kufanya kazi zilizohitaji nguvu kama vile kufyeka misitu kwa ajili ya kutengeneza mashamba, kuchimba migodi, kuchonga mawe, kufua vyombo vya dhahabu na fedha, kuehonga vinyago, na kazi nyingine zilizohitaji nguvu. Mke naye alitengewa jukumu la ulezi, si wa watoto wake tu, bali pia wa mume wake, na hata jamii pana. Ilikuwa jukumu la mwanamke kubaki nyumbani kumpikia mumewe na watoto, kufua nguo na kunadhifisha mazingira.

Wakati mwingine waume wao walipojitoma msituni kupigania uhuru, wanawake ndio waliowapikia chakula na kutafuta nibinu za lcuwafikishia huko huko msituni.

Watoto wa kike walifunzwa kuzilinda jamii zao, si kwa mali tu, bali pia kwa hali. Walifiinzwa kwamba furaha na afya ya familia zao, kimwili, kihisia na kisaikolojia ilimtegemea mama.

Ndiye aliyeliakikisha kwamba familia yake imepata lishe bora, ndiye aliyekuwa mwalimu wa kwanza wa watoto wake; akawafunza namna ya kmjithamini na kuwathamini wenzao; akawafunza pia namna ya kutatua migogoro yao kwa njia ifaayo. Kwa upande mwingine, watoto wa kiume walifunzwa umuhimu wa kuwa watu wa kutegemewa na jamaa zao, pamoja na kubuni mikakati ya kuzihakikishia familia zao usalama.

Jamii ya kisasa inazidi kukua na kutwaa uchangamano, nayo mitazamo ya binadamu kuhusu masuala na hali mbalimbali inaendelea kubadilika.

Siku hizi kwa mfano, si ibra kupata kwamba majukumu ambayo awali yalikuwa yametengewa jinsia mahususi sasa yametwaliwa na jinsia zote.

Imedhihirika kwamba kupanda kwa gharama ya maisha kumezua haja ya waume kwa wake kushirikiana bega kwa bega kuchumia vyungu vya familia zao. Asilimia ya wanawake ambao wanafanya kazi za ajira katika mashirika ya umma na ya kibinafsi imepanda. Kadhalika, kinyume na zamani, idadi kubwa ya wanawake imesoma.

Hakika wapo wanawake wengi ambao wameibuka kuwa magwiji katika taaluma kama vile uhandisi, udaktari na usoroveya ambazo awali zilikuwa milki ya wanaume pekee.

Ulingo wa siasa nao umetwaa sura mpya.

Idadi ya wabunge wanawake inaendelea kupanda kila kuchapo. Wapo pia wanawake ambao wamejiunga na vikosi vya kulinda usalama; jambo ambalo halikuwa la kawaida katika jamii nyingi hapo awali. Wanaume nao wametwaa kazi ambazo awali zilitengewa wanawake pekee. Katika baadhi yajamii za Kiafrika, mwanamume ambaye alipatikana jikoni alichukuliwa kuwa anaufedhehesha ukoo.

Siku hizi si ajabu kuwapata akina baba wengine wakiziandalia familia zao vyakula. Vilevile idadi ya wanaume wanaosomea kazi ya uuguzi inazidi kuongezeka.

Pia wapo wanaume ambao wanafanya kazi ya ususi na kuwarembesha wanawake. Hali hii ya mwingiliano wa majukumu haisaidii tu kukabiliana na changamoto ya tofauti za kijinsia, bali pia hupalilia mshikamano wa kijamii. Watu wanapobadilishana zamu katika kutekeleza majukumu ya kijamii huthaminiana. Hujiona kama wanaotegemeana kwa hali zote, na kwa njia hii utangamano hujengeka zaidi. Kadhalika, kubadilishana majukumu ni njia bora ya kufidia udhaifu wa wenzetu.

Ni dhahiri kwamba kumekuwa na mwingiliano mkubwa wa kimajukumu, hali ambayo imeziwezesha jamii nyingi kufikia ufanisi mkubwa. Hata hivyo, imebainika kwamba hali hii inaelekea kumomonyoa faida ambazo jamii nyingi zimepata kwa wanaume na wanawake kuslurikiana kutekeleza majukumu anuwai.

Mathalani, wazazi wengi siku hizi wamo mbioni kutafuta elimu, ama kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya kikazi, au kwa kukamia malipo zaidi. Kuna baadhi ya wazazi ambao hujisajili kwa kazi mbalimbali, si kwa sababu wanahitaji maarifa fulani, bali kwa sababu wanataka kuwapiku wenzao katika ndoa.

Matokeo ni kwamba mume na mke wanajipoka muda wa kukaa pamoja na kufahamiana, pengo la kimahusiano nalo linajengeka, hali ambayo imesababisha kusambaratika kwa baadhi ya ndoa. Hali kadhalika imebainika kwamba, kwa sababu ya mume na mke kuwa mbioni kujiendeleza kitaaluma na kielimu, malezi ya watoto yameanza kutetereka.

 

Jukumu la kuwalea watoto na vijana limetelekezewa vijakazi, vitwana na hata vibonzo! Ibainike kwamba kila jambo sharti liwekewe mipaka. Yapo majukumu ambayo sharti yatekelezwe na jinsia maalum, yumkini kwa sababu za kimaumbile. Yapo majukumu kama vile malezi ya watoto ambayo sharti yachangiwe na kila jinsia.

(a) Fupisha ujumbe wa aya tatu za kwanza kwa maneno 80. (alama 7, 1 ya mtiririko)

Matayarisho

Nakala Safi

 

 

(Visited 389 times, 1 visits today)
Share this:

Written by