KCSE Past Papers 2017 Kiswahili Paper 1 (102/1)

Kiswahili Paper 1 (102/1)

1. (i) Hili ni swali ambalo linamhitaji mtahiniwa kuandika barua rasmi kwa mhariri.

(ii) Kaida Za uandishi Wa barua rasmi zifilatwe.

(iii) Vipengele viwili vya tungo za aina hii vishughulikiwez.

I. Muundo na mfindo.

(a) Sura ya barua kwa mhariri

(i) Anwani mbili

— ya mwandishi

— ya Mhariri Wa Gazeti la Mzalendo

(ii) Tarehe – baada ya anwani ya mwandishi

b) Mwili

ii) Utangulizi – Kongowezi/mtajo: Kwa Mhariri. ..

– Kusudi- Kiini cha barua kijitokeze kwenye mada hii.

– Aya ya kwanza iangazie kusudi la kuandika.

– Hoja zijadiliwc kwa kupangwa kiaya. Kila hoja ijadiliwe na kukamilika kwenye aya mahsusi.

iii) Hitimisho

Mtahiniwa ahitimishe rnawazo yake. Maoni yake kuhusu kiwanda hiki yajitokeze.

iv) Kimalizio

Sahihi, jina na cheo cha mwandishi kijitokeze.

(b) Mtindo

Hii ni barua ya maoni wala si ya malalamishi. Hoja zijadiliwe kwa namna ambavyo msimamo wa mwandishi utajitokeza. Lahaja sanifu ya Kiswahili itumiwe. Urasmi udumishwe.

Tanbihi

Ikumbukwe kwamba barua hii bado haijachapishwa katika gazeti, hivyo sharti iwe na anwani zote mbili.

Mhariri ndiye auayehariri baadaye na kutoa mojawapo. Mtahinjwa akiandika anwani moja atakuwa amepungukiwa kimuundo.

II. Maudhui

Mtahiniwa aonyeshe faida na hasara/matatizo yanayoweza kutokana na kiwanda hiki. Baadhi ya hoja ni:

Faida

(i) Kusaidia katika ujenzi

(ii) Kuboresha makazi

(iii) Kubuni nafasi za kazi

(iv) Riaia kindandaki kupata soko kwa bidhaa, kama vile chakula, zinazozalishwa humo

(v) Kuchochea kuirnarishwa kwa miundomsingi

(vi) Husaidia ukuaji wa viwanda vingine vinavyosaidia shughuli za kiwanda hiki.

(vii) Kukuza utangamano kati ya wageni na raia

(viii) Kuwafunza//kuwarithisha raia stadi Za ufyatuaji matofali kwa njia ya kisasa.

(ix) Kupunguza idadi ya vijana wanaohamia mijini kutafuta kazi.

(x) Kudhibiti visa vya ukosefu wa usalama, kutokana na vijana/Watu ambao hawana ajira.

(xi) Kuimarisha stadi ya utafiti- raia kutafuta njia endelevu za kucndeleza kiwanda hiki baada ya Wageni kuondoka

(xii)Kupalilia stahamala ya kij amii- raia na wageni kujifunza kutambua na kuheshimu tofauti zao za kitamaduni

Hasara

(i) Huenda wageni wakaja na wafanyakazi Wao, hivyo kutowafaidi Wenyeji.

(ii) Huenda kikaua viwanda vingine vya aina hii.

(iii) Kuzorota kwa maadili, hasa wafanyakazi Wa kigeni wanapotagusana na Wenyeji kwa njia isiyofaa.

(iv) Kupalilia ajira ya watoto; baadhi ya vijana kuvutiwa na pesa na kujiunga na shirika hili

(v) Kukatishwa kwa masomo ~ vijana kuacha shule ili kufanya kazi

(vi) Ndoa za mapema- baadhi ya vijana huenda Wakaacha masomo na kuolewa wakiwa wachanga.

(vii)Kinaweza kupalilia ukosefu wa usalama- baadhi ya watu kutaka kuwaibia wenye kiwanda.

Tanbihi

i) Mtahiniwa aangazie angaa changamoto mbili.

ii) Hitimisho ionyeshe msimamo wa mwandishi. Pengine aonyeshe kwamba japo kuna hasara natija inazidi hasara hii. Anaweza kuipongeza serikali kwa kiwanda hiki.

iii) Kaida nyingine zote za usahihishaji Wa insha zizingatiwe kama ilivyo kwenye mwongozo wa kudumu.

1. Umuhimu Wa vyama vya wanafunzi

Huwezesha wanafunzi:

(i) Kupalilia vipawa vya uongozi — kwa mfano kupitia vyama vya riadha ambapo kuna mwanafunzi ambaye ni kinara.

(ii) Kukabilina na changamoto — kwa mfano Chama cha Washauri Marika ambacho hueleke- za wenzao kuhusu namna na kutatua matatizo.

(m) Kupalilia maadili ya kidini- kwa mfano kupitia vyama vya kidini kama vile CU, YCS, CA.

(iv) Kukuza utangamano- wanafunzi wanapokuja pamoja katika shughuli za chama.

(v) Huimarisha mbinu za kushawishi, kwa mfano kupitia Chama cha Mjadala.

(vi) Kujiimarisha kielimu — kupitia Chama cha Mjadala/Mdahalo ambapo wanafunzi hub- adilishana maarifa.

(vii) Kutumia nishati kwa njia chanya- Badala ya kuingilia vitendo viovu Wanaweza kujiunga na vyama kama vile vya lmhifadhi mazingira shuleni.

(vii) Kuimarisha ubunifu — kwa mfano kupitia Chama cha Waandishi/Uchapishaji.

(ix) Kuelekezwa kitaaluma ~ kwa mfano kupitia Chama cha Viongozi Chipukizi na Chama cha Wakulima ambavyo hushughulikia masuala ya kitaaluma.

(x) Kujenga ukakamavu na kujiamini — Chama cha Drama.

(xi) Kujipumbuza — Chama cha Drama.

(xii) Kuj enga stahamala — hali ya kuwakubali Wengine jinsi walivyo- kupitia mitagusano yao katika shughuli za chama.

(xii) Humwezesha mwanafunzi kuratibu muda Wake ipasavyo ili kukabiliana. na majukumu ya vyama hivi pamoj a na mahitaji ya masomo.

3. Kisa kidhihirishe maana ifuatavo

Jambo, hata likawa gumu vipi, likifanywa kwa kurudiwarudiwa mwishowe hufaulu.

Au

Hata mtu akikabiliwa na hali gumu vipi, na atie bidii kuitatua hali hiyo; asikate tamaa katika kuitatua, mwishowe hufanikiwa.

Ruwaza zifuatazo zinaweza kujitokezaz

(i) Mhusika/msimulizi azaliwe katika familia maskini, apate tatizo la karo, asikate tamaa, ajitahidi masomoni na mwishowe kufanikiwa.

(ii) Mzazi awe na mtoto aliyepotoka kimaadili. Ajaribu kumrckebisha. Hali iwe ngumu, asi- kate tamaa, mwishowe afanikiwe kumrekebisha.

(iii) Nchi ikabiliwe na tatizo la mkurupuko wa ugonjwa, madaktari waj aribu kwa udi na uvum- ba kupata tiba, rnwishowe wafanikiwe.

(iv) Msimulizi/mhusika awe mwenye mahitaji maalum, ajaribu kukabiliana na adha zake, abaguliwe, asikate tamaa, mwishowe afanikiwe rnaishani/kitaaluma.

(v) Mwanasiasa ajaribukupata kiti cha ubunge, akose mara mbili au tatu, asikate tamaa, awa- nie mara kwa mara, mwishowe achaguliwe.

(vi) Mhusika atafute kazi kwa muda, asipate, aj aribu bila kukata tamaaa, mwishowe afanikiwe.

Tanbihi

Kwa vyovyotc vile insha lazima ionyeshe pande zote mbili za methali. Ugumu wa jambo ujitokezc, bidii au juhudi za kulishughulikial kutokata tamaaa kujitokeze, hatimaye mafanikio yaonekane.

4. (i) Hii ni insha ya mdokezo.

(11) Inadokeza kwamba msimulizi ameyatenda makosa ambayo yanastahili kumfanya ajute.

(11) Hata hivyo amekata shauri kujirekebisha.

Hali zifuatazo zaweza kujitokeza

(i) Msimulizi azembee masomo, asifikie lengo la kielimu, atake kujuta lakini ajiase.

(ii) Msimulizi atoroke kwao, ajiingize kwenye anasa. Pengine atunge mimba au aingilie matumizi mabaya ya dawa. Afikie mporomoko, lakini aamue kujirekebisha.

(iii) Mhusika ajiingize katika ugaidi bila kujua. Ang’amue baadaye kuwa kapoteza utu wake. Atake kujuta, ajiase na kujirekebisha.

(iv) Mwanafunzi atoroke shule, apatikane na mwalimu, aadhibiwe, pengine afukuzwe shule.

Ateseke. Atake kujuta lakini ajikanye nakuamua kuyajenga maisha upya. (V) Mhusika ashiriki mauaji, asijulikane. Aishi kwa kusumbuliwa na dhamiri, anyong’0nyee ki- hali na kimwili, afikie uamuzi wa kujirekebisha.

(vi) Mhusika awe mraibu wa vileo, azembee kazi, afi1twe, ateseke, lakini awe na azima ya ku- jirekebisha.

(vii) Mtahiniwa adanganye katika mtihani, agunduliwe, ibidi arudie masomo katika kiwango hicho

Tanbihi

(i) lakini awe na nia ya kujirekebisha.

(ii) Kisa kioane na mwisho aliopewa.

(iii) Asichopeke tu mwisho huu.

Kisa kidhihirishe tatizo/matatizo ambayo yanasababisha mhusika/msimulizi kufikia kilele cha kuvunjikiwa au kuteseka.

(iv)Anapofikia hali hii ndipo moyo unapomwelekeza kukata tamaa. Hata hivyo, anataka kurekebisha mambo, Ndipo anahitimisha kwa kauli hii.

(v) Kisa sharti kiwe katika nafsi ya kwanza, umoja. Hata hivyo, msimulizi anaweza kutumia day- olojia za Wahusika kuendeleza kisa. Katika hali hii nafsi ya tatu inaweza pia kutumiwa.

 

(Visited 1,309 times, 1 visits today)
Share this:

Written by