Karatasi ya 3
FASIHI
SEHEMU A : FASIHI SIMULIZI
Lazima
(a) Soma utungo ufilatao kisha ujibu maswali.
Hadithi ya Jabari inasimuliwa na jamii nyingi. Jabari alizaliwa kashika mkuki mkononi. Mawio ambayo kilio chakc, ambacho kwa kweli kilikuwa mugurumo, kilipopasua anga, nyota kubwa ilianguka kutoka mbinguni. Ulimwengu mzima ulitetemeka na kutwaa giza.
Hata kabla mama mtu hajampa ziwa, Jabari alikuwa amevuvumuka ua kuwa ghulamu wa miraba minne. Haikuchukua muda, hata vita kati ya jamii ya Sule na Suna vikaanza; kikosi cha Sule cha wapiganaji mia moja kikawajia vijana wa Suna kwa sime na nyuta. Jabari aliwakabili kwa konde moja pekee, akakirambisha dongo kita kizima
(i)Bainisha kipera cha utungo huu. (alama 1)
……………………..
(ii)Toa sababu mbili kuthibitisha jibu lako la (i)hapa juu. + (alama 1)
……………………..
(iii)Eleza manufaa sita ambayo jamii itapata kwa kukirithisha kipera hiki kwa vizazi vijavyo. (alama 6)
……………………..
(b) Soma utungo ufuatao kisha ujibu maswali.
Ndimi Mwimo mdumishaji ukoo
Ndimi ndovu mtetemesha ardhi
Aliyegigang vita, ukoo kuauni
Ziliporindima zangu nyayo
édui alinywea, mafahali na mitamba akatukabidhi
Kwenye misitu sikuwa na kifani
Paa na hata visungura
vilijikabidhi kwangu
kwa kuinusa tu mata
Nani aliyewahi
ngomani kunipiku?
Makoo hawakunisifu, wakalilia nikaha?
Kwenye nyanja za michuano
nani angethubutu, ndaro kunipigia?
Sikuwabwaga chini, kwa yangu maozi, hata kabla hatujavaana?
(i) Andika aina ya sifo hii. (alama 1)
………………………
(ii) Bainisha shughuli mbili za kiuchumi na mbili za kijamii zinazoendelezwa na jamii inayosawiriwa na utungo huu.(alama 2)
………………………
(iii) Eleza mambo matano ambayo yanaweza kuzingatiwa ili kufanikisha uwasilishaji wa mungo huu .(alama 5)
………………………
(c) Eleza faida nne za matumizi ya nyimbo katika uwasilishaji wa ngano. (alama 4)
………………………
SEIIEMU B: RIWAYA
K. Wllibora: Kidagaa Kimemwozea
Jibu swali la 2 au la 3.
2. “Moyo ulimpapa na kijasho chcmbamba kumtekenya juu ya mwanzi wa pua. Akahisi uchungu wa mwiba wa kujidunga.”
(a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
……………………
(b) Huku ukirejelea riwaya hii, fafanua kwa kutoa hoja nane, namna anayelengwa na kauli hii alivyojidunga miiba. (alama 16)
…………………………..
3. (a) “Imani ni kielelezo cha vijana waliowajibika.” Thibitisha kauli hii kwa kurejelea mifano kumi kutoka Kidagaa Kimemwozea. (alama 10)
…………………………..
(b) “Nadhani Mzungu pale alipo hana budi kutambua ukomavu Wa Mwafiika katika kila sekta ya maisha”
Onyesha kinyume katika kauli iliyopigiwa mstari kwa kurejelea uongozi wa Tomoko (alama 10)
…………………………..
SEHEMU C: TAMTHILIA
T. Arege: Mstahiki Meya
Jibu swali la 4 au la 5. 4. “Kushindana naye ni kama kushindana na ndovu. Utapasuka”
(a) (i) Eleza muktadha wa dondoo hili.(alama 4)p> …………………………..
(ii) Bainisha tamathali moja ya usemi inayojitokeza katika dondoo hill.(alama 2)
…………………………..
(b) Kwa kurejelea hoja saba, thibitisha kwamba kushindana na anayerejelewa na kauli hii ni sawa na kushindana na ndovu.(alama 14)
…………………………..
5. “Wahenga wanasema dawa ya adui ni kummegea unachokula.” (a) (i) Andika suala linalodokezwa na kauli iliyopigiwa mstari.(alama 2)
……………………….
(ii) Jadili hoja nane zinazoonyesha namna suala hili linavyozorotcsha hali ya maisha Cheneo.(alama 8)
………………………
(b) Jadili jinsi vyombo vya usalama vilivyotumiwa kuuendeleza uongozi wa Cheneo.(alama 10)
……………………..
SEHEMU D: USHAIRI
Jibu swali la 6 au la 7. 6.Soma shairi Iifuatalo kisha ujibu maswali.
Daima alfajiri na mapema
Hunipitia na jembe na kotama
Katika njia iendayo kondeni
Kama walivyofanya babuze zamani;
Nimuonapo huwa anatabasamu
Kama mtu aliye na kubwa hamu
Kushika mpini na kutokwa jasho
Ili kujikimu kupata malisho.
Anapotembea anasikiliza
Vidcge vya anga vinavyotumbuiza
Utadhani huwa vimemngojea
Kwa usiku kucha kuja kumwimbia;
Pia pepo baridi kumpepea
Rihvi ya maua zikimletea
Nao umande kumbusu miguu;
Na miti yote hujipinda migongo
kumpapasa, kumtoamatongo;
Na yeye kuendelea kwa furaha
kuliko yeyote ninayemjua
Akichekelea ha ha ha ha ha ha
Na mimi kubaki kujiuliza
Kuna siri gani inayomliwaza?
Au ni kujua au kutojua?
F uraha ya mtu ni furaha gani
katika dunia inayomhini?
Ukali wa jua wamnyima zao
Soko la dunia lamkaba koo;
Dini za kudhani zamsonga roho
Ayalimia matumbo ya waroho;
Kuna jambo gani linamridhisha?
Kama si kujua ni kutokujua
Laiti angalijua, laiti angalijua!
(T. Arege)
(a) Eleza hali ya mzungumziwa katika shairi hili. (alama 4)
……………………..
(b) Huku ukitoa mifano, onyesha aina mbili za uhuru wa kishairi uliotumiwa katika shairi hili.(alama 2)
……………………..
(c) Fafanua aina tatu za taswira ukirejelea ubeti wa pili.(alama 3)
…………………..
(d) Eleza umuhimu wa maswali ya balagha katika shairi hili.(alama 2)
…………………
(e) Bainisha vipengele vifuatavyo vya kimtindo katika shairi hili:(alarna 3)
(i) tashhisi
………………………
(ii) kinaya
………………………
(iii) tashbihi
……………………….
(f) Eleza toni ya shairi hili.(alama 2)
………………………
(g) Bainisha nafsineni katika shairi hili.(alama 1)
………………..
(h) Changanua muundo wa shairi hili.(alama 3)
……………………….
7.Soma Shairi lifixatalo kisha ujibu maswali.
T. Arege: Mwili
Leo kitaka nifike, natamani, ila wauma mwili
Kwa kazi nihusike, samahani, unahiliki mwili
Napenda nihesabike, makundini, ila huwezi mwili.
Vitisho amw kelele ninavicha, kwa nafsi na mwili
I1a , umechacha, na kuudhili mwili
Msikose simile, magalacha, si gurudumu mwili.
Vingekuwepo viraka, kuutia, ngeushuruti mwili
Kifundi kivipachika, kuingia, hata kuridhi mwili
Upya ukaungilika, kuvutia, roho na wake mwili.
Lakini kamwe haiwi, kuvipata, vipande vyake mwili
Sihofu kupata mawi, sitajuta, kupigania mwili
Hata kufutwa sikawi, nitakita, kidete nao mwili.
Kazi ninaithamini, ni hakika, akilini na mwili
Ila kamwe siamini, kusagika, damu, jasho na mwili
Uwele hususani kioheka, nguvu hitishi mwili.
(a) Eleza dhamira ya mtunzi wa shairi‘hi1i. (alama 4)
……………………..
(b) Fafanua mbinu nneza lugha zilizotumiwa katika shairi hili. (alama 8)
……………………..
(c) Eleza toni ya shairi hili.(alama 2)
………………………
(d) Ni nani anayezungumziwa na nafsineni katika shairi hili? (alama 1) (e) Eleza bahari ya shairi hili kwa kurejelea vipande. (alama 2)
……………………….
(f) Andika ubeti wa mwisho kwa lugha ya nathari. (alama 3)
………………….
SEHEMU E: HADITHI FUPI
K. Walibora na S. A. Mohamed (Wah) : Damu Nyeusi na Hadithi Nyingine
“Mizizi na Matawi” (A. Abdulla Ali)
8. (a) “Mwisho, naomba sote tusameheane kwa dhati.”
(i) Fafanua muktadha Wa dondoo hili. (alama 4)
………………………..
(ii) Jadili umuhimu wa hotuba ya mzungumzaji katika hadithi hii. (alama 8)
…………………………..
(b) Onyesha jinsi hadithi, “Mke wangu” ilivyotumia kinaya kufanikisha ujumbe Wake. (alama 8)
…………………………..