KCSE Past Papers 2015 Kiswahili Paper 2 (102/2)

Karatasi ya 2

LUGHA

UFAHAMU: (Alama 15)

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.

Siku moja nilifika kumwona babu yangu kule kwetu kijijini bila kumtolea taarifa mbele. Nilipofika nilimkuta amevaa magwanda yake yaliyokula chumvi hadi yakakinai. Alinitazama huku akitabasamu akisema, “Tabia hii ya kuja kwako bila taarifa utaikoma. Ukiendelea hivi utakuja kwenda kwa wakwe wako upate ndio wanakwenda uchi

Kauli hii ya babu ilinifanya kucheka. Tulisalimiana huku tukipigana pambaja. Harufu ya manukato niliyojirashia asubuhi hiyo ilikutana na kuchanganyika na harufu ya jasho lake. Baadaye tuliingia ndani, tukaketi kwenye makochi yaliyokuwa yameanza kuonyesha dalili za kuchoka. Baada ya kuulizana habari za kimsingi nilitaka kujua alipokuwa nyanya.

“Nyanyako ameenda kumwona jirani yetu mgonjwa. Amepata ajali akitoka mjini alikokuwa ameenda kuwatembelea wajukuu wake. Raha yote ya kuwaona iligeuka karaha.” Alinyamaza kidogo, akaguna , kisha akaendelea, “Barabara hizi , sijui mwaziita ‘haibei’ , zimewala watu wetu. Huwezi kuwahesabia vidole tena.”

Kwa muda nilikosa la kusema. Niliona niubadili mkondo wa mazungumzo. Nilianza kwa kumwclcza kuwa mazingira ya kijijini yalipendeza. Kwa kweli mandhari yale ya kijani kote hadi upeo wa macho yalinisisimua sana. Sauti za ndege zilikuwa mfano wa muziki wa chini uliochezwa ili kuyapamba mazungumzo yctu. Mara mojamoja nilitckwa na sarakasi ya jogoo aliyetanua mabawa yake na kukaribia kuzungumza, utadhani ni sauti ya mwanadamu. Nilipokuwa ninamtazama yule jogoo, nilishtukia mkono wa babu ukiushika wangu, akaniongoza nje akiscma, “Haina haja kuyamezameza mate. Huyu jogoo ni wako. Leo tutamfanya kitoweo kwa ajili yako. Najua kule mjini mnakula kuku wa miigizo tu. Faida yao kwa mwili ni duni.”

Tulishirikiana kumkamata yule jogoo lakini baada ya muda nilichoka. Moyo wangu ulikuwa unapiga kwa nguvu ajabu. ,b>Niliona kisunzi, nikakaa. Nikiwa ninajipumzisha chini ya kivuli cha mpera nilisikia sauti za watoto waliokuwa wamejiunga na babu kumkamata yule jogoo.

Tukiwa tunasubiri chakula cha mchana, niliona hii kuwa fulsa mufti kumweleza babu kwamba nilifika kusudi niende naye mjini. Nilipolitamka tu hili alicheka sana. Aliniambia, “Mji ni wenu nyinyi. Sisi watu wa shamba raha yetu ni kufukuzana na kazi hizi za sulubu. Kwenda kukaa mjini na nguvu zote hizi faida yake nini? Nasikia siku hizi huko mjini kuna misongamano ya magari isiyoisha. Kuna haja gani kwenda kushinda kwenye gari kuharibu muda wako kwa sababu ya msongamano? Mimi hapa kwangu nikitaka kwenda kuzitekeleza shughuli zangu sipati kizuizi. Ninakwenda tu.”

“Sikiliza babu,” nilimwambia, “mji una raha yake. Wingi Wa magari ni ishara ya maendeleo. Uwezo wa kifedha wa watu uko juu kuliko wa hapa kijijini. Leo hii mtu akipatwa na dharura ya ugonjwa hapa, kijiji kitafanyé takilifu kumfikisha hospitalini. Mjini usafiri upo kila mahali Wakati wowote.”

“Kule mjini mnadai kuona mwanga na kuujua ustaarabu ila mmcnoa,” alisema babu, “maisha ycnu,afadhali ndegc warukao angani. Ni kama mnachupa kutoka upande mmoja hadi mwingine, kana kwamba mnaendeshwa kwa nguvu za mtambo usioonekana. Jamaa hawajuani tena. Mizizi yenu hamuitambui. Mmekuwa mithili ya miti inayopcndeza lakini isiyo na mizizi ya kutosha. Upepo hafifu uvumapo inalemewa na kujibwaga chini. Jc, huo ndio ustaarabu? Ustaarabu kwetu sisi watu wa hapa kijijini ni mtu kuwaamkua wenzake kila kukicha. Ni kujuliana hali. Ni kuombana kibaba cha unga au kibakuli cha mboga. Tunaishi tukijuana, si majina na sura tu, bali pia hata upishi wctu. Nyinyi mnaishi pasi na kujua majirani Wenu. Je, wcwe hukuona hata kuku wangu hawa wanatangamana?”

Swali hili lilipoachiliwa nilihisi kama aliyetwikwa nanga. Kijasho chembamba kilinitoka. Kwa bahati nzuri meza ilikuwa imeisha kuandaliwa; kipindi cha kupambana mezani kikawadia. Nilipokuwa nikila nilitambua kitu kimoja; yule kuku alikuwa na ladha ya kupendeza, tofauti na tuliozoea kuwala kule mjini. Ila nililoliona tu ni kuwa alikuwa mgumu kidogo. Nilipokuwa nikilifikiria hili niliisikia sauti ya babu tena.

“Chunga asikung’oe meno. Huyu ni kuku hasa. Atakusaidia kuimarisha meno. Hutakuwa na haja ya kwenda kumwona daktari wa meno. Sisi hapa hata kushiriki chakula kunatukumbusha kuwa kila shughuli ni kazi tosha. Hatuna muda Wa kulaza damu.” Alichukua bilauri ya maji, akapiga tama, kisha akaendelea kuinyofoa sima yake ya bada.

(a) Huku ukirejelea kifungu, fafanua faida sita utakazopata ukiishi shamba. (alama 6)

…………………………

(b) Eleza mtazamo wa wahusika wafuatao.kuhusu mji:

(i) msimulizi (alama 3)

……………………

(ii) babu (alama 4)

……………………

(c) Andika maana ya fungu lifuatalo la mancno kwa mujibu wa taarifa: (alama 1)

kwenda kwa wakwe wako upatc ndio wanakwenda uchi

………………………..

(d) Andika kisawe cha: Niliona kisunzi(alama 1)

………………………..

2. UFUPISHO: (Alama 15)

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.

Katika ulimwengu huu tunaoishi wenye hekaheka nyingi, mwanadamu anaendeshwa na maisha mfano wa gurudumu la gari. Kwa watu wenye kufanya kazi katika mazingira ya ofisi ambapo wanaketi mchana kutwa, mazoezi ni muhimu sana. Baadhi ya watu huona fahari wapigapo tai na kuelekea au kutoka kazini kwa gari. Tabia hii ya mwanadamu inamsahaulisha kuwa mwili wake ulidhamiriwa kufanya mazoezi ya viungo kwa kutembea au kufanya kazi zenyc kuhitaji misuli kupashwa moto. Watu wengi hawana habari kuwa mazoczi yana faida tele kwao.

Wataalamu Wa sayansi wamebainisha kuwa watu wanaoidhiki miili yao kwa mazoezi ya mara kwa mara huishi zaidi kuliko wasiofanya mazoezi. Watu hawa huwa wamo katika hali nzuri ya afya na wenye nguvu kuliko wale ambao hawaishughulishi miili yao kwa mazoezi au kazi zinazohitaji utumiaji nguvu.

Ni dhahili kwamba mazoezi huchochca kuundwa kwa seli mpya za ubongo. Utafiti wa kisayansi umcbainisha kuwa sehemu za ubongo zenye kusisimuliwa kwa mazoezi ndizo hutckeleza jukumu la kukumbuka na kujifunza. Bila mazoezi sehemu hizi zitashindwa kukumbuka au kujifunza maarifa mapya. Vile vile, imethibitishwa kwamba watu wanaoshiriki shughuli zenye kuwahitaji kutumia nguvu hutia fora katika mambo yanayowahitaji kukumbuka, kufanya rnaamuzi, pamoja na kusuluhisha matatizo.

Hali kadhalika, mazoezi huimarisha siha ya binadamu. Mathalani, matatizo ya moyo yanaweza kukabiliwa kwa kufanya mazoezi ya viungo. Kufanya mazoezi mara kwa mara huufanya moyo kuwa imara na kuuwezcsha kutekeleza jukumu lake ipasavyo. Ifahamike kwamba moyo wenye siha huwcza kupiga kiasi kikubwa cha damu bila ya juhudi kubwa. Hili bila shaka litamkinga binadamu dhidi ya kulemewa na kazi.

Isitoshe, kushiriki mazoezi na shughuli zcnye kutumia nguvu mara kwa mara huuweka mwili katika hali nzuri ya kupambana na magonjwa. Utafiti wa kisayansi umeonyesha kuwa shughuli kiasi zinazomhitaji mtu kutumia nguvu, pamoja na upunguzaji wa uzito, na uzingatiaji wa lishe bora, huweza kupunguza uwczekano wa kupata ugonjwa wa kisukari kwa baina ya asilimia 50 na 60. Mazoezi hayapunguzi tu shinikizo la damu, bali pia hatari ya kupata kiharusi. Aidha, kufanya mazoezi mara kwa mara husaidia kudhibiti uzani wa mwili. Mtu anapokula kiasi cha chakula kinachozidi mahitaji yake ya kimwili huweza kujinenepea na kushindwa kutekeleza majukumu ya kimsingi. Mazoezi husaidia kuzichoma kalori zisizohitajika mwilini. Hatua hii, licha ya kusaidia kupunguza uzani, huvisisimua viungo vya mwili. Matokeo ya haya ni utendakazi Wa hali ya juu bila kuchoka. Vilevile mwili unaofanya mazoezi haudorori. Umbo la mtu anayefanya mazoezi hupendeza.

Juu ya hayo, kufanya mazoezi mara kwa mara husaidia kujenga misuli yenye nguvu. Misuli inapokuwa na nguvu tunaweza kulifanya jambo kwa muda mrefu bila kuchoka. Mbali na misuli kuimarika, mazoezi na shughuli zinazohitaji utumiaji nguvu husukuma hewa na virutubisho kwenye viungo mahususi vya mwili na kuvisaidia kufanya kazi vyema zaidi.

Hali kadhalika, mazoezi husaidia kujenga mifupa. Kadiri binadamu anavyoshiriki katika shughuli kama vile kuruka, ndivyo anavyoiimarisha mifupa yake. Shughuli ya aina hii huipa mifupa uzito ambao unaiwezesha kukua na kujengeka ikiwa na nguvu. Mazoezi pia hukawiza kudhoofika kwa mifupa.

Kunyooshanyoosha viungo nako huchangia kuufanya mwili kuwa imara na wenye kunyumbuka. Hali hii ya mwili hupunguza uwczckano wa kupata majeraha. Mwili usionyumbuka humfanya mtu ashindwe kutekeleza hata shughuli nyepesi zinazomhitaji kutumia nguvu. Si ibra kupata kwamba kuitekeleza shughuli ndogo tu humfanya mtu kupata maumivu.

Utulivu wa akili nao huweza kupatikana kwa kufanya mazoezi. Imcbainishwa kwamba kufanya mazoezi kwa angalau dakika thelathini kwa muda wa baina ya siku tatu na tano kwa wiki hupunguza kwa kiasi kikubwa, dalili za unyong’yonyevu. Na je, Wajua kwamba kufanya mazoezi husaidia kupata usingizi? Mazoezi ni mfano Wa bembea inayokutuliza na kukupa usingizi.

Mke ni nguo, mgomba kupaliliwa. Nao mwili Wa binadamu, kama mgomba, unahitaji kushirikishwa katika mazoezi ili kuuwezesha kuwa na hamu ya kutenda kazi.

(a) Kwa kurejelea aya tano za kwanza, eleza matatizo ya kiafya yanayoweza kupatikana kwa kutofanya mazoezi. (maneno 100) (alama 9, 1 ya mtiririko)

Matayarisho

…………………………..

Nakala Safi

………………….

(b) Fupisha ujumbe wa aya tano za mwisho kwa maneno 80. (alama 6, 1 ya mtiririko)

Matayarisho

………………

Nakala Safi

………………

3. MATUMIZI YA LUGHA: (Alama 40)

(a) Andika sauti zenye sifa zifuatazo: (alama 2)

(i) nazali ya kaakaa laini

……………………………..

(ii) kikwamizo ghuna cha mdomo na meno

……………………………..

(iii) irabu ya nyuma, Wastani

……………………………..

(iv) kiyeyusho cha kaakaa gumu

……………………………..

(b) Bainisha silabi katika neno: wanyweshavyo. (alama 1)

……………………………..

(c) Andika upya sentensi ifuatayo kwa kubadilisha nomino zilizopigiwa mstari kuwa vitcnzi.

Wafanyakazi wote watafanyiwa Qjhmini ili kupata sulghg ya matatizo hayo. (alama 2)

……………………………..

(d) Andika sentensi ifuatayo katika umoja.

Mkihifadhi nafaka hizo vizuri maeneo haya yatakuwa na vyakula vya kutosha.(alama 2)

……………………………..

(e) Andika neno moja lenye mofimu zifuatazo: (alama 2)

nafsi ya kwanza wingi, wakati uliopita, yambwa, mzizi, kauli tendesha, kauli tcnda

……………………………..

(f) Tunga sentensi kuonyesha matumizi yafuatayo ya neno: kama (alama 2)

(i) kiunganishi

……………………………..

(ii) kihusishi

……………………………..

(g) Tunga sentensi yenye kishazi kirejeshi ambacho ni kivumishi. (alama 2)

……………………………..

(h) Andika sentensi ifuatayo katika hali ya ukubwa.(alama 1)

Nyumba hizo zilijengwa mbali na mji ule.

……………………………..

(i) Tunga sentensi yenye muundo ufuatao (alama 2)

nomino ya jamii, kirai kihusishi, kitenzi kishirikishi,kielezi cha mahali

……………………………..

(j) Andika sentensi ifuatayo kulingana na Inaagizo. (alama 1)

Chakula kinachozalishwa kwa njia za kiasili kina viinilishe vingi.

Anza kwa: Viinilishe vingi

……………………………..

(k) Tumia viwakilishi badala ya nomino zilizopigiwa mstari.

Mtalii atazuru mbuga. (alama 1)

(l) Akifisha sentensi ifuatayo

basi mwanangu akascma daudi hivyo ndivyo tunavyoweza kufikia vision 2030 wewe waonaje (alama 3)

……………………………..

(m) Unganisha sentensi zifuatazo kwa kutumia kiunganishi cha wakati.

Beti alijishindia tuzo. Beti alishiriki katika utunzaji wa mazingira. (alama 1)

……………………………..

(n) Tumia ‘kwa’ katika sentensi kuonyesha: (alama 2)

(i) sababu

……………………………..

(ii) pamoja na

……………………………..

(o)Changanua sentensi ifuatayo kwa kiclelezo cha matawi.

Mvua ilinyesha tulipokuwa tukilima. (alama 3)

……………………………..

(p)Andika sentensi ifuatayo katika kauli ya kutendewa.(alama 2)

Malik alipuliza siwa akiwa kwa Shaka.

……………………………..

(q)Onyesha matumizi ya ka katika sentcnsi ifuatayo:(alama 1)

Mumbi alitia embe kapuni likaiva.

……………………………..

(r)Andika sentensi ifuatayo katika hali ya mazoea.(alama 2)

Mmomonyoko wa udongo ulipozuiliwa mashamba yalinawiri.

……………………………..

(s)Tunga sentensi moja kutofautisha maana ya vito na fito. (alama 2)

……………………………..

(t)Methali: Mzigo wa mwenzio ni kanda la usufi, huambiwa mtu anayezidharau shida za wengine. Mtu asiyetambua kuwa kuna wengine wanaoweza kulimudu jambo kuliko yeye huambiwa methali gani? (alama 1)

……………………………..

(u) Bainisha kiima na chagizo katika séntensi ifuatayo. (alama 1)

Mwenyewe alikipenda kwa dhati.

……………………………..

(v) Tunatumia kihisishi “makiwa” tunapotaka kumtuliza aliyefiwa, na …………………………..tunapotaka mtu atupishe. (alama 1)

(W) Tunga sentcnsi ya masharti inayoonyesha kwamba tendo lilifanikiwa kwa sababu ya kufanikiwa kwa tendo lingine. (alama 1)

……………………………..

(x) Andika nahau inayojumuisha ujumbe ufuatao: (alama 1) kumzuia mtu kupata kitu japo huna haja nacho

……………………………..

(y) Shumbi ni kwa udongo,…………….kwa chumvi, na ……………..kwa mtama.(alama 1)

4. ISIMUJAMII: (Alama 10)

Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali.

Mtu I: Wcwe njoo hapa! (Kwa sauti kubwa.) Fanya upesi!

Mtu II: (Anakimbia mbio.) Naja Sir.

Mtu I: (Anamtazama.) Unajifanya mwerevu?

Mtu H: Hapana Sir…eh…afande.

Mtu I: Jina?

Mtu II: Samwel Kibao

Mtu I: (Huku anaandika.) Lete kitambulisho.

Mtu H: Sina hapa Sir.

Mtu I: Huna kitambulisho? Utafanyiwa booking vipi?

Mtu II: Naomba…

Mtu I: Naomba! Naomba! Unaomba nini? Wazururaji kama nyinyi tunawajua. Mnajidai hamjui kuna curfew. Mnajiponza wenyewe na kuwahasiri wenzenu. Kisha, “Serikali saidia”. Usiniharibie muda wangu. (Akiashiria.) Ingia ndani! Utakuwa mgeni wetu leo. Tutakukirimu chakula na chumba. (Anamsukuma ndani.)

(a) Bainisha sajili ya makala haya. (alama 2)

…………………

(b) Eleza sifa nane za sajili hii kwa kurejelea makala haya. (alama 8)

…………………

(Visited 401 times, 1 visits today)
Share this:

Written by