KCSE Past Papers 2014 Kiswahili Paper 3 (102/3)

Karatasi ya 3

FASIHI

SEHEMU A: RIWAYA

1. Lazima

K. Walibora: Kidagaa Kimemwozea

“Labda ni suala la mzigo wa mwenzio kanda la usufi.” “….Sijui ‘mwenyewe’ aliyetajwa ni nani. Lakini sharti awe mtu ambaye kwake msiba kwa wengine kwake arusi.”

(a) Fafanua muktadha wa dondoo hili. (alama 4)

(b) Bainisha‘ tamathali mbili za usemi zinazojitokeza katika dondoo hili. (alama 2)

(c) Jadili jinsi ambavyo hali ya, ‘msiba kwa wengine kwake arusi’, inavyojitokeza katika Kidagaa Kimemwozea. (alama 14)

SEHEMU B: TAMTHILIA

T. Arege: Mstahiki Meya

Jibu swali la 2 au la 3.

2. “Waache wagome, Watajiponza Wenyewe.”

(a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama. 4)

(b) Dondoo hili linadokeza mojawapo ya mbinu hasi za ulawala. Iandike. (alama 2)

(c) Fafanua mbinu nyingine saba hasi za utawala zilizotumiwa katika tamthilia hii. (alama 14)

3 “Ngoja ngoja huumiza matumbo.” Thibitisha kauli hii kwa kurejelea tamthilia ya Mstahiki Meya. (alama 20)

SEHEMU C: HADITHI FUPI K. Walibora na S. A. Mohamed: Damu Nyeusi na Hadithi Nyingine Jibu swali la 4 au la 5.

“Maskini, Babu Yangu!” (K. Walibora)

4 (a) “Salalaa! Mbona wasirudi kwao waishi maisha ya maana kidogo.”

(i) Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)

(ii) Fafanua umuhimu wa mzungumzaji katika hadithi hii. (alama 8)

(b) “Shangazi wakumbuke watoto. Waonee huruma!”

(i) Andika tamathali ya usemi inayojitokeza katika kauli hii kwa kurejelea hadithi:

“Samaki wa Nchi za Joto”. (alama 2)

(11) Bainisha matumizi mengine matatu ya tamathali hii ya usemi katika hadithi hii. (alama 6)

“Maeko” (Mohamed Khelef Ghassany)

5. “Hutaki kuwaeleza, kuwa meridhika, oo ‘ridhika’

Eleza kinyume kinachojitokeza katika maneno yaliyopigiwa mstari kwa kurejelea hadithi hii. (alama 20)

SEHEMU D: USHAIRI

Jibu swali la 6 au la 7.

Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.

Amiri A.S. Andanenga: Sauti ya Kiza

1. Ngakua na mato, ya kuonea
Ngalisana kito, cha kuchezea
Kilicho kizito, cha kuelea
Kikamuenea, akivae.

2. Makusudi yangu, ngaliandaa
Ngafinyanga chungu, cha mduwaa
Ngatia vitangu, vinavong’aa
Ili ziwe taa, kwa apikae.

3. Mkungu wa tano, wa mduwara
Ulo bora mno, kisha imara
Ulo na maono, kuwa ni dira
Kwenye barabara, itindiae.

4. Ngaomba baraka, kwake Rabana
Punje za nafaka, kila aipa
Chunguni kuweka, kwa kulingana
Hajaangu suna, yule alae.

5. Ngafanya bidii, kwenda mwituni
Sio kutalii kukata kuni
Ya miti mitii, huko jikoni
Isio na kani, ni iwakae.

6. Kwa yangu rnabega, nikathubutu
Ngabeba mafiga, yalo matatu
Bila hata Woga, kwenye misitu
Simba tembo chatu, sinitishie.

7. Miti yenye pindi, na jema umbo
Ngajenga ulindi, mwema wimbombo
Fundi aso fundi, penye kiwambo
Moyo wenye tambo, agekechae.

8. Singaajiri, ngachimba mimi
Kisima kizuri, cha chcmchemi
Maji ya fahari, ya uzizimi
Jua la ukami, siyaishae.

9. Tamati nafunga, kwa kuishia
Mato ndo malenga, kanikimbia
Nahofu kutunga, mabeti mia
Asije chukia, ayasomae.

(a) Eleza ujumbe Wa shairi hili. (alama 2)

(b) Kwa kurejelea ubeti wa pili, eleza umuhimu wa aina mbili za uhuru wa kishairi alioutumia mshairi.(alama 4)

(c) Andika ubeti wa saba kwa lugha ya nathari. (alama 4)

(d) Eleza toni ya shairi hili. (alama 2)

(e) Fafanua aina tatu za urudiaji zilizotumiwa katika shairi hili. (alama 6)

(f) Bainisha nafsineni katika shairi hili. (alama 2)

7. Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.

T. Arege: Watafuta Riziki

1. Watafuta riziki, watokwa jasho vijijini
Wakulima shakiki, wakuza chai na mibuni
Vyakula wahakiki, visipungue vinyuani.

2. Watafina riziki, wahangaikao mijini
Kutwa kile na hiki; kamawatanga na mipini
Japo hawasikiki, hawakosi kujiarnini.

3. Watafuta riziki,wazalendo Wa nchi hii
Kaniwc hawajidhiki, tamaa za moyo kutii
Bali huafiki, kupingfiha na ulaghai.

4. Watafuta riziki, pate ambalo la halali
Ndoto haizimiki, ya kesho kuwa njema hali
Wiki baada wiki, la haramu jasho hawali.

(a) Fafanua sifa tano za Watu wanaozungumziwa katika shairi hili. (alama 5)

(b) Bainisha umuhimu wa tamathali tatu za usemi zilizotumiwa katika shairi hili. (alama 6)

(c) Eleza kwa kutoa mifano, mbinu tatu ambazo mshaifi ametumia kutosheleza mahitaji ya kiarudhi. (alama 6)

(d) Ainisha shairi hili kwa kuzingatia vigezo vifuatavyo (alama 3)

(i) idadi ya mishororo katika beti

(ii) mpangilio wa vina

(iii) mpangilio wa maneno

SEHEMU E: FASIHI SIMULIZI

8 (a) Soma hadithi ifuatayo kisha ujibu maswali.

Basi Mulungu akamtuma kinyonga duniani kumpasha binadamu ujumbe ufuatao: “Maisha yako hayatakuwa na mwisho, hata ukifa utafufuka.”

Kinyonga akaondoka kama mshenga apelekaye posa. Akatambaa polepole, moyoni amejawa na hofu ya kuiharibu ardhi ya wenyenwe. Hata alipowafikia binadamu machweo ya siku ya saba baada ya kupashwa ujumbe, alimpata mnana keshaubatilisha ujumbe huo; ameisha kumwambia binadamu kuwa akifa atatokomea kama mizizi ya msubili. Huo ukawa ndio mwanzo Wa mauti.

(i) Andika aina ya hadithi hii. (alama 2)

(ii)Fafanua umuhimu wa aina hii ya hadithi katika jamii. (alama 10)

(b) Eleza majukumu manne ya fomyula ya kumalizia katika ngano. (alama 8)

 

(Visited 271 times, 1 visits today)
Share this:

Written by