KCSE Past Papers 2013 Kiswahili Paper 3 (102/3)

4.23 Kiswahili Paper 3 (102/3)

SEHEMU A : FASIHI SIMULIZI

1 Lazima

(a) Huku ukitoa mfano, eleza maana ya vitanza ndimi. (alama. 2)

(b) Fafanua majukumu sita ya vitanza ndimi katika jamii. (alama 6)

(c) Eleza mbinu sita unazoweza kutumia kalika kukusanya na kuhifadhi habari kuhusu vitanza ndimi. (alama 12)

SEHEMU B: RIWAYA

Said A. Mohamed: Utengano

Jibu swali la 2 au la 3.

2 “Walifanya kazi, walimenyeka,

Lakini walilala na njaa

Njaa, ndiyo ilikuwa misumeno

Iliyokeketa matumbo yao, …”

(a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)

(b) Bainisha tamathali mbili za usemi zinazojitokeza katika dondoo hili. (alama 4)

(c) Kwa kurejelea riwaya, onyesha jinsi wanyonge walivyomenyeka. (alama 12)

3 Jadili uhusiano uliopo kati ya wahusika na maudhui kwa kurejelea wahusika wafuatao:

(a) Shoka (alama 10)

(b) Kazija (alama 10)

SEHEMU C: TAMTHILIA

T. Arege: Mstahiki Meya Jibu swali la 4 au Ia 5.

4 Jadili mchango wa Wanacheneo katika kuivunja jamii yao. (alama 20)

5 “Ndiyo hivyo bwana. Elimu yetu hapa ni ya kawaida mno. Haina kubwa la kumfaa mtoto mwenye mzazi anayeona mbali.“

(a) Eleza muktadha wa maneno haya. (alama 4)

(b) Bainisha tamathali ya usemi inayojitokeza katika dondoo hili ukirejelea msemaji wa kauli hii. (alama 2)

(c) Kwa kurejclea tamthilia, fafanua mifano mingine saba ya matumizi ya tamathali uliyotaja katika (b) hapo juu. (alama 14)

SEHEMU D: USHAIRI

Jibu swali la 6 au la 7.

Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.

Sinongi aushi yangu, hii leo, kwa ukungu wa ujana,

Nikaiga rika langu, kwa vileo na mbio za wasichana,

Kiwa ni riziki yangu, mapokeo, kuoa na kuona,

Ni wakati utanena.

Nashukuru kwa ugumba, wenye ndimi, wanipagazao nao,

Wapitao wakiimba, eti mimi, ningapenda hali zao,

Haupandiki mgomba, wana nyemi, fisadi wa hadhi zao,

Eti ni kwa raha zao.

Ni lipi lenye kukera, kwa Muumbi, marufuku kwenye misa,

Ni mtu kuwa hawara, wa vitimbi, ama alozawa tasa?

Ugumba na ukapera, sio dhambi, wala haujawa kosa,

Waama sina makosa.

Bora tungeni vitabu, magazeti, mutangaze kwa rediyo,

Muwaite watribu, kina Siti, watuzwa ilimu hiyo,

Na zaidi muhutubu, kwa umati, muwambe ambayo siyo,

Kwalo sichafuki moyo.

Hidhuru yote ni bum, sio kitu, kudhiki asodhikika,

Siwi nikaona ghere, lailatu, nyota njema itafika,

Kwa shangwe na njerejere kila mm, mdomo utafumuka,

Akiri amejibika.

(Mwalaa M. Nyanje)

(a) Eleza jambo ambalo mzungumzaji (nafsineni) katika shairi hili anasingiziwa. (alama 2)

(b) Fafanua mambo matano ambayo mzungumzaji (nafsineni) anapinga katika shairi hili. (alama 5)

(c) Eleza umuhimu wa viishio vya beti za shairi hili. (alama 2)

(d) Andika ubeti wa tatu kwa lugha ya nathari. (alama 4)

(e) Eleza muundo wa shairi hili. (alama 5)

(O Bainisha matumizi mawili ya tasfida katika shairi hili. (alama 2)

Soma shairi lifuatalo kisha ujibu aswali.

Huno wakati mufti, vijana nawausia,
Msije juta laiti, mkamba sikuwambia,
Si hayati si mamati, vijana hino dunia,
Uonapo vyang’aria, tahadhari vitakula.

Japo aula kushufu, na machoni vyavutia,
Dunia wana dhaifu, yaugua nisikia.
Vijana nawasarifu, falau mkisikia,
Ukiona vyang’aria, tahadhari vitakula.

Jepusheni na zinaa, mlale penye sharia,
Msije andama baa, makaa kujipalia,
Jepusheni na zinaa, madhara kukadiria,
Uonapo vyang’aria, tahadhari vitakula.

Ngawa waone wazuri, nadhifu kukuvalia,
Wajimwaie uturi, na mapoda kumichia,
Si mlango nyumba nzuri, ngia ndani shuhudia,
Uonapo vyang’aria, tahadhari vitakula.

Wawapi leo madume, anasa walopapia?
Wamepita ja umeme, leo yao sitoria,
Shime enyi wana shime, bora kumcha Jalia,
Uonapo vyang’aria_ tahadhari vitakula.

Nambie faida gani, nambie ipi fidia?
Upatayo hatimani, waja wakikufukia,
Ila kufa kama nyani, kasoro yako mkia,
Uonapo vyang’aria, tahadhari vitakula.

Kikiki ikaze kamba, u kijana vumilia,
Ujifanyc kama kwamba, u jiwe huna hisia,
Wakwambe watalokwamba, kwa lolote vumilia,
Uonapo vyang’aria, tahadhari vitakula.

Vyatiririka liriri, vina vyanikubalia,
Alo bora mshairi, pa tamu humalizia,
Nahitimisha shairi, dua ninawapigia,
Uonapo vyang’aria, tahadhari vitakula.

9. Ewe Mola mtukuka, si shaka wanisikia,
Wakingie wanarika. na anasa za dunia,
Amina wangu Rabuka, dua yangu naishia,
Uonapo vyang‘aria, tahadhari vitakula.

(Mwalaa M. Nyanje)

(a) Eleza ujumbe wa shairi hili. (alama 4)

(b) Fafanua kwa kutoa mifano, mbinu nne alizotumia mshairi kutosheleza mahitaji ya kiarudhi katika shairi hili. (alama 8)

(c) Nafsineni (mzungumzaji) katika shairi hili inasema na pande mbili. Zieleze pande hizo. (alama 2)

(d) Eleza umuhimu wa maswali ya balagha katika shairi hili. (alama 3)

(e) Bainisha toni ya shairi hili. (alama 3)

SEHEMU E: HADITI-II FUPI

K Walibora na S. A. Mohamed: Damu Nyeusi na Hadirhi Nyingine

“Kikaza” (Robert Oduori)

‘Wakaacha chungu kinatokota – bila kuivisha chakula‘. Kwa hakika walijibu, “Ndio mtindo, na sisi rulifuata mitindo.”

(a) Fafanua muktadha wa dondoo hili. (alama 4)

(b) Onyesha jinsi Wanatekedc wanavyofuata mitindo na kuacha chungu kinatokota bila kuivisha chakula. (alama 16)

 

(Visited 479 times, 1 visits today)
Share this:

Written by