KCSE Past Papers 2013 Kiswahili Paper 2 (102/2)

4.2.2 Kiswahili Paper 2 (102/2)

UFAHAMU: (Alama 15)

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali. Gari lake kuukuu lilikuwa linapambana na barabara yenye mashimo yaliyoshiba na kutapika maji ya mvua ambayo sasa ilikuwa inaanza kupusa.

Japo daima alipambana na usukani kunako mashimo haya yaliyotosha kuitwa magenge, alishukuru kwa hali hii.

Vipi angeweza kulidhibiti gari lake hili kwenye barabara iliyosakafiwa nayo ikahitimu? Magurudumu haya yaliyong’ara kama upara wa shaibu aliyekula chumvi hadi ikamwogopa yangetii uelekezi wake?

Mara ngapi gari hili limetaka kumwasi barabarani?

Haya yalikuwa baadhi ya maswali yaliyompitikia akilini.

Hakujitakilifu kutaka kuyapa mji maana mara ile mawazo yake yalitekwa na kubwagwa katika nchi ya mbali – nchi ambayo sasa aliiona kama sinema akilini mwake.

Alipofika nyumbani aliliegesha gari lake na kufululiza ndani.

Siku mbili zilikuwa zimepita akiwa pale kazini.

Madaktari kama yeye hawakuwa wengi.

Alikuwa miongoni mwa madaktari wenye ujuzi katika hospitali hii ya kitaifa.

Wenzake wengi walikuwa wamehamia ughaibuni walikokwenda kutafuta maisha.

Mshahara wao wa mkia wa mbuzi uliwasukuma na kuwatema nje ya nchi yao.

Wengi wa waliohamia ng’ambo waliona vigumu kubaki katika ajira ambayo kivuno chake kilishindwa kumvusha mtu hata nusu ya kwanza ya mwezi.

Malalamishi ya kulilia ujira wa heshima yaligonga kwenye masikio yaliyotiwa zege.

Na kweli wanavyosema, mwenye macho haambiwi tazama.

Basi walitazama hapa na pale wakaona penye mianya ya matumaini, nao wakaiandama.

Hadi leo hii hamna la mno lililofanyika.

Ndiyo maana Daktari Tabibu anarudi nyumbani tangu kuingia kazini hiyo juzi alfajixi.

Hafanyi kwa kuwa katosheka, maana pia yeyc ana dukuduku.

Ana shaka ya mustakabali wake ikiwa mazingira ni haya ya kumsoza, maana umri nao unazidi kumla.

Japo anatia na kutoa, mizani ya hcsabu yake imeasi ulinganifu. Daktari Tabibu waama ni mfungwa. Ametekwa na kuzuiwa katika kupenda na kuchukia mambo.

Ni kama mti uliodumaa.

Anatamani barabara nzuri za lami.

Anatamani mshahara wa kumwezesha kukidhi mahitaji yake na kutimiza majukumu yake ya kimsingi.

Jana amesema na rafiki yake aliye ng’ambo kwa simu ambayo sasa imetulia mkabala naye.

Ingawa mwenzake huyu alikuwa mchangamfu na kumdokolea hali ya maisha ya kuridhisha kule ugenini kama vile wanataaluma kuenziwa, yapo vilevile yaliyomtia unyonge moyoni.

Upweke ndio uliomtia fukuto kuu.

Licha ya hela zote hizo za kupigiwa mfano, watu hawana muda wa kutembeleana na kujuliana hali au hata kukutana tu mkahawani wakashiriki mlo.

Eti ni kila mtu na hamsini zake. Halafu ipo changamoto ya hali ya hewa.

Baridi ya ng‘amb0 haifanyi mzaha katika kumtafuna mtu.

Ni hali tofauti na ile aliyoizoea.

 

Daktari Tabibu alizitia kauli za rafiki yake kwenye mizani ya moyo wake.

Akawaza ikiwa kweli si bora kulemazwa na mzizimo ugenini badala ya kuishi katika kinamasi cha kuumbuliwa nyumbani.

Kisha punde lilimjia wazo la marehemu nyanyake na wengine kama yeye waliofadhili masomo yake kupilia kwa serikali na njia ya kodi.

Je, si usaliti huu? Vipi aikimbie nchi kabla ya kuihudumia ilhali imemjenga hadi kuwa daktari?

Na je, wafanyakazi wake wa nyumbani watakwenda wapi?Atawaambiaje kuwa sasa hahitaji huduma zao kwa kuwa anakimbia nchi yaks?

Mawazo yake yalikatizwa na simu iliyolia na kumshtua.

Alipoitazama aliiona imeng’ara kwa mwangaza ulioweka wazi jina la mpigaji.

Alifahamu kuwa leo hii tena dharura nyingine ilikuwa inamwalika hospitalini.

Mwili wake ulimsaliti ingawa moyo wake ulimkumbusha kuwa lisilo budi hulendwa.

Hapo ndipo alipoiinua ile simu layari kusema na mwenzake upande wa pili.

“Haloo!” Sauti nyororo kutoka upande wa pili iliita.

“Haloo!”

“Naam! Dharura nyingine lena daklari. Unaombwa kuokoa maisha mengine tena!”

“Haya. Ila mwanzo nitahilaji kujimwagia maji”, na pale pale akaikata ile simu.

Dakmri Tabibu aliingia hamamuni huku kajifunga taulo kiunoni tayari kuoga.A1iyafungulia maji

lakini ule mfereji uligoma kutapika maji. Ulikuwa umekauka kabisa. Daktali Tabibu aliduwaa pale. Aliufunga ule mfereji kabla ya kuiaga bafu.

(a) Eleza sababu nne zinazowafanya walaalamu kuhamia nchi za nje. (alama 4)

(b) “Hakuna masika yasiyokuwa na mbu.” Thibitisha kauli hii kwa kurejelea hali ya waliohamia ng’amb0. (alama 3)

(c) Fafanua athari tatu zinazoikumba nchi ya msimulizi kutokana na uhamiaji ng’ambo wa wataalamu. (alama 3)

(d) Eleza mchango wa teknolojia kwa kurejelea kifungu. (alama 3)

(e) Eleza maana za msamiati ufualao kulingana na taarifa. (alama 2)

(i) kuyapa mji (ii) fukuto UFUPISHO: (Alama 15)

Soma kifungu kifimtacho kisha ujibu maswali.

Wakenya walipoipifisha katiba mpya waliidhinisha mfumo wa ugatuzi.

Katika mfumo huu, mamlaka ya serikali kuu katika uongozi, usimamizi na utumiaji wa rasilimali za nchi hupunguzwa.

Kiasi fulani cha mamlaka hutwaliwa na maeneo ya ugatuzi.

Suala hili halikuzingatiwa katika katiba ya awali ambapo mamlaka yote yalikuwa mikononi mwa serikali kuu.

Kutokana na upana na wingi wa maeneo nchini, iliiwia vigumu serikali kuu kuhakikisha kwamba kulikuwa na usawa wa kimaendeleo katika sehemu zote nchini.

Kwa mujibu wa katiba mpya, scrikali kuu haina budi kuyasaidia maeneo yote ya ugatuzi ili yaweze kujinyanyua kiuchumi na kuboresha hali za maisha za wakazi wake.

Vilevile ni jukumu la kila eneo la ugatuzi kuweka mikakati madhubuti ili kuchunguza na kubainisha rasilimali zote katika maeneo husika.

Hili litasaidia kuvumbua rasilimali ambazo zinaweza kuchangia katika ustawishaji wa maeneo haya.

Maeneo haya pia yanatakiwa kutafuta mbinu zitakazofanikisha uzalishaji na utumiaji wa rasilimali hizi kwa njia endelevu.

Mojawapo ya mbinu hizi ni uongezaji thamani katika rasilimali yoyote inayozalishwa kwenye eneo mahususi.

Maeneo mengi ya ugatuzi nchini humu yanategemea kilimo cha ufugaji kama mhimili wa uchumi.

Licha ya kuwa nguzo, kilimo hiki hakijawahi kupigiwa darubini vizuri kwa lengo la kukiimarisha ili kiwanufaishe wenyeji kikamilifu.

Aghalabu wafugaji wengi huandama mbinu zajadi za ufugaji ambazo haziwahakikishii ongezcko la mapato.

Isitoshe, wafugaji hawa wanakabiliwa na tatizo katika soko la mifugo ambapo wengi hupunjwa na matapeli.

Pamoja na haya, baadhi ya wakazi huuza mifugo nje ya nchi wakiwa wazimawazima bila kuwazia matokeo ya kitendo hiki.<

Si ajabu kuwaona ng’ombc, ngamia, mbuzi na kondoo wakipakiwa kwenye malori na kusafirishwa nje ya nchi.

Ukweli ni kwamba jambo hili ni hatari sana, si kwa uchumi wa maeneo husika tu, bali pia kwa Kenya kwa jumla.

Hii ni kwa kuwa walionunua mifugo wazimawazima wanaweza kuhiari kutowachinja na badala yakc kuwatumia kama mbegu za kuzalisha mifugo wao.

Hapa pana hatari ya rnaeneo haya kupoteza wateja kwani baada ya muda huenda wanaonunua mifugo wakajitosheleza na kukosa kuja kununua mifugo wengine.

hali ikiwa hivyo, maeneo yaliyotegemea soko hili huenda yakalipoteza taratibu, na bila shaka kupoteza natija inayotokana na soko lenyewe.

Ili kudhibiti hali hii, itakuwa bora ikiwa viwanda vya kuchinjia mifugo na kupakia nyama vitajengwa katika maeneo haya ya ugatuzi.

Hili litawawezesha wakazi kuuza nyama badala ya kuuza mifugo wazimawazima.

Fauka ya haya, maeneo haya yatajikinga dhidi ya kupoteza bidhaa zinazotokana na mifugo.

Hizi ni kama vile ngozi, kwato na pembe ambazo bila shaka zina natija kuu.

Ngozi kwa mfano, ni bidhaa muhimu sana katika sekta ya utengenezaji wa mavazi na mifuko.

Viwanda vinavyotumia ngozi kama malighafi vikijengwa katika maeneo haya, wakazi wake watanufaika si haba.

Mathalani, viwanda vya kutengenezea viatu, mishipi, mifuko na nguo vikianzishwa, wawekezaji watalazimika kuanzisha viwanda vingine vitegemezi.

Kadhalika, ni dhahiri kwamba bidhaa zinazotokana na ngozi huhitaji kutiwa nakshi.

Kuanzishwa kwa viwanda hivi basi kutazua haja ya kuanzishwa kwa viwanda vya kutengenezea rangi, pamoja na maduka ya kuuza bidhaa yenyewe.

Isitoshe, gundi ya kugandisha bidhaa hizi itahitajika, hivyo kusababisha haja ya kuanzishwa kwa kiwanda cha gundi.

Matokeo ya shughuli hizi zote ni kuzalishwa kwa nafasi anuwai za kazi kwa wakazi.

Hili litakuwa na matokeo zaidi chanya, hususan kwa vijana.

Badala ya kushiriki ulevi na burudani zinazowahatarisha, wataweza kujitafutia riziki katika viwanda hivi.

Juu ya hayo, mfumo wa ugatuzi utayawczesha maeneo husika kuongezea thamani utoaji wa huduma za kijamii na kiutawala kulingana na mahitaji ya maeneo haya.

Ni muhimu hata hivyo kuzingatia kwamba kila cneo la ugatuzi lina upekee wake, navyo vipaumbele hutofautiana kulingana na maeneo.

Kuna yale ambayo yatasisitiza usalama, mengine ujenzi na uimarishaji wa miundomsingi kama vile barabara, vituo vya afya na hata taasisi za elimu.

La muhimu ni wakazi wa maeneo husika kubainisha ni lipi litatekelezwa kwanza.

Kinga na kinga ndipo moto uwakapo.

Kufanikiwa kwa mfumo wa ugatuzi kutategemea juhudi za kila mkazi wa eneo husika.

Ni muhimu kila mkazi kujiona kuwa mmiliki wa eneo zima la ugatuzi na kuwajibika katika kuliendeleza kwa hali na mali.

Uwajibikaji huu unajumuisha uteuzi wa viongozi wenyc muono mzuri na ambao watawawezcsha kuyafikia malengo yao ya kimaendeleo.

Hakika, mustakabali na uwepo wa eneo la ugatuzi utakuwa zao la maamuzi ya wanaeneo.

Vilevile ufanisi wa maeneo ya ugatuzi utakuwa msingi wa ufanisi wa taifa kwa jumla.

(a) Fupisha ujumbe wa aya tatu za mwanzo kwa maneno 85-90.

(alama 8, 1 ya mtiririko)

Matayarisho:

Nakala safi:

(b) Kwa kutumia mancno 75-80, bainisha masuala ambayo mwandishi anaibua katika aya tatu za mwisho. (alama 7, 1 ya mtirin’ko)

MATUMIZI YA LUGHA: (Alama 40)

(a) (i) Eleza maana ya sauti mwambatano. (alama 2)

(ii) Andika sauti mwambatano inayotamkiwa kwenye ufizi. (alama 1)

(b) Andika sentensi ifuatayo upya ukibadilisha neno lililopigiwa mstari kuwa kielezi. Komuameshona nguo gum na kuiuza sokoni. (alama 1)

(c) Tunga sentensi mojamoja kubainisha: (alama 4)

(i) kihusishi cha wakati

(ii) kivumishi cha pekee chenye maana, “bila kubagua”.

(d) Andika sentensi ifuatayo katika hali yakinishi.

Askari wasipopiga doria wala kushirikiana na raia hawatakuwa wamctuhakikishia usalama. (alama 2)

(e) Bainisha mofimu katika neno: atamnywea (alama 3)

(f) Andika sentensi ifuatayo katika hali ya udogo: Madebe hayo yatasafirishwa pamoja na nyundo hizi. (alama 2)

(g) Ainisha vishazi katika sentensi ifuatayo: Ingawa mshahara wake si mkubwa anaikimu familia yake. (alama 2)

(h) Tunga sentensi tatu kuonycsha matumizi matatu tofauti ya kiambishi ‘li’. (alama 3)

(i) (i) Eleza maana ya sentensi ya masharti. (alama 1)

(ii) Tunga sentensi ya masharti. (alama 2)

(j) Tumia kiwakilishi cha ‘a’ unganifu katika sentensi kuonyesha

(i) umilikaji (alama 2)

(ii) nafasi katika orodha au nafasi katika kundi (alama 2)

(k) Tunga sentensi yenye kikundi tenzi chenyc muundo ufuatao

Kitenzi kisaidizi, kitenzi kikuu, nomino (alama 2)

(1) Tunga sentcnsi mbili kuonyesha matumizi mawili tofauli ya kistari kirefu. (alama 2)

(iii) Unganisha sentensi zifuatazo kuwa sentensi moja bila kurudia kitenzi.

Osore amempigia Ngungui simu. Ngungui amempigia Osore simu.

(n) Andika upya scntensi ifuatayo ukibadilisha vitenzi vilivyomo kuwa nomino: Mayaka anapotumbuiza huchekesha sana.

(0) Andika maana tatu za nenoz kanda.

(p) Andika visawe viwili vya nahau: enda kombo.

ISIMUJAMII: (Alama 10)

Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali.

Haya ng‘ara Ng’ara leo! Nguo motomoto. Ng’ara leo kwa bei rahisi. Hamsini hamsini shati. Kuona ni bure. Bure kwa bure. Shika mwenyewe ujionee. Bei nafuu. Bei ya starehe. Haya haya. Usikose mwanangu! Hamsa! Fifiy! Hamsa! Fifiy! Hamsa na nyingine.

(a) Bainisha sajili ya mazungumzo haya.

(b) Eleza sifa nane za sajili hii kwa kurejelea kifungu hiki.

(Visited 1,078 times, 2 visits today)
Share this:

Written by