KCSE Past Papers 2019 Kiswahili Karatasi ya 2 (102/2)

Majibu

1. UFAHAMU

(a) (i) Walikuwa hawaujui.

( ) Watu wengi walifariki. 2 x 1 = 2

(b) Madhara ya kemikali ya mbolea

(i) Hudhuru afya za watu/husababisha magonjwa/ husababisha kansa/saratani

(ii) Huwadhuru wanyama/ mifugo

(iii) Hutia sumu kwenye mimea.

(iv) Huchafua visima na mito.

(v) Husababisha vifo vya watu na mifugo. 4 x 1 = 4

(c) Mambo yanayochochea teknolojia mpya kubuniwa:

(İ) Kupungua kwa mashamba/ ardhi inazidi kujibana

(ii) Kuzorota kwa rutuba na kupunguza uzalishaji/ vipando hurudiwa.

(iii) Ongezeko la watu watakao lishe/ wingi wa watu.

(iv) Kutoipa ardhi nafasi ya kupumua na kujirutubisha. 3 x 1 = 3

(d) Wazee wana hadhi kwa sababu.

(i) Jamii inataka kujua wanachokifikiria kuhusu janga/ jamii inatambua mchango wao katika usuluhishaji wa changamoto..

(ii) Mzee mmoja anapewa nafasi kuhitimisha kikao. 2 a 1 = 2

(e) ‘Nywele za koto inarejelea wenye mawazo finyu au ya kubabaisha na ‘nywele za singa’ inarejelea wenye mawazo ya kina/mapevu. / Kila mtu ana uelewa wake; Viwango vya uelewa havifanani. 1 x 2 = 2

(f) Anwani Mwafaka kwa kifungu.

(i) Madhara ya mbolea

(ii) Hofu kijijini

(iiİ) Janga la saratani/ Saratani

(iv) Madhara ya teknolojia 1 x 2 = 2

2. UFUPISHO

(a)Demokrasia ni mfumo wa utawala wa kuwachagua wawakilishi moja kwa moja. Demokrasia ni utawala wa umma.

(iii) Umma huhakikishiwa haki fulani za kimsingi ambazo haziwezi kukiukwa. (iv) Haki hizo hutambuliwa na kudhibitiwa kimataifa.

(v) Demokrasia hushirikisha uchaguzi ulio huru na wenye haki.

(vi) Huwezesha kuhusika kikamilifu kwa umma katika siasa na masuala mengine ya kijamii.

(vii) Husisitiza kulindwa kwa haki za kibinadamu na za wananchi.

(viii) Huwa ni utawala wenye usawa wa kisheria/ ni utawala ambao huongozwa na sheria.

(ix) Kila nchi hufasiri dhana ya demokrasia kwa namna inayoifaa yenyewe.

(x) Kuna demokrasia ya moja kwa moja: raia hupigia sera fulani kura bila kupitia kwa wajumbe.

(xi) Kuna demokrasia ya uwakilishi — demokrasia ya uwakilishi ya urais, demokrasia ya uwakilishi ya bunge na demokrasia ya uwakilishi ya kimabavu.

(b) (i) Demokrasia hulinda maslahi ya raia wote.

(ii) Hugatua mamlaka na kuzuia kundi dogo kudumu mamlakani.

(iii) Hukuza usawa kwa wote kwa kuwa sheria haibagui.

(iv) Wanaochaguliwa huweka sera mwafaka.

(v) Kuhusishwa kwa raia hupunguza uwezekano wa kutokea mapinduzi.

(vi) Hukuza mabadiliko kwa kuwa uongozi huwa na kipindi maalumu cha kuhudumu.

(vii) Demokrasia hufunza watu kuhusu siasa hasa wakati wa kampeni.

(viii) Watawala huwa na tahadhari na kuwajibika.

(ix) Demokrasia ina dhima muhimu kwa nchi hivyo inafaa kuendelezwa.

3. MATUMIZI YA LUGHA (Alama 40)

(a) (i) Ondoka, ongoka, anguka, atwaza

(ii) Ndoa, ngao, mbao, twaa

(b) (i) a – nafsi ya tatu/mtenda/ ngeli/ kiambishi cha umoja/ kiambishi cha kiima sem- mzizi.

a – kauli tenda/ kiishio/ kimalizio vyo – kirejeshi/namna

(ii) mw — umoja angwi — mzizi

(c) Shule – nomino ya jamii/ makundi / ya kawaida ukarimu. nomino dhahania Shirika la Tugawane — nomino ya pekee 3 x 1 = 3

(d) Maseremala walizilainisha mbao hizo ili kutengeneza makasha wawauzie walinzi hao.

(e) (i) Mungla alikuwa wa kwanza katika mbio hizo.

(ii) Kuli yeyote anaweza kupakia mizigo hiyo chomboni.

(f) Jitu hilo lilifuata jia/ jijia lililolielekeza jijini.

(g) (i) (i)Mhandisi alikarabatia mtambo kiwandani.

Au (ii) Mtambo ulikarabatiwa kiwandani na mhandisi.

Au (iii) Kiwandani kulikarabatiwa /mlikarabatiwa/palikarabatiwa mtambo na mhandisi. Au Mtambo uliokuwa/ ambao ulikuwa kiwandani ulikarabatiwa na mhandisi.

(ii) Kembo alishona fulana hiyo tena. Au Kembo alishona fulana hiyo mara nyingi/maradufu/daima/maranyingine.

(h) (i) “Tutatoa nyongeza ya mshahara mwaka ujao,” Mkurugenzi akasema. Au (ii) “Watatoa nyongeza ya mshahara mwaka ujao,” Mkurugenzi akasema.

Au (iii) “Mtatoa nyongeza ya mshahara mwaka ujao,” Mkurugenzi akasema.

Au (iv) Mkurugenzi: Tutatoa nyongeza ya mshahara mwaka ujao.

(i) (i) Ni wazi kwamba gharama ya maisha ilikuwa imepanda baada ya kupanda kwa bei ya mafuta. Au

(ii) Ni wazi kwamba gharama ya maisha ilikuwa imepanda kutokana na kupanda kwa bei ya mafuta. Au

(iii) Ni wazi kwamba gharama ya maisha ingekuwa imepanda iwapo bei ya mafuta ingekuwa imepanda. Au

(iv) Ni wazi kwamba gharama ya maisha ilikuwa imepanda bei ya mafuta ilipopanda.

(j) Badi huwa anapitia (hupitia) hapa, huenda ukampata/ umpate/utampata.

(k) aminifu — saliti 1/ 0 vivu — kakamavu/ shupavu

(i) (i) sukari I-I, I-ZI( aina nyingi)

(ii) teo U — ZI

Mvua imepusa na watu wameanza kundoka. KN (N) KT(T) U

KN(N) KT(T+S T)

Au S /+ U+S2

Si KN+KT

N

N Mvua

KT T

T imepusa

U na

S2 KN+KT

N

N watu

KT Ts T

Ts wameanza

T kuondoka

KN (N) KT(T) U+KN(N)+KT(Ts+T)

(n) (i)Vyakula vilivyokuwa na viinilishe muhimu viliandaliwa.

Au (ii) Vyakula vilivyoandaliwa vilikuwa na viinilishe muhimu.

Au (iii) vyakula ambavyo viliandaliwa vilikuwa na vinilishe muhimu. 2

(o) Keto — yambwa tendewa / kitondo watoto hao — yambwa tendwa /kipozi kwa upendo-Chagizo.

(p) (i)Ku-nafsi ya pili umoja Baba anakupenda.

(ii)Mahali/ ngeli ya mahali/ mahali kusikodhihirika — Huku kwao kunapendaza. Kitenzi jina/ ngeli ya kitenzi-jina — kucheza kule kunavutia.

(iii)Wakati uliopita/ wakati uliopita hali ya kukanusha— wageni hawakufika mapema.

(r)hoyee!/ huree!/hario!/ oyee!

(s)jamani!/jama! enyi!/nyungwa!/ aisee! 1/ 0 ukuta — kiambaza/ kizuizi/ kizingiti/ngome/boma

1/ 0 njia — baraste/namna/mbinu/mtindo/ jinsi/ sampuli

(t) dua — ombi

tua — sita, pumzika, tulia, aibu, weka mzigo chini. Tanbihi: Sentensi sharti ibainishe maana hizi.

Mfano:

Msafiri alitua mzigo akapiga magoti na kumpigia Mola dua.

(u) (i)Mti rnkuu ukigwa wana wa ndege huyumba.

Au (ii) Mwana akibebwa hutazama kisogo cha nina.

Au (iii) Samaki huanza kuozea kichwani.

(v) (i) Doto hakula wala kunywa kwa siku kadha.

(ii) Je, utakula wali au sima?

(iii) Anna usome kwa bidii au ufeli mtihani wako.

4 ISIMUJAMII (Alama 10)

(i) Msamiati wa kidini/ matumizi ya msamiati teule wa kidini.

(ii) Lugha ya kuwashawishi kumtii Mungu.

(iii) Kurejelea vifungu vya vitabu vitakatifu.

(iv) Kuchanganya ndimi/ kubadili msimbo.

(v) Lugha inaweza kuwa rasmi au isiyo rasmi.

(vi) Lugha yenye toni kali ya kuonya.

(vii) Kuwasawiri kama viumbe ambao ni wategemezi kwa Mungu.

(viii) Maswali ya balagha ili kuwahusisha zaidi/kuteka hisia zao.

(ix) Lugha ya mafumbo/matumizi ya majazi.

(x) Kurudia vifungu/baadhi ya maneno kama vile ‘Amina’.

(xi) Anaweza kutumia misimu ya vijana iii kujinasibisha nao.

(xii) Matumizi ya ucheshi/ utani kiasi cha haja.

(xiii) Lugha ya unyenyekevu/ upole/ kusihi.

(xiv) Kutumia lugha sahili kulingana na kiwango cha wanafunzi.

(xv) Matumizi ya msamiati wa shuleni.

(Visited 384 times, 1 visits today)
Share this:

Written by