KCSE Past Papers 2018 Kiswahili Paper 2 (102/2)

Majibu

(a) “Malengo yetu ya kuwateua viongozi yamesalitiwa.” Thibitisha kauli hii kwa kurejelea hoja sita kutoka kwenye taarifa. (alama 6)

 

 • Vijana kusoma na kutopata kazi.
 • Waliosoma kupewa kazi za hadhi ya chini huku wasiosoma wakiwa wakubwa. Raia kuteua
 • viongozi wasiofaa kwa sababu ya ufisadi.
 • Raia kutopata huduma walizoahidiwa, kama vile maji ya mabomba.
 • Watoto wa maskini kutopata elimu licha ya kuwepo kwa hazina ya eneo bunge. Nyadhifa za juu kutwaliwa na watu wa nasaba moja/ukabila/unasaba.
 • Viongozi kuwatumia vijana kulangua dawa. Viongozi kuwatunga mimba watoto.
 • Ajira ya watoto.
 • Hazina ya eneo bunge kutowafaidi watoto wanaohitaji zaidi msaada.(b) Eleza mchango wa wanyonge katika hali ya uongozi nchini Tungama. (alama 3)

   

 • Kupoteza nafasi ya kuuwajibisha uongozi kwa kupokea hongo/kuuza kura. Kuwaimbia viongozi nyimbo ili kuwapembeja raia wawapigie kura.
 • Kuamini kwamba wanasiasa wote ni sawa; kukata tamaa ya kuchagua kiongozi tnwadilifu. (iv) Baadhi ya wale waadilifu kutojiunga na siasa — kwa mfano, Angaza. 3 x 1 = 3(c) Bainisha mbinu nne ambazo Bi. Mkesha anatumia kuishawishi hadhira yake. (alama 4)

  Kujinasibisha na wasikilizaji wake ndugu wapenzi, mama mwenzangu. Maswali ya balagha ili kuwachochea/ kuwavutia kwake. Je, mnajua … Kuwasawiri wasikilizaji kama wanaofaa — haya si mageni/anayasawiri mambo kama ya kawaida ili yeye na hadhira yake wayafasiri kwa namna sawa.

  (iv) Kuwaonyesha wasikilizaji wake kuwa ni mwenye mainlaka ya kuleta uthabiti katika uongozi.

  (v) Anajitenga na wanasiasa wengine na (kwa) kudokeza udhaifu wao. hawa hawa viongozi … ahadi ya ‘mwenzetu’…

  (d) (i) Andika kisawe cha, ‘kuwapembeja’ kwa mujibu wa taarifa.

  (i) Kuwapembeja — kuwarai, kuwalaghai.

  (ii) Andika maana ya, ‘amejikosha’ kulingana na taarifa.

  (ii) Amejikosha — amejitoa lawamani.

  2. (i) Majukumu ya kijinsia yalikuwa bayana.

  (ii) Majukumu yalirithlshwa kwa vizazi.

  (iii) Vijana walifunzwa kukabiliana na majukumu.

  (iv) Jamii kuwa na matarajio kuhusu jinsia.

  (v) Mwanaume kutarajiwa kukimu familia.

  (vi) Mama kuwa na jukumu la malezi.

  (vii) Watoto wa kike kutarajiwa kuzilinda familia.

  (viii) Mama kuwa mwalimu.

  (ix) Watoto wa kiume kufunzwa kuwa wa kutegemewa.

   

 • Watoto wa kike walifunzwa kuzilinda jamii zao.
 • Mama ndiye aliyekuwa mwalimu wa kwanza wa watoto wake.
 • Watoto wa kiume walifunzwa umuhimu wa kuwa watu wa kutegemewa. Uchangainano wa jamii umesababisha kubadilika kwa mitazamo.
 • Majukumu yameingiliana. Kwa mfano, wake wanafanya mambo ambayo awali hayakufanywa na jinsia hiyo.
 • Idadi ya wanawake wanaofanya kazi ya ajira imeongezeka.
 • Wanawake kusomea taaluma na nyanja zilizotengewa wanaume awali. Wanaume kufanya kazi zilizotengewa wanawake.
 • Hali ya mwingiliano wa kimajukumu hupalilia mshikamano na kukabiliana na tofauti za kijinsia.
 • Hufidia udhaifu wa wenzao.
 • Mwingiliano wa majukumu unaweza kuathiri vibaya faida iliyotarajiwa, kama vile kutelekezea malezi kwa vljakazi.
 • Baadhi hujisajili kwa kazi ili kushindana na wenzao. Hali hii huzua utengano na kusambaratika kwa ndoa.
 • Kila jambo sharti liwe na mipaka/kuna majukumu yanayostahili kutengewa tu jinsia maalum na mengine jinsia zote/mipaka hii idumishwe.(b)Miambakofi Yatazoleka

  (c) (i) ki — li — nunu — liw — a wa — li — tembe lew — a zi li — jeng — ew — a

  (ii) Mi-kate — (mi} wingi (kate} — mzizi

  Vi-ti Ny-ufa

  (vi} — wingi

  {ti} — mzizi

  {ny} — wingi (ufa} — mzizi

  (d) (İ) Mtu mwaminifu huheshimiwa.

  (Ü) Wao ndio walioibııka washindi.

  (iii) Mchuuzi alinunua kicha cha mboga.

  (iv) Seluwa ni mtiifu kama Maria / Seluwa ni mtiifu kuliko Maria.

  (e) (i) Ugwe — U — ZI.

  (ii) Lîmau — LI — YA

  Vifaa vya kutosha visingalikuwapo moto usingalidhibitiwa. Kama vifaa vya kutosha visingekuwepo moto usingedhibitiwa.

  Kama pasingekuwa na vifaa vya kutosha moto haingedhibitiwa. Vifaa vya kutosha visingekuwepo moto usingedhibitiwa.

  (g) Manahodha waliyakwepa majabali hayo vyoınbo vikafika fuoni salama.

  (h) Kwa mfano: Wanafunzi waliotia bidii masomoni walipata alama nzuri mno. Nomino kishazi kitegemezi kitenzi Nomino kivumishi kielezi

  (i) Barabara nyingi zitakuwa zikisakafiwa. au

  Barabara nyingi zitakuwa zinasakafiwa.

  (j) Wanafunzi wamefurahia kufika kwa wageni. Au

  Wanafunzi ivamefurahi wageni walipofika. Au

  Wanafunzi wamefurahi baada ya wageni kufika.

  (k) Maguo ambayo yanauzwa kwenye majiduka hayo yanavutia.

  (1) (i) Watoto wa Maki walilelewa na Muutu.

  (ii) Maji yalipojaa yalimwagika. Au Maji yalijaa yakamwagika.

  Au Maji yaliyojaa yalimwagika. Au Baada ya maji kujaa yalimwagika.

  (m) Sewe alituelezea jambo hilo tena. Au Sewe alituelezea jambo hilo mara mbili/mara kwa mara.

  (n) viongozi wengi — kirai nomino walikuwa waadilifu mno — Kirai tenzi waadilifu mno — kirai vumishi kabla ya uchaguzi mkuu — kitai husishi uchaguzi mkuu — kirai nomino.

  (i) KN (W * V) +KT (Ts + T) + U + KN (Ø) + KT (T)

  (ii) KN(N+KH)KT(T+E) Au KN( N+W+N) +KT( T*E)

  (i) Nyumba ni ya Medi.

  (ii) Nyumba ni ya mtu mwingine.

  (iii) Medi ndiye atairithisha nyumba.

  (iv) Mtu mwingine ndiye atairithisha nyumba.

  (v) Nyinyi (nafsi ya pili) ndio mtakaorithishwa.

  (vi) Wao (nafsi ya tatu) ndio watakaorithishwa.

  (q) “Jihadhari” akasema Kulei, “uamuzi wako unaweza kukuathiri vibaya.” (r) Mkulima hahitaji magunia haya.

  (s) (i) kusifu — kukashifu kupongeza — kukashifu chache / haba/kidogo — tele

  (iii) Nasaba/akraba/m1ango/ – ukoo Natija/tija – faida

  (t) Maana zifuatazo zijitokeze:

  (i) Kugawanya/kutenganisha, pengine kwa kisu.

  (ii) Ondoa sehemu ya kitu, kwa mfano, kukata ujira/kupunguza kitu.

  (iii) Chombo cha kuchotea maji mtunguni.

  (iv) Eneo la ardhi/sehemu inayoongozwa na kiongozi fulani k.v. Lokesheni.

  (v) Kitambaa au majani yaliyoviringwa kwa ajili ya kuwekwa kichwani kubebea mzigo.

  4.(a) Kuibua utangamano kwa kuwarejelea waumini kama ‘ndugu’, ‘wenzangu’. Kutaja jina la mwenyezi Mungu,/msamiati wa kidini.

  Kumsawiri binadamu kama anayehitaji huruma ya Mungu — ni mwenye dhambi/anayetegemea huruma.

  (iv) Kurejelea vifungu/mifano kutoka msahafu.

   

 • Atumie lugha inayoeleweka na hadhira.
 • Avute makini ya hadhira kwa kuwashirikisha, kwa mfano kupitia maswali ya balagha, kuwarejesha kwenye msahafu.
 • Kutasifidi lugha pale inapohitaji.
 • Lugha isiyowatia waumini unyanyapaa kwa mfano, aepuke kutumia kauli kama vile, “ukimwi unawapata wenye dhambi. .. utakuua”. Huenda kuna walioathiriwa moja kwa moja na ugonjwa wenyewe.
 • Kuzingatia fomyula na mtindo maalum/uliokubalika wa kuendeshea ibada ili wasikanganyike.
 • Kurudia baadhi ya kauli iii kuwaaminisha waumini/kuwafanya waelewe. Kuchanganya msimbo ili kurahisisha uelewa.
 • Kutumia miondoko na ishara ambazo zinakubalika na jamii — lugha husika. Pale anapohitajika/inapobidi atumie toni kali ya kuonya.
 • Atumie lugha inayotia tumaini na matarajio miongoni mwa waumini kuwa hali zao hata zingawa ngumu, zinaweza kutengenea.
 • Atumie mbinu za kushawishi/lugha ya kushawishi ili kuwavutia waumini na kuwadumisha kwenye dhehebu lake.
 • Lugha ya kuelekeza/kushauri. Kwa mfano: “Kesheni mkiomba” “Kaeni tayari kwani hamjui siku atakaporudi”.Tanbihi: Mifano itolewe ili atuzwe alama (1) kamili.
(Visited 141 times, 1 visits today)
Share this:

Written by