KCSE Past Papers 2018 Kiswahili Paper 1 (102/1)

2019 KCSE Kiswahili Paper 1 (102/1)

Majibu

1. Hii ni insha ya kumbukumbu. Vipengele vya:

(a) Kimuundo vya utungo wa aina hii vidhihirike kama ifuatavyo:

(i) Kichwa : Kionyeshe :

(a) Kundi linalokutana

(b) Mahali pa mkutano

(c) Tarehe ya mkutano

(d) Wakati wa mkutano

(ii) Waliohudhuria — vyeo na nyadhifa zidhihirishwe.

(iii) Waliotuma udhuru

(iv) Ambao hawakuhudhuria

(v) Waalikwa / katika mahudhurio/waliohudhuria, bali si wanachama (si lazima).

(vi) Ajenda za mkutano

(vii) Kumbukumbu zenyewe

(a) Utangulizi

(b) Wasilisho la mwenyekiti

(c) Kusomwa na kuthibitishwa kwa kumbukumbu za mkutano uliopita/uliotangulia

(d) Yaliyoibuka kutokana na kumbulcuinbu hizo

(e) Masuala yanayojadiliwa leo / masuala mapya (kulingana na ajenda).

(viii) Masuala mengineyo

(ix) Hitimisho:

(i) sahihi, jina la Mwenyekiti na tarehe

(ii) sahihi, jina la Katibu na tarehe

(b) Maudhui

(i) Mtahiniwa adhihirishe majadiliano na uamuzi uliofıkiwa na wanachama kuhusu hali ya uhabirifu wa mazingira shuleni na katika ujirani wa shule/eneo lao/mtaa.

(ii) Madhara (hatima) ya uharibifu huu yajitokeze. Zifuatazo ni baadhi ya hoja:

(i) Utupaji taka ovyo wa wanafunzi — umesababisha hali kama vile kuambulia magonjwa kama vile pepopunda kutokana na kukatwa na vigae vya chupa.

(ii) Ukataji wa misitu kwenye ujirani ambayo ingepunguza madhara ya upepo mkali.

(iii) Kuacha miti na magugu kujiotea ovyo karibu na majengo ya shule; hiudhoofisha usalama kwani vichaka vinaweza kuwa makao muffi ya majangill rla wanyama/wadudu kama vile mbu.

(iv) Viwanda kwenye ujirani wa shule kuelekeza taka shuleni; matokeo yakiwa magonjwa ya aina mbalimbali.

(v) Mioshi kutoka mabiwi ya taka yanayochomewa karibu na shule.

(vi) Kelele kutoka kwenye magari yanayopita karibu na shule; zinavuruga utulivu madarasani.

(vii) Maeneo ambayo yanaweza kutumiwa kupandia vyakula kutumiwa kwa ujenzi, hlvyo kutîshia kutojitosheleza kwa chakula.

(viii) Majengo yaliyosongamana kwenye ujirani wa shule kuwa hatari wakati wa janga kama vile janga la ınoto.

(ix) Upuliziaji dawa mimea kwenye mashamba jirani; dawa hizi zinaweza kuwadhuru baadhi ya wanafunzi ikiwa upuliziaji haudhibitiwi.

(x) Kuelekeza taka kwenye mito/mto ulio karibu na shule huchafua maji yanayoweza, kutumiwa na wanafunzi. Taka hizi huua wanyama wa majini.

Tanbihi

Hii ni kumbukumbu, si ripoti sharti majadiliano yadhihirike na uamuzi uliofikiwa kuonyeshwa.

2. Utungo uonyeshe madhara ya kudanganya katika mitihani, kwa mwanafunzi na kwa jamii yake. Hoja zifuatazo zijadiliwe:

(i) Udanganyifu husababisha kupata alama ambazo hazilingani na kiwango cha utambuzi cha mwanafunzi.

(ii) Huenda mwanafunzi akapatwa na wasiwasi na hivyo kutofanya vyema.

(iii) Hupalilia upujufu wa maadili hasa unapokuwa na mazoea.

(iv) Humletea mwanafunzi fedheha/hushusha hadhi ya mwanafunzi.

(v) Hushusha hadhi ya shule.

(vi) Huvifanya vyeti vya nchi/vilivyotuzwa na mabaraza ya mitihani nchini kutothaminiwa/kutoaminika kimataifa.

(vii) Wanafunzi wanaweza kukosa nafasi katika vyuo vya kimataifa kutokana na sifa mbaya ya mitihani nchini mwao.

(viii) Udanganyifu unapogunduliwa mwanafunzi hupoteza matokeo.

(ix) Mwanafunzi kuwa mzigo kwa wazazi kulazimika kulipa karo tena ili arudlC. Wazazi kufedheheka.

(x) Baadhi ya wanafunzi hujiua udanganyifu unapogunduliwa.

Xi) Hudhoofisha viwango vya elimu kwani baadhi ya walimu hungojea kufunza yale tu yaliyo kwenye mtihani ulıosambazwa kwao.

(xii) Kufutwa kwa baadhi ya walimu wanaoshukiwa kuhusika na udanganyifu. Wanafunzi waliodanganya kufanya kazi wasizozimudu; hulazimika kubadilisha kozi au kuacha masomo.

(xiii) Kuvyaza wanataaluma ambao humudu kazi zao.

Kudidimiza ubunifu kwani wanafunzl hungojea kupewa maswali, kuyatafutia majibu iii kukidhi haja ya kupita mtihani tu.

(xiv) Husababisha uharibifu wa mali; wanafunzi wanaoshindwa kupata maswali ya mtihani awali, huanza kujiingiza katika vitendo vya utovu wa nidhamu kama vile kuchoma shule.

(xv) Huwafanya wanafiınzl wanaotia bidii masomoni kuvunjika moyo wanaposhindwa na wale wasiotia bidii.

Tanbihi

Sharti mtahiniwa ajadili hoja zinazoonyesha athari kwa mwanafunzi na kwa jamii (kama wazazi, walimu na nchi).

3. Mtahiniwa atunge kisa kinachodhihirisha maana ifuatayo:

Kiongozi /mkuu/mzazi akiondoka/akifa, wale wanaomtegemea/wale anaowaongoza hupatwa na shida/ (huzuni)/hupungukiwa.

Au

Kiongozi/mzazi/mkuu akipotoka wale anaowaongoza/wanaomtegemea hutatizika/hupotoka pia.

Au

Mtahiniwa aonyeshe kwamba matatizo/maovu yanayofanywa na kiongozi/mzazî huiathiri jamii/familia yake vibaya.

Hali zifuatazo zinaweza kujitokeza:

(i) Mzazi afariki, watoto wapate shida kama vile kupokwa urithi.

(ii) Wazazi wazozane, mwishowe wafarakane na kuwasababishia watoto matatizo.

(iii) Baba/mama apotoke, pengine awe mlevi, watoto wainukie kuwa walevi/wakose mahitaji ya klmsingi.

Kiongozi afanye lnaamuzi yasiyofaa, pengine kuchukua mikopo kutoka nchî nyîngine na kuvipagaza vizazi vya kesho madeni.

Kîranja mkuu wa shule apotoke, awapotoshe wanafunzi wenzake. Kiongozi/Viongozi waibe mali ya umma na kuwasababishia raia umaskini. Kiongozi wa kidini apotoke na kuwafanya waumini wapotoke.

Tanbihi

Sehemu mbili za methali zijitokeze:

(i) Kugwa/kuangulca/kupotoka/kufa kwa kiongozi/mzazi/mtu anayetegemewa.

(ii) Kuyumba kwa wana/ kuteseka/kuhuzunika/kupotoka kwa wanaomtegemea.

4. Hii ni insha ya mdokezo.

Mtahiniwa abuni kisa kinachoafikiana na mwe1ekeo/toni/mtazamo wa kauli hii. Kisa kidhihirishe machungu anayoyapitia msemaji (Tuanxa), pengine kutolcana na mtu mwinginc, ugonjwa au hali mbaya inayoınzunguka.

Yafuatayo yanaweza kudhihirika:

(i) Mhusika ametafuta kazi kwa muda asipate, uvumilivu wake unafıkia ınwisho.

(li) Mhusika asimulie kisa aınbamo pengine amekabiliwa na tatizo la kuwa na watoto walemavu, mmoja baada ya mwingine. Anatarajia apate angaa mmoja mwenye afya nafuu.

(iii) Msimulizi awe na mtafaruku na mwenzake; labda mume au mke. Avumîlie hadi ku1”ıkia kiwango hiki.

Msimulizi auguc ugonjwa, atafute matibabu, ugonjwa uendelee kumwathiri hata baada ya kutumia pesa nyingi.

(v) Mhusika akumbwe na matatizo ya ukosefû wa fedha, atafute njia ya kujiinua asipate.

Tanbihi

(i) Kisa sharti kidhihirishe hali mbaya/machungu/mahangaiko/changamoto anazopitia Msimulizi/Mhusika (Tuama).

(ii) Ajaribu/avumilie hadi kufikia kiwango hiki cha kuvunjikiwa.

(iii) Kauli hii inaweza kuwa ndiyo muisho wa kisa, Msimulizi akaturudisha nyuma kulıadithia yaliyotokea.

(iv) Msîmulizi/mtahiniwa pia anaweza kuanza kwa kauli hii na kuendeleza kisa kuanzia hapo bila kutumia mbinu rejeshi.

 

(Visited 196 times, 1 visits today)
Share this:

Written by