KCSE Past Papers 2016 Kiswahili Paper 3 (102/3)

Kenya Certificate of Secondary Education

2016 Kiswahili Karatasi ya 3

Lugha

SEHEMU A: HADITHI FUPI

K. Walibora na S. A. Mohamed: Damu Nyeusi na Hadithi Nyingine

1. Lazima Jadili maudhui ya elimu kwa mujibu wa “Kanda la Usufi”, “Shaka ya Mambo” na “Tazama na Mauti”. (Alama 20)

SEHEMU B:

RIWAYA K. Walibora: Kidagaa Kimemwozea Jibu swali la 2 au la 3

2. Fafanua mjukumu ya elimu na dini katika jamii kwa mujibu wa riwaya: Kidagaa Kimemwozea. (Mama 20)

3. “Wasemao husema, atafutaye hachoki.” (a) Fafanua muktadha wa dondoo hill. (Alama 4)

(b) Kauli hii ina maana gani kwa mujibu wa muktadha huu. (Alama 2)

(c) Jadili umuhimu wa kinachotafutwa katika riwaya ya Kidagaa Kimemwozea. (Alama 14)

SEHEMU C:

TAMTHILIA T. Arege: Mstahiki Meya Jibu swali la 4 au la 5

4. “Anwani Mstahiki Meya ni kinaya.” Jadili ukweli wa kauli hii kwa kurejelea tamthilia. (Alama 20)

5. “…dawa ya adui ni kummegea unachokula.”

(a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (Alama 4)

(b) Jadili jinsi dawa inayorejelewa inavyozorotesha hali katika mji wa Cheneo. (Alama 16)

SEHEMU D:

USHAIRI Jibu swali la 6 au la 7 6.

Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali. Kilio cha Lugha

Ni wimbo najiimbia, nijiliwaze

Sina wa kusaidia, nasongwa sina

nafasi Kiwa kwetu naumia, kwcngine

si mahususi Lugha ya mtu mweusi, Kiswahili chalilia.

Wataalamu ni nani, mulipo mwaninyanyasa

Hamna nami imani, wala kupanga siasa,

Mwasema sayansini, siku ningalitosa,

Mwanambia nikotosa, kuiva sijafika.

Ela muelewe sana, Maamuma na Imamu,

Mulipokuwa vijana, kwenu nilikuwa timamu,

Sasa mumesoma sana, mwaniona ni haramu,

Mujue kuwa dawamu, utumwa mwauridhia.

Mzaliwapo mwalia, `maa’, maneno ya kwanza,

Lugha munayokulia, ya mama zetu ya kwanza,

Wa lugha muwedoria, muweze na kuikuza,

Sio kujipendekeza, uzungu kuigiza.

Majira ya ukoloni, ukombozi kusambaza,

Lugha mulithamini, Kiswahili kufukiza,

Hata kule risavuni, kizungu hanikuwaza,

Sasa mbona mwanibeza, mbali mwanitupilia?

Sayansi sio asili, msamiatiwe sinao,

Sayansi yataka mbali, msamiati ni wa hao

Nitakuwa Kiswahili, kiomba majina yao

Lugha kujikuza kwao, huomba linalofaa.

Enyi viongozi wetu ipangeni nadharia,

Kujenga siasa yetu, tuzidi kuwa huria

Lugha hata `mbusha watu, tuche kuriaria,

Sifa ni kwa chake mtu, cha mwenzi hutoringia.

Utajiri wangu hasa, nikiwatajia wote,

Msamiati huwa, ni wa Afrika yote,

Na methali za kuasa, nahau na ngeli zote,

Na nisemwapo popote, ujumbe hukamilika.

Afrika ndipo petu, pa wabantu halisi,

Baba na mama ni Bantu, shina la wangu ukwasi,

Warabu na wengi wetu, sio wangu Adinasi

Kwao `meomba kiasi, iii kujizidisha.

Mfumo mpya hongera, wa elimu humu Kenya,

Lugha takuwa imara, ukabila tutafinya,

Kiswahili ni ibara, kila mtu kiimanya,

Methali imetuonya, mtumwa si mwasilia.

Tamati lugha yalia, yabaguliwa bayana,

Kukua imeridhia, msamiati kufana,

Wengine wataijulia, kwa marefu na mapana,

Lugha yenu ya maana, mwaipuuza yalia.

(a) Shairi hili ni la aina gani? Toa sababu. (Alama 2)

(b) Kwa kutoa hoja nne, eleza kwa nini shairi hill likaitwa kilio cha lugha. (Alama 4)

(c) Andika ubeti wa tatu kwa lugha ya nathari. (Alama 4)

(d) Eleza toni ya shairi hili. (Alama 2)

(e) Tambua uhuru wa kishairi uliotumiwa kwa kurejelea mifano mitatn. (Alama 3)

(f) Bainisha nafsineni katika shairi. (Alama 2)

(g) Eleza maana ya maneno yafuatayo kwa mujibu wa shairi. (Alama 3)

(i) nasongwa

(ii) kuriaria

(iii) adinasi 7. Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.

T. Arege: Barabara

Barabara bado ni ndefu

Nami tayari nimechoka tiki

Natamani kuketi

Ninyooshe misuli

Nituliza akili.

Lakini

Azma yanisukuma

Mbele ikinihimiza kuendelea

Baada ya miinuko na kuruba

Sasa naona unyoofu wake

Unyoofu ambao unatisha zaidi.

Punde natumbukia katika shimo

Nahitaji siha zaidi ili kupanda tena

Ghafla nakumbuka ilivyosema

Ile sauti zamani kidogo

“Kuwa tayari kupanda na kushuka.”

Ingawa nimechoka

Jambo moja li dhabiri

Lazima nifuate barabara

Ingawa machweo yaingia

Nizame na kuibuka

Nipande na kushuka.

Jambo moja nakukumbukia: Mungu

Je, nimwombe tena? Hadi lini?

Labda amechoshwa na ombaomba zangu

Nashangaa tena!

Kitu kimoja nakiamini

Lazima niendelee kijitahidi kwa kila hatua mpya

Nijikokote kuiandama hii barabara yenye ukungu

Nikinaswa na kujinasua

Yumkini nitafika mwisho wake

Ingawa wangu mwisho haitauwahi kabla.

(a) Eleza toni ya shairi hili. (Alama 2)

(b) Tambua nafsineni katika shairi hili. (Alama 2)

(c) Mshairi ana maana gani anaposema “Kuwa tayari kupanda na kushuka” katika ubeti . wa tatu? (Alama 2)

(d) Fafanua tamathali tano za usemi zilizotumiwa katika shairi hili ukizitolea mifano mwafaka. (Alama 10)

(e) Eleza ujumbe unaojitokeza katika ubeti wa tano wa shairi hili. (Alama 2)

(f) Eleza maana ya:

(i) kuruba

(ii) barabara yenye ukungu (Alama 2)

SEHEMU: FASIHI SIMULIZI

8. (a) Kwa kutumia mifano mwafaka eleza majukumu matano ya nyimbo katika jamii. (Alama 10)

(b) Ili kuweza kufanikisha uwasilishaji wa utanzu wa nyimbo kwa hadhira eleza mambo anayohitaji mwimbaji. (Alama 10)

 

 

(Visited 172 times, 1 visits today)
Share this:

Written by