BKS 122: MISINGI YA SARUFI

CHUO KIKUU CHA MAASAI MARA
BACHELOR OF ARTS KISWAHILI
BKS 122: MISINGI YA SARUFI
AUGUST 2015 TIME: 2HRS

MAAGIZO:
Jibu maswali MATATU. Swali la KWANZA ni la lazima.

Swali la Kwanza
a) Fafanua dhana zifuatazo;
i. Sarufi
ii. Viambishi
iii. Ngeli
iv. Kielezi
v. Kihisishi (alama 10)
b) Kwa kuzingatia kigezo cha Kisintaksia, fafanua ngeli za Kisawhili. ( alama 20)
Swali la Pili
a) Huku ukitoa mifano, fafanua sehemu tatu kuu katika kitenzi. ( alama 6)
b) Tathmini matumizi ya mofu zifuatazo katika vitenzi
i) Mofu za wakati ( alama 6)
ii) Mofu za hali ( alama 8)
Swali la Tatu
Fafanua aina zozote SITA za vivumishi. ( alama 20)
Swali la Nne
Huku ukitumia michoro matawi, toa vielezo vya sentensi zifuatazo
a) Gari bovu lilipata ajali.
b) Maria analima na mama anapika.
c) Mvua iliyonyesha jana ilisababisha mafuriko.
d) Wakulima walivuna mahindi mengi . ( alama 20)
Swali la Tano
Eleza umuhimu wa kuakifisha katika matumizi ya lugha. ( alama 20)

(Visited 165 times, 1 visits today)
Share this:

Written by