KCSE Past Papers 2013 Kiswahili Paper 3 (102/3)

  • 5.2.3 Kiswahili Paper 3 (102/3)

    FASIHI SIMULIZI

    l. (a) Maana ya Vitanza Ndimi

    Vitanza ndimi ni virai/vishazi au sentensi zenye sauti zinazokaribiana au zinazofanana’ kimatamshi na ambazo hutatiza rntu kuzitamka. Aghalabu huundwa kwa vitate, vitawe, au hata kurudia maneno yalc yalc katika scntensi. Kwa mfano:

    (i) Wali huliwa na mwana wa liwali.Asiyekuwa mwana wa liwali hali wali.

    (ii) Wali huliwa na wanawali, wasio wanawali hawali wali.

    (iii) Shirika la reli la Rwanda lililiathiri lile la reli la Kenya.

    (iv) Mzee aliyevaa koti lililofika gotini alianguka akaumia goti kisha koti lake lenye kufika magotini likachanika. (alama 2)

    (b) Majukumu ya Vitanza ndimi

    (i) Kumzoesha mtoto/mtu kuzitamka sauti au maneno vizuri.

    (ii) Ni nyenzo ya burudani. Vikao vya mashindano ya utamkaji hutumiwa kuwachangamsha wanajamii.

    (iii) Msingi wa kumsaidia mtolo kujua lugha kwa undani. Huundwa kwa vitate au vitawe, hivyo mtu hujifunza vipengele hivi vya lugha.

    (iv) Husaidia kuimarisha uwezo wa kimawasiliano wa anayehusika. Utamkaji wa vitanza ndimi kwa kasi humzocsha mzungumzaji kuweza kuwasilisha hoja bila kusitasita.

    (v) Huendeleza utamaduni. Jinsi wanajamii wanavyoshirikishwa katika utamkaji ndivyo wanavyorithishwa utamaduni wao au dcsturi yenycwe ya kushiriki katika utamkaji.

    (vi) Hujcnga stadi ya ukakamavu. Kadiri mtu anavyoshiriki katika utamkaji ndivyo anavyoimarisha ujasiri wake wa kuzungumza hadharani.

    (vii) Huibua ucheshi na kudumisha uhusiano mwema. Utani unaoibuliwa katika mashindano ya utamkaji ni msingi wa kujenga uhusiano.

    (viii) Hukuza ubunifu. Wanajamii huweza kubuni vitanza ndimi hapohapo, wakavitamka.

    (ix) Ni kitambulisho cha jamii. Kila jamii ina vitanza ndimi vyake vinavyohusu mazingira yake.

    (x) Hukuza utangamano katika jamii. Vikao vya mashindano ya utamkaji huwaleta wanajamii pamoja hivyo kujihisi kuwa kundi moja.

    Tanbihi

     

  • Kuonya/kushauri – baadhi hufumbata maonyo/ushauri. Kwa mfano, Mzaha mzaha huzaa usaha. (6 x 1 = 6)c. Utazamaji wa kushiriki au kutoshiriki. Mtu anaweza kushiriki katika kikao cha utamkaji wa vitanza ndimi, hivyo kujua vinavyoendelezwa katika jamii husika.

     

  • Video. Mtu anaweza kupiga picha za video watu wakitalmka/wakishindana katika. utamkaji wa vitanza ndimi ili kuja kuchanganua baadaye.
  • Matumizi ya hojaji. Mtu anaweza kuandaa maswali katika hojaji ili kudadisi kwa mfano, kama vipo katika jamii fulani, wanaohusika katika vikao vya utamkaji na uundaji wake.
  • Kurekodi kimaandishi (kuandika) ili kuvirithisha au hata kuvichanganua baadaye.
  • Majadiliano ya vikundi lengwa, Mtafiti anaweza kutcua vikundi, kwa mfano, vijana,i1i kuchunguza namna wanavyoviunda na kuvitamka, na athari ya vitanza ndimi hivi kwao.
  • Mahojiano Mtafiti anaweza kuandaa mahojiano rasmi na kundi / sampuli lengwa ili kuchunguza kwa mfano, majukumu ya vitanza ndimi katika jamii husika
  • Matumizi ya vinasa sauti na sidii ili kunasa utamkaji wenyewe na kuchanganua sifa zake.
  • Kutumia kumbukumbu ya mtafiti mwenyewe. Utafiti ambaye in mmoja wapo wa wanajamii katika eneo analofanyia utafiti anaweza kurithisha yale anayokumbuka baada ya kuyashuhudia.
  • Kusoma majarida na vitabu (maktabani) vyenye habari kuhusu vitanza ndimi. (6 x 2 = 12)Hoja zifafanuliwe ili kupata alama kamili.

    Utengano: Said A. Mohamed

    2. a) Ni shairi analolikumbuka (Inspekta) Fadhili katika diwani yake: Kilio cha Wanyonge.

    Au:

     

  • Ni maneno ya Fadhili Katika diwani yake : Kilio cha Wanyange. ~
  • Yumo nyumbani (sebuleni)mwa Maksuudi.
  • Alikuwa ameitwa na Maksuudi.
  • Ameyaona mabadiliko (fanicha) katika sebule ya Maksuudi ndipo akakumbuka haya.(4 x l = 4)

    Tanbihi

    Dondoo limetolewa uk. 71 – 72

     

  • Kinaya – Wafanyakazi kufanya kazi kwa bidii lakini wanalala njaa
  • Sitiari – Njaa kufananishwa moja kwa moja na msumeno.
  • Taswira – Picha ya watu wakimenyeka/wakiteseka. Picha ya msumemo ukikeketa matumbo. 
  • Jazanda – Msumeno ni jazanda ya njaa inaydwaumiza raia. »(2 x 2 = 4)

    c. Wakulima wanalima lakini mapato hawayapati Rejelea maneno ya Shoka (Uk. 113).

  • Wanyonge kuandamwa na magonjwa (uk. 72).
  • Wakulima wanapunjwa; wageni k.v Marekani ndio wanaodhibiti bei za mazao.
  • Maimuna, Dora na wenzake danguroni kwa Mama Jeni – wanashiriki ukahaba lakini mapato yanamwendea Mama Jeni.
  • Maimuna anatumiwa na Bili Sururu kama kivutio cha walevi. Biti Sururu anamtazama na kusema kimoyomoyo atawafaa (UK.95). Anawaambia walevi amepata kisura. Kazi kwa Biti Surum inamfanya Maimuna kudhoofika kiafya.
  • Wazazi k.v Mama Dora anamtelckeza kwa kumuuza kwa Mama Jeni.
  • Dora anakuwa kahaba.
  • Dhuluma katika ndoa – Tamima kutawishwa, kupigwa – Mwanasururu na kutalikiwa na Maksuudi.
  • Dhuluma katika malezi – Maimuna kutawishwa, Maksuudi kukinyima kitoto chake na Tamima malezi ya mama na kusababisha kifo.
  • Wanawake kubaguliwa katika eiimu. Maimuna anasomeshewa nyumbani ilhali Mussa amesoma hadi chuo kikuu.
  • Maimuna kutumiwa kama chombo cha kuzalisha pesa pale Rumbalola – mapato yanamwendea mwingine.
  • Maksuudi kumpokonya Mwanasumru mali na kumfanya kuishia kuwa mwendawazimu.
  • Wizi/unyakuzi wa mali ya umma. Maksuudi kunyakua shamba la Via – kina
  • Haji wanaishia kuwa maskini wanaomtcgcmea.
  • Maksuudi kuwatesa wanyonge, anauza sahihi yake; anamtaka mke wa Mzee
  • Japu kulipa shiilingi 200 kwa sahihi yakc tu (Uk. 78).
  • Mwanasururu anamtaka Kabi kutenda yasiyofaa na baadaye kusababisha kukzxi”-.. .. kwa mguu wake.
  • Biti Kocho na Farashuu wanamtorosha Maimuna na kumwingiza kwenyc mtandao wa ufasiki / ukahaba.Tanbihi

    a) Farashuu anamuumbua Maimuna mbele ya mchumba wake – Kabi. Anamwita mhuni na mchafu (uk.l68)

  • Raia wametekelezwa kwenye ujinga na umaskini. Maazimio ya baada-uhuru. kutofikiwa (uk. 72).
  • Kazija anashirikiana kimapenzi na Mussa ambaye ana umri mbichi, kwa nia ya kumtenganisha Mussa na babake. Anaishia kumfanya kupigwa na baba yake. ’ Anawatenganisha.
  • Farashuu – kumenyeka kazini, mwanawe Mwanasururu kudhulumiwa, mazingira duni, n.k.
  • Maksuudi – baada ya kifungo, kupoteza asilimia kubwa ya mali yake, kupoteza hadhi, kuumbuliwa na Maimuna pale Rumbalola, ukiwa unaomwandama baada ya kusambaratika kwa familia yake, kipigo na ugonjwa, Tamima kukataa kumsamehe, nk.(a) Mnyonge anaweza kufasiriwa kwa namna zufuatazo:
  • Maskini
  • Asiye na mamlaka kisiasa
  • Anayehitaji msaada
  • Mwenye umri mdogo kuliko mwingine
  • Aliye katika hali fulani, kama vile ugonjwa
  • Mwana kwa mzazi
  • Wafanyakazi(b) Kumenyeka kunaweza kumaanisha:

     

  • Utangulizi
  • kuteseka
  • kudhulumiwa/kunyimwa haki
  • kuaibika
  • kutofikia maazimio
  • kutengwa na familiautangulizi

    Wahusika na maudhui huchangiana kujenga kazi ya sanaa. Wahusika huteuliwa kuendeleza maudhui. Matendo yao ni msingi wa maudhui. Nayo maudhui hujumuisha matukio au hali zinazowaathiri wahusika. Tabia za wahusika huathiriwa na hali au matukio yanayowazunguka

    a)Shoka

     

  • Anaendeleza maudhui ya ukoloni. Anapinga hali ya wafanyakazi kuzalisha mali bila kufaidika.
  • Anaonyesha ukosefu wa uwajibikaji katika ndoa. Anamwachia Sclume mzigo wa malezi.
  • Anaendeleza uozo wa kijamii (usherati) kwa kuhusiana na Maimuna kimapenzi.
  • Anaendeleza ukandamizaji wa wanawake. Anamwambia Selume hatamwacha talaka, anamwachia ulimwengu umtimbe.
  • Anaonyesha matumizi mabaya ya vileo. Pesa zake zinaishia vilabuni.
  • Anacndeleza maudhui ya ubinafsi. Anakula nje na kuja kugawana kidogo kilichoko na wanawe.
  • Anaonyesha changamoto zinazohusishwa na ndoa. Ingawa anamtcsa Selume, Selume bado anaishi naye kutokana na mapenzi ya Selume kwake.
  • Ni ishara ya ubabedume Anatarajia mkewe amheshimu licha ya kwamba hamshughulikii. Selume analalamikia utumwa wa wanawake.
  • Anaonyesha ajizi ya wanawakc / ukosefu wa wanawake kung’amua hadhi yao.
  • Selume anadai kuteseka lakini mumewe akikosa kurudi anakwenda kumtafuta.
  • Anachimuza / Ni ishara ya shida zinazowakabili wafanyakazi. Wachukuzi na wakulima wanafanya kazi za sulubu na hali mazao yanawaendea wageni.
  • Ndiye anayesababisha na kukuza ugomvi kati ya Maimuna na Kijakazi, hivyo kuonyesha jinsi wanawake wanavyong’ang‘ania kuwategemea wanaume.(5 x 2 = 10)

    b) Kazija

     

  • Ni kielelezo cha ukandamizaji wa jamii ya mwanamke. Anasema mamlaka, elimu na pesa zote ni kwa mwanamume.
  • Anaendeleza upujufu wa kimaadili kwa kushirikiana na Mussa na babake kimapenzi.
  • Anaonyesha wanawake kama vyombo vya kusambaratisha asasi ya familia.
  • Anamtenganisha Maksuudi na Mussa. Anamtcka maksundi kuzuru kwake hata kumwacha mkewe akiwa mja mzito.
  • Anaendeleza dhamira ya kisasi. Anamkutanisha Mussa na babakc ili kumlipizia kisasi Farashuu.
  • Ndiye anayewafichulia raia unafiki wa Maksuudi hivyo kuendeleza maudhui ya mapinduzi.
  • Anachangia katika mwamko wa kijamii. Anawafanya raia kutomchagua Maksuudi na Zanga.Tanbihi

     

  • Anaendeleza maudhui ya tamaa na ubinafsi. Anahusiana na Maksuudi na Mussa ili afaidike kwa fedha zao.
  • Anaendeleza maudhui ya unafiki. Anamwita Maksuudi Bwana ili aendelee kufaidika kwake.
  • Ni kielelezo cha ujasiri. Kule kumkabili Maksuudi katika uwanja wa uhuru kunaonyesha ukakamavu wake.
  • Kutatizwa kwake katika ploti kunaakisi kutojengeka (kutokamilika) kwa dhamira ya ukombozi wa mwanamke. Mwandishi anambainisha tu mara_mbili katika hadithi na baadaye kumfifilisha. i
  • Anafichua (anaonyesha) mfumo wa ubabedume. Anamchukia mwanamume kwa kuwekwa mbele. Anachukia kujipamba ili kumfurahisha mwanamume.
  • Anaonyesha usaliti wa viongozi k.v Zanga ambaye hatimizi ahadi alizowapa waliomchagua.,p> (5 x 2 = 10)Si lazima mtahiniwa atangulize kwa kuonyesha uhusiano kati ya maudhui na wahusika.

    La muhimu ni kujadili maudhui, hali au dhamira zinazoendelezwa na wahusika aliopewa.

    Mstahiki Meya: T. Arege

  • Badala ya Meya kushughulikia matatizo ya Wanacheneo, anasema Cheneo ni kisiwa cha kupigiwa mfano. Anajifananisha na majirani dhaifu kiuchumi na kukosa kuiendeleza Cheneo zaidi.
  • Meya anaupujua uongozi wa Cheneo kwa kuwaacha washauri wapotoshi kuuingilia. Anamhusisha Bili katika maamuzi muhimu kama vile utoaji wa kandarasi na hali Bili si mtaalamu katika masuala haya.
  • Meya anaifilisi Cheneo kwa kuidhinisha malipo yasiyofaa kama vile nyongeza ya mshahara wa madiwani, na malipo kwa Bili kwa kutoa ushauri ambao kwa kweli unahusu wizi wa fimbo ya Meya. –
  • Viongozi wa kidini kama vile Mhubiri wanachangia katika kudhoofika kwa uongozi wa kisiasa kwa kutomshauri Meya vyema. Anamwombea Meya ili naye (Mhubiri) afaidike kwa sadaka anayoidhinisha Meya.
  • Viongozi wanaufisidi uchumi kwa kutotekeleza malengo ya kimaendeleo. Meya anasema yeye anazingatia maazimio ya kimilenia ambayo kwa kweli hayashughulikii; watoto bado wanakufa kwa magonjwa yanayotokana na ukosefu wa lishe.
  • Viongozi wanawaachia wageni kuingilia masuala ya kiuchumi. Maamuzi muhimu kama vile kugawana kwa gharama ya matibabu yanatolewa na wageni na kuwafanya raia watesekc.
  • Meya anaifanya jamii ya Cheneo kuwa tegemezi kwa misaada. Anahofia kwamba hali ya usaii ikizorota wafadhili hawatakuja.
  • Viongozi wanaufifilisha uchumi kwa ubadhmfu wao. Meya anatumia pesa za ufadhili kununulia mvinyo kutoka ng’ambo badala ya kuanzishia miradi.
  • Meya anapunguza kodi ya mapato ya Baraza kwa kuidhinisha kutolipa kodi kwa madiwani. Kupuuza malalamishi ya wafanyakazi kunasababisha kutokusanywa kwa pesa, hivyo kuliteteresha pato la Baraza.
  • Wafanyakazi kama vile Waridi wanajiuzuiu wanapoona hali ni mbaya badala ya kukabiliana nayo.
  • Viongozi wanashindwa kuwahakikishia raia usalama wa chakula. Mama anamlisha mwanawe wali na maharagwe yaliyolala na kusababisha kifo. Anasema wanakula chakula cha mbwa.
  • Wanataaluma wanajiepusha na siasa, hivyo kutochangia kuiboresha siasa (mfano Siki).
  • Kumpa Meya mamlaka makubwa kunachangia kupalilia udiktela badala ya demokxasia.
  • Kutoshughulikia afya ya kijamii kunasababisha magonjwa kama vile utapiamlo yanayotokana na ukosefu wa lishe.Waridi anashangaa vipi mama anawaletea mtoto mwenye ugonjwa wa utapiamlo; kwake hili ni jambo dogo.
  • Badala ya raia kuimarisha viwango vya climu na huduma za afya, wanawapeleka jamaa zao ng’ambo kwa huduma hizi. Meya analalamikia eiimu duni, anampeleka mwanawe kusomea ng’ambo. Anampeleka mkewe kuzaiia ng’ambo. Kwa njia hii anaujenga uchumi wa nchi husika na kuuibia ule wa Cheneo.
  • Meya analiibia baraza na kuufisidi uchumi wake kupitia kwa kandarasi. Pia anaidhinisha wizi wa fimbo ya Meya/ardhi.
  • Askari wanazorotesha amani na usalama wa raia. Wanawahangaisha raia kwa bunduki na vitoa machozi.
  • Viongozi wanasababisha kuzorota kwa hali ya usafi Cheneo kwa kutoshughulikia malalarnishi ya wafanyakazi. I-Iili linailctca Cheneo aibu na kuiumbua machoni mwa jamii ya kimataifa. Wageni wanaahirisha ziara yao. Mji umejaa uvundo unaohisika hata nyumbani mwa Meya.
  • Watu wanawachagua viongozi licha ya kujua kuwa viongozi hao wamekosa uwajibikaji, hivyo kuzizorotesha siasa za nchi/kuuzorotesha uongozi wa kisiasa. Meya anauangamiza uongozi wake mwenyewe kwa kupuuza ushauri wa Diwani wa III na Siki.
  • Mapuuza ya Meya yanapalilia ukosefu wa utuiivu kupitia kwa migomo ya wafanyakazi.
  • Meya analifilisha Baraza kwa kulipagaza deni. Bili anamshawishi amwambie mwanakandarasi alishtaki Baraza alipwe fidia, naye Meya apate fungu lake.
  • Meya na madiwani wanazorotesha uongozi kwa kutumia mbinu hasi za utawala kama vile propaganda, badala ya kuyashughulikia matatizo.5. (a) (i) Haya ni maneno ya Meya.

     

    Tanbihi

    (ii) Anamwambia Bili.

    (iii) Wamo afisini mwa Meya.

    (iv) Meya anaelezea sababu za kuwapeleka wanawe ng‘ambo_kusomea huko.

    Dondoo limetolewa uk.25.

    Nakala nyingine zinaweza kutofautiana kiukurasa. (b)Kinaya, Meya anaikosoa elimu ambayo anastahili kuiboresha. (alama 2)

    an Kejelildhihakal stihizai. Meya kuidunisha elimu. Meya anajidhalilisha kwa kudunisha elimu ambayo anastahili kuiboresha mwenyewe. (alama 2)

    Kinaya

    (i) Kauli ya Meya inadokeza kuwa yeye ni mzazi mwenye busara (kuona mbali) na hali anahiari kutumia pesa nyingi kuwasomeshea wanawe ng‘ambo badala ya kuboresha elimu humu.;

    (ii) Meya anawadanganya raia kwamba dawa zimeagizwa ilhali sivyo, hatutarajii haya kutoka kwa kiongozi.

    (iii) Meya anadai Cheneo ni kisiwani cha hazina na hali watu wanakufa (yule mtoto) kwa kukosa huduma za afya.

    (iv) Badala ya Meya na madiwani kuendeleza mpango wa kimaendclco wa mji, Meya anadai kwamba wanathamjni malengo ya kimilcnia na hali kwa kweli hata haya hayashughulikiwi.

    (v) Meya anamruhusu Bili kuiba fimbo ya Meya ambayo kwa kweli ndiyo kitambulisho cha umeya.

    (vi) Meya anampeleka mkewe kujifungulia ng’ambo badala ya kuimarisha huduma za kiafya Cheneo.

    (vii) Meya anataka mwanawe apate uiaia ng’ambo na hali yeye ni kiongozi anayetarajiwa kupalilia uzalendo.

    (viii) Meya anabadhiri mali ya umma kupitia ‘entertainment vote’, huku akidai kuwa ni matunda ya jasho lake. Haya hayazarajiwi kwa kiongozi.

    (ix) Meya anaidhinisha kuongeza mishahara ya madiwani ilhali Baraza lina nakisi ya fedha.

    ( x)Meya kulalamikia udogo wa mayai na hali watu hawana chakula.

    (xi)Meya analipagaza baraza deni badala ya kulisaidia kutumia fedha vyema.

    (xii)Meya analalamikia kupunjwa kwa kuletewa viyai vidogo na hali yeye anawapa wafanyakazi mishahara duni.

    (xiii) Watu wanamchagua Meya wakitarajia kuimarika kwa hali zao za maisha. Meya anaishia kuwatelekeza katika njaa na magonjwa .

    (xiv) Meya anaidhinisha pendekezo la Diwani H la kuundwa kwa kamati za kuhudumu na hali anafahamu kwamba baraza halimudu gharama hii.

    (xv) Ni kinaya kutarajia mama muuza ndizi kulipa kodi na hali Meya anawaruhusu walionacho kama vile madiwani na kutolipa.

    (xvi) Meya, badala ya kudhibiti matumizi mabaya ya mali ya umma, anajigawia vipande vinane vya ardhi na kumgawia Bili pia.

    (xvii) Ni kinaya kwa Meya kutomshughulisha Diwani III katika maamuzi yanayohusu matumizi ya fedha na hali ndiye mtaalamu katika masuala haya.

    <xviii)ni kinaya=”” kwa=”” meya=”” kumruhusu=”” diwani=”” i=”” ambaye=”” anastahili=”” kulihakikishia=”” baraza=”” usalama=”” kufanikisha=”” wizi=”” wa=”” fimbo=”” ya=”” meya.<p=””>(xix)Meya anaidhinisha Baraza kutoa sadaka ya shilingi laid moja kila mwezi na hali anajua lina nakisi ya fedha.</xviii)ni>

    (xx)Badala ya Meya kushughulikia matatizo ya raia, anaeneza propaganda kupitia Diwani I kuhusu kujitolea kwa Baraza kutetea demokrasia.

    (7 x 2= I4)

    b)Mtahiniwa anaweza kuibua hoja zifuatazo kuhusiana na kejeli.

    Kejeli

     

  • Anwani ya tamthilia inafumbata kejeli kwa kumwita Meya mstahiki na hali hata anaidhinisha wizi wa fimbo yake.
  • Meya anajidhalilisha kwa kulalamikia mambo madogomadogo kama vile mayai. Uongozi wa Meya unadhihakiwa kwa kushindwa hata kuiendesha zahanati. Zahanati haina hata dawa za kimsingi. _
  • Meya anaikejeli elimu ya humu nchini kwa kusema ni duni mno; kwa njia hii anajidhalilisha pia kwani yeye anastahili kuchangia kuiboresha .
  • Meya anajidhalilisha mwenyewe kwa kumwachia Bili kuliendesha Baxaza na hali Bili si mtaalamu katika masuala ya uongozi.
  • Meya anaudunisha uongozi wake kwa kuidhinisha nyongeza ya mishahara ya madiwani huku akifahamu kwamba hazina ya Baraza haimudu kughaxamia nyongeza hii.
  • Mwandishi anamkcjeli Meya kwa kumfanya kushindwa kung’amua udanganyifii wa Bili.
  • Mwandishi anamkejeli Meya kwa kumfanya kutumia pesa za msaada kuagizia mvinyo kutoka ng’amb0 na kuishia kurudisha pesa hizo hizo huko ng’ambo.
  • Meya anadai kwamba kungekuwa na Phd ya uongozi angekuwa nayo na hali anaendeleza mbinu hasi za uongozi kama vile propaganda.
  • Meya anasawiriwa kama mwenyc mawazo finyu, anayeshindwa kuona umuhimu wa mpango wa kimaendeleo wa Cheneo. ‘ ,
  • Meya anadhihaki uongozi wake kwa kuidhinisha malipo kwa kazi ambayo haijatekelezwa. Anaidhinisha kulipwa kwa Bili.
  • Meya anajidhalilisha kwa kulipagaza Baraza deni. Anakubali mshawasha wa Bili kwamba amwambie mwanakandarasi alishtaki Baraza n.k.
  • Meya amajidhalilisha kwa kudai kuwa ni mzazi mwenye kuona mbali na hali hata anashidwa kung’amua umuhimu wa usafi. Pia anahadaiwa na Bili kwa urahisi.(7 x 2= 14)

    Tanbihi

    (i) Hoja zinazohusu kinaya zinaweza pia kujadiliwa kama kejeli au stihizai, mradi mtahiniwa amezifafanua zikaeleweka kuwa ni Kejeli.

    (ii) Mifano yote, ihusiane na Meya hata kama inawarejelea wahusika wengine.

    (iii) Baadhi ya watahiniwa, ambao si makini, huenda wakachukulia kuwa tamamali ya usemi iliyotumiwa ni nahau au msemo (anayeona mbali). Hawa washughulikiwe kulingana na jinsi wanvyojieleza na kutoa mifano. Hata hivyo, mifano ya semi wanayotoa lazima, ihusiane moja kwa moja na Meya.

    Ushairi

    6. (a) Mzungumzaji (nafsineni) asingiziwa ugumba hasa kwa kutoshiriki mapenzi nje ya ndoa.

    (1 x 2 = 2)

    (b) Mambo ambayo anapinga ni:

     

  • Kuiga rika; hususa kushiriki ulevi pamoja na kufukuza wasichana
  • Mzungumzaji kupakwa topc (kuaibishwa) kwa kuwa ycye ni gumba
  • Wamsemao kudai kuwa anatamani kuwa kama wao
  • Eti kuwa ugumba na ukapera ni kosa
  • Kuharibu maisha kwa ujana
  • Kusingiziwa atapenda (atatamani) hali za wamsemao
  • Watu kueneza uvumi kuwa yeye ni gumba (5 X l = 5(c) Umuhimu wa viishio

     

  • Viishio hivi ni vifupi na hivyo vinatoa ujumbe kwa namna iliyo madhubuti
  • Viishio hivi vinaunga ujumbe wa kila ubeti/vinasisitiza ujumbe; wa shairi
  • Viishio vinachimuzafkuonyesha/kubainisha dhamira au mwelekeo wa mshairi kuhusu hali ya vijana kujiingiza katika mahusiano yasiyofaa. (1 x 2 = 2)d)Mtindo ufuatao unaweza kukubalika:

    Ni jambo gani ambalo linamkasirisha Mungu ambalo halikubaliki kanisani? Je, ni mtu kuwa kahaba na mwenye vioja ama mtu aliyezaliwa akiwa tasa? Kuwa gumba au kapera si kosa na wala haliwezi kuwa kosa. Kwa kweli mimi sina makosa.

    (4 x 1= 4)

    e)

  • Kila ubeti una mistari minne.
  • Mistari mitaru ya kwanza ina viapande vitatu ilhali wa nne una kipande kimoja.
  • Vina katika kila ldpande vinabadilika kutoka ubcti mmoja hadi mwingine.
  • Kiishio kimefupishwa.
  • Kila mstari una mizani 20 isipokuwa kiishio chenye mizani 8.
  • Shairi lina beti 5.(4 x 1 = 4)<p) f)mbio=”” za=”” wasichana=”” -=”” uasherati=”” uzinzi=”” uzinifu=”” <li=””> Haupandiki mgomba – hana uwezo wa kujamiiana.</p)>

    (2 x 1 = 2)

    7. a)Shairi hili ni wasia kwa vijana; unaowaonya dhidi ya kushiriki mapenzi.

  • Linashauxi kuwa wanaovutia machoni wanaugua na hivyo wanaweza kuwaambukjza maradhi yasiyotjbika.
  • Zinaa hii haichagui wala kupendelea yeyote. Hata wenyc nguvu au warembo wamesalimu amri (ubeti 4).
  • Vijana wajikaze kuhakiksiha kuwa hawaingii kwenye mtego wa kushiriki mapenzi.
  • Wapo watakaowasema wenyc kujitunza lakini hilo lisiwafanye kutetereka.(4 X 1= 4)

    b)Tabdila – Kubadili miendclezo ya maneno pasi na kubadili idadi ya-mizani. Neno ‘nisikia‘ lingekuwa ‘nisikie’.

  • (i) Limetumiwa hivi ili kukidhi mahitaji ya vina. ii.Inkisafi – kufupisha maneno. Inkisaxi imetumiwa kuleta ulinganifu wa mizani. Maneno yaliyofupishwa nikama vile: 
  • ‘Sikuwambia’ badala ya ‘Sikuwaambia’ 
  • ‘Jepusheni’ badala ya ‘Jiepusheni” 
  • ‘ngawa’ badala ya ‘ingawa’ 
  • ‘waone’ badala ya ‘uwaone’ ‘mkamba‘ badala ya ‘mkaamba’
  • ‘ngia’ badala ya ‘ingia‘
  • ‘walopapia’ badala ya ‘waliopapia’
  • ‘watalokwamba’ badala ya ‘watakalokwamba’iii.Miundo ngeu ya kisintaksia / kuboronga sarufi. Mpangilio wa maneno katika tungo haufuati utaratibu wa kisarufi wa lugha ya Kiswahili. Baadhi ya matumizi ya mbinu hii ni: ’

    (a) ‘yaugua nisikia’ badala ya ‘nisikie yaugua’

    (b) ‘si mlango nyumba nzuri‘ badala ya ‘nyumba nzuri si mlango’

    (c) ‘makaa kujipalia’ badala ya ‘kujipalia makaa‘,

    ‘madhara kukadiria’ badala ya ‘kukadiria madhara’

    ‘mapoda kumichia’ badala ya ‘kumichia mapoda’

    iv. Mazida – ‘vyang’aria’ badala ya ‘vyang’ara’

    v. Utohozi – Sitoria – histori

    Mazida na utohozi zimetumiwa kuleta urari wa vina

    Mbinu (4 x 2 = 8)

    Kutaja – alama 1

    Kufafanua, au mfano – alama 1

    (c) Pande mbili ambazo mshairi anascma nazo ni:

     

  • Vijana (ubeti 1 – 8) 
  • Mungu (ubeti 9)(2 x l = 2)

    (d) Umuhimu wa maswali ya balagha.

     

  • Maswali ya balagha ambayo yanalenga msomaji wa kazi ya fasihi hunuiwa kumfanya kulitafakad jambo hivyo kujifunza kwalo.
  • Humfanya msonaji kulidadisi jambo linaloibuliwa. Katika ubeti wa sita msomaji atavuta fikra kuhusu ‘faida’ ya kuingia kwenye anasa ya kumuua.
  • Kwa kulidadisi hili ataona kuwa hamna faida na hivyo kujirudi.
  • Hutumiwa kusuta watu au kukashifu jambo. Ubeti wa 5 unawakashifu waliopapia anasa na kuwatahadharisha wasomaji kwa kuonyesha kuwa hatima ya anasa ni kifo. 
  • Hutumiwa kusisitiza wazo au kumfanya msomaji kushawishika na mtazamo wa msanii. Kwa mfano, katika ubeti we 6, mshairi anamshawishi msomaji kwamba hakuna faida ya kuingilia anasa.
  • Hutumiwa kuzindua. Ubeti wa 5 unamzindua msomayi kuona kuwa hata wenye nguvu huangamizwa na zinaa(3 x 1 = 3)

    d.Toni ya huzuni kusikitika i . Anasikitikia maclhara yatakayowapata wanaoingilia, zinaa kwa kauli kama vile ‘wawapi leo madume, anasa walopapia”.7(ubeti5)

    Au ii.Toni ya kunasihi au kushawishi. Anawasihi vijana kuepuka zinaa. Kwa mfano anawaambia, “kikiki ikaze kamba, u kijana vumilia”. (ubeti 7)

    iii.Kukejeli/kudharau/stihizai/bezo.

    iv.Uchungu – anaonea uchungu tabia ya vyana.

    Kulaja – alama 1

    Kueleza na kutoa mfano – alama 2

    (1 x 3 = 3)

    8.a) Mandhari ni nyumbani mwa Mzee Babu.

    Wanatekede wamekusanyika kwa Mzee Babu kujadili kuhusu mabadiliko ya hali ya anga.

    Bi Cherehani na Bwana Pima ambao ndio washona kikaza wamo kikaoni.

    Bwana Machupa amemwomba mzee Babu kuwafafanulia kitendawili cha hali hii ya anga Mzee Babu anawaambia wanakijiji wawaulize washona kikaza. (Cherehani na Pima)

    Wanapoulizwa hawatoi jibu la kuridhisha, wanasema ndio mtindo na walifuata mLindO.

    (4 x l=4)

    Tanbihi

    Dondoo limetolewa uk. 42

    b) Maneno kiini katika swali hili ni wanavyofuata mitindo na kuacha chungu kinatokota bila kuivisha

    Watahiniwa wanaweza kulifasiri swali kwa nan-ma zifuatazo:

     

  • Watu/viongozi kutoshughulikia hali inayowakabili
  • Viongozi kufuata mitindo ya uongozi ya viongozi watangulizi badala ya kuiboresha
  • Walu kufumbia macho makosa ya viongozi
  • Viongozi kusaliti nafasi yao kwa kuendeleza uovu na uharibifu badala ya kuukosoa, nk.
  • Viongozi na raia kuendelcza vitendo na hali hasi kama vile tamaa na ubinafsi
  • Raia kuwawekea vikwazo viongozi na kungojea waporomoke.Hoja zifuatazo zinaweza kujitokeza.

     

  • Kobe anachangiwa manyoya na ndege kupaa angani lakini wanapofika anakula wanavyopewa bila kuwagawia waliomkweza ila waliobahatika kupata makombo.
  • Mtajika anahujumu demokrasia kwa kupata kura kwa iijia ya udanganyifu;
  • Mtajika hafanyi lolote kutatua shida za wanakijiji. Tunaambiwa mambo yakiwa mabaya hasemi lolote kwani ameshapata aliyotaka.
  • Viongozi wanawasaliti washona kikaza (wapiga kura) kwa kuwadharau, kuwapuuza na kutowathamini licha ya kwamba ndio waliowachagua.
  • Wanakijiji (raia) wanajua Mtajika amevunja masharti ya kikaza (uongozi) lakini hawamkosoi, wananyamaza, wanayafungia macho makosa ya viongozi.
  • Mtajika anamruhusu mkewe kukishika kikaza (kuingilia uongozi) kinyume na kaida za jamii.
  • Bi Mtajika anavunja kanuni za uhusiano mwema hata katika sherehc. Hata anatamka kuwa hakuna kiongozi mwingine kushinda yeye.
  • Viongozi wanayaharibu mazingira badala ya kuyahifadhi. Tunaambiwa jibu la kitendawili cha mawingu bila maji limo katika kikaza.
  • Machupa ambayc ni msemaji wa wanakijiji si wa kutegemewa. Anafaidika kwa Mtajika. Tunaambiwa kwamba yeye huenda na (huunga) upande unaomfaidi. Tunaambiwa alijua namna ya kuishi.
  • Viongozi wamewatelekeza raia kwenye njaa na magonjwa (uk 47).
  • Mtajika amewaaibisha wanakijiji kwa kutokilinda kikaza (uongozi). Bi Chirenga anasema kikaza kimepasuka.
  • Mtajika na wenzake wanaipora mali ya umma; wanaifukarisha jamii kwa ubinafsi wao. Tunaambiwa kama ni nguruwe walijua kuchagua (uk 47).
  • Raia kutokuwa na uwajibikaji wa pamoja japo wote ni washiriki katika ushonaji wa kikaza (uteuzi wa viongozi). Wanawatarajia Bi Cherehani na Bwana Pima kuelezca kitcndawili cha kutonyesha kwa mvua (uk 42).
  • Raia kutowajibikia vitendo vyao. Wanashiriki katika ushonaji wa kikaza (uteuzi wa viongozi) bila kuwazia uzito wa tendo hili. Wanachagua viongozi ambao wanawaathiri wenyewe (uk 43- 44).
  • Viongozi wanakwezwa uongozini na raia kisha wanawatelekeza pindi tu wanapofika kileleni (istiara ya kobe – na ndege (uk. 44). 
  • Vikaragosi wanashirikiana na viongozi kuwadhulumu wanyonge. Kobe na vibarakala wake wananyakua kila kitu na kuwaachia wachache waliobahatika masalio (uk.44). ‘
  • Raia wanashiriki katika uharibifu wa mazingira na kusababisha kutotegemewa kwa hali ya anga. Mvua, ama inanyesha nyingi kupindukia, au hainyeshi kabisa (uk. 40).
  • Machupa anawaambia wanakijiji kuwa jibu la kitendawili cha wawingu bila maji ni kikaza na raia ndio wenye kupima na kushona kikaza (uk. 46).
  • Viongozi kuendeleza uongo na udanganyifu. Mtajika angeubadilisha ukweli kuwa uongo na uongo kuwa ukweli (uk 44).
  • Badala ya viongozi kushughulikia uhalisia wa mambo, wanaishi katika ulimwengu wa ndoto. Hata nchi inapokumbwa na changamoto, Bwana Mtajika anaota tu badala ya kukabiliana na changamoto zenyewe (uk. 44).
  • Hata raia wanapoutaka ushauri wake, hasemi lolote; ashapala aliyopangia kupala (uk 44).
  • Raia wanaogopa, hivyo wanayafumbia kinywa matendo hasi ya viongozi. Tunaambiwa ni wachache wanaoweza kusema ukweli, hasa unaohusu viongozi (uk. 45).
  • Bwana Mtajika anavunja kaida za kikaza (Kaida za uongozi) na hawamkosoi. Unafiki wa baadhi ya raia unaifanya Tekede kudorora kimaendeleo. Tunaambiwa kuwa Machupa hula kuwili. wasemayo wanakijiji kumpelekea Mtajika na hapohapo anawaonyesha wanakijiji kuwa talizo limo kwenye uongozi. Yeye anajitoa lawamani badala ya kushirikiana na raia kutatua tatjzo la uharibifu wa mazingira (uk. 46).
  • Viongozi wanawalelekeza raia waliowachagua katika njaa, umaskini na ugonjwa. (uk. 47).
  • Bwana Mtajika anashindwa kuulinda uongozi: anashindwa kulidhibiti taifa. Cherehani anasema kwamba ldkaza kimepasuka. Wizi wa mali ya umma unawafanya wafuasi wengine wa Mtajika kutotaka kuonekana hadharani isipokuwa Machupa ambaye anajua namna ya kuishi (uk 47).
  • Hivyo viongozi hawadiriki kutatua matatizo ya raia. Raia wanawawekea viongozi vikwazo vinavyosababisha kuanguka kwao. Cherehani anapunguza kiwango cha kikaza maksudi; kikaza kinapasuka. (uk 48)(8 x 2 = 16)

     

(Visited 205 times, 1 visits today)
Share this:

Written by